Wimbo wa Kusifu | Kutoa Sadaka ya Thamani Sana kwa Mungu

17/04/2020

Baada ya miaka mingi kupita,

mwanadamu amedhoofika,

kwa kuupitia ugumu wa usafishaji na kuadibu.

Ijapokuwa mwanadamu amepoteza “utukufu” na “mapenzi” ya wakati uliopita,

bila ya kufahamu amekuja kuelewa kanuni za tabia ya mwanadamu,

na amekuja kutambua kazi ya Mungu ya kujitolea kuokoa wanadamu,

na amekuja kutambua kazi ya Mungu ya kujitolea kuokoa wanadamu.

Taratibu mwanadamu anaanza kuchukia ushenzi wake mwenyewe.

Anaanza kuchukia jinsi alivyo mkali, na lawama kuelekea kwa Mungu,

na mahitaji yote yasiyokuwa na mwelekeo aliyodai kutoka Kwake.

Wakati hauwezi ukarudishwa nyuma,

matendo ya zamani huwa ya kujuta katika kumbukumbu za mwanadamu,

na maneno na upendo wa Mungu

vinakuwa ndivyo vinavyomwendesha mwanadamu katika maisha Yake mapya.

Wakati hauwezi ukarudishwa nyuma,

matendo ya zamani huwa ya kujuta katika kumbukumbu za mwanadamu,

na maneno na upendo wa Mungu

vinakuwa ndivyo vinavyomwendesha mwanadamu katika maisha Yake mapya.

Majeraha ya mwanadamu hupona siku baada ya siku,

nguvu humrudia, na akasimama na kutazamia uso Wake mwenye Uweza …

ndipo anagundua kuwa daima Ameishi kando yangu,

na kwamba tabasamu Lake na sura Yake ya kupendeza bado zinasisimua.

Moyo Wake bado unawajali wanadamu Aliowaumba,

na mikono Yake bado ina joto na nguvu kama ilivyokuwa hapo mwanzoni.

Ni kama mwanadamu alirudi kwenye bustani ya Edeni,

lakini wakati huu mwanadamu hasikizi ushawishi wa nyoka,

na hatazami kando na uso wa Yehova.

Mwanadamu anapiga magoti mbele ya Mungu,

na kutazama uso Wake wenye tabasamu,

na kumtolea Mungu kafara yenye thamani—

Ee! Bwana wangu, Mungu wangu!

Mwanadamu anapiga magoti mbele ya Mungu,

na kutazama uso Wake wenye tabasamu,

na kumtolea Mungu kafara yenye thamani—

Ee! Bwana wangu, Mungu wangu!

Mwanadamu anapiga magoti mbele ya Mungu,

na kutazama uso Wake wenye tabasamu,

na kumtolea Mungu kafara yenye thamani—

Ee! Bwana wangu, Mungu wangu!

Ee! Bwana wangu, Mungu wangu!

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp