Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 162

31/07/2020

Watu wengine watauliza, “Nini tofauti kati ya kazi aliyoifanya Mungu wa mwili na ile ya manabii na mitume wa zamani?” Daudi pia aliitwa Bwana, na hivyo pia akawa Yesu; ingawa kazi waliyoifanya ilikuwa tofauti, waliitwa kitu kimoja. Mbona, unauliza, hawakuwa na utambulisho mmoja? Kile Yohana alichoshuhudia kilikuwa maono, moja iliyotoka pia kwa Roho Mtakatifu, na aliweza kuyasema maneno ambayo Roho Mtakatifu alikusudia kuyasema; kwa nini utambulisho wa Yohana ni tofauti na ule wa Yesu? Maneno aliyoyasema Yesu yaliweza kumwakilisha Mungu kikamilifu, na kuwakilisha kikamilifu kazi ya Mungu. Kile alichokiona Yohana kilikuwa maono, na hakuweza kuwakilisha kikamilifu kazi ya Mungu. Ni kwa nini Yohana, Petro na Paulo walizungumza maneno mengi—kama alivyofanya Yesu—lakini bado hawakuwa na utambulisho sawa na Yesu? Ni hasa kwa sababu kazi waliyoifanya ilikuwa tofauti. Yesu aliwakilisha Roho wa Mungu, na Alikuwa Roho wa Mungu Akifanya kazi moja kwa moja. Alifanya kazi ya enzi mpya, kazi ambayo hakuna aliyekuwa amefanya mbeleni. Yeye Alifungua njia mpya, Alimwakilisha Yehova, na Alimwakilisha Mungu Mwenyewe. Ilhali kwa Petro, Paulo na Daudi, bila kujali walichoitwa, waliwakilisha tu utambulisho wa kiumbe wa Mungu, ama walitumwa na Yesu na Yehova. Kwa hivyo bila kujali kiasi cha kazi walichofanya, bila kujali jinsi walivyofanya miujiza kubwa, walikuwa bado tu viumbe wa Mungu, na hawakuweza kuwakilisha Roho Mtakatifu. Walifanya kazi kwa jina la Mungu ama baada ya kutumwa na Mungu; zaidi ya hayo, walifanya kazi katika enzi iliyoanzishwa na Yesu ama Yehova, na kazi waliyoifanya haikutengwa. Walikuwa, hatimaye, viumbe wa Mungu tu. Katika Agano la Kale, manabii wengi walizungumza utabiri, ama kuandika vitabu vya unabii. Hakuna aliyesema kuwa yeye ni Mungu, lakini punde tu Yesu Alipojitokeza, kabla yeye kutamka neno lolote, Roho wa Mungu Alimshuhudia kuwa Yeye ni Mungu. Mbona hivyo? Kwa sasa, unapaswa kujua tayari! Awali, mitume na manabii waliandika nyaraka mbalimbali, na kufanya unabii mwingi. Baadaye, watu walichagua baadhi zao kuweka katika Biblia, na baadhi zikapotea. Kwa vile kuna watu wanaosema kuwa vitu vyote wanavyozungumza vimetoka kwa Roho Mtakatifu, mbona baadhi yavyo vinachukuliwa kuwa nzuri, na baadhi yavyo vinachukuliwa kuwa mbaya? Na mbona baadhi vilichaguliwa, na sio vingine? Kama kweli yalikuwa maneno Aliyoyasema Roho Mtakatifu, ingekuwa lazima kwa watu kuyachagua? Kwa nini akaunti ya maneno yaliyosemwa na Yesu na kazi Aliyoifanya ni tofauti katika kila moja ya Injili Nne? Makosa sio ya waliyoyarekodi? Watu wengine watauliza, “Sababu nyaraka zilizoandikwa na Paulo na waandishi wengine wa Agano Jipya na kazi walizozifanya zilitokana kidogo na matakwa ya mwanadamu, na zilichanganywa na dhana za mwanadamu, basi hakuna uchafu wa binadamu katika maneno ambayo Wewe (Mungu) unazungumza leo? Je, kweli hayana dhana hata moja za mwanadamu?” Hii hatua ya kazi aliyoifanya Mungu ni tofauti kabisa na zile walizozifanya Paulo na wengi wa mitume na manabii. Sio tu kwamba kuna tofauti na utambulisho, lakini, hasa, kuna tofauti kati ya kazi inayofanywa. Baada ya Paulo kupigwa chini na kuanguka mbele ya Bwana, aliongozwa na Roho Mtakatifu kufanya kazi, na akawa mtume. Na hivyo akaandikia makanisa nyaraka, na hizi nyaraka zote zilifuata mafundisho ya Yesu. Paulo alitumwa na Bwana kufanya kazi kwa jina la Bwana Yesu, lakini Mungu Mwenyewe alipokuja, Hakufanya kazi kwa jina lolote na Hakuwakilisha yeyote isipokuwa Roho wa Mungu katika kazi Yake. Mungu alikuja kufanya kazi Yake moja kwa moja: Hakukamilishwa na mwanadamu, na kazi Yake haikufanywa juu ya mafundisho ya mwanadamu yeyote. Katika hatua hii ya kazi Mungu haongozi kwa kuzungumza juu ya uzoefu Wake binafsi, ila Hufanya kazi Yake moja kwa moja, kulingana na Alicho nacho. Kwa mfano, Anafanya kazi ya watoa huduma, wa nyakati za kuadibu, kazi ya kifo, ya kumpenda Mungu…. Hii yote ni kazi ambayo haijawahi kufanywa mbeleni, na ni kazi ya enzi ya sasa, badala ya uzoefu wa binadamu. Kwa maneno Nimesema, ni yapi mazoefu ya mwanadamu? Je, yote hayatoki moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu, na hayatolewi nje na Roho Mtakatifu? Ni vile tu aina yako ni maskini sana hadi huwezi kuona kupitia ukweli! Maisha ya vitendo Ninayozungumzia ni ya kuongoza njia, na hayajawahi zungumziwa na yeyote mbeleni, wala hakuna aliye na uzoefu wa njia hii, wala kujua ukweli huu. Kabla Niliyatamka maneno haya, hakuna aliyewahi kuyasema. Hakuna aliyezungumzia mazoefu haya, wala hakuna aliyewahi kusema maelezo hayo, na, zaidi ya hayo, hakuna aliyewahi kuonyesha hali kama hizo kufichua mambo haya. Hakuna aliyewahi kuongoza njia Ninayoongoza leo, na kama ingeongozwa na mwanadamu, basi isingekuwa njia mpya. Chukua Paulo na Petro, kwa mfano. Hawakuwa na mazoefu yao binafsi kabla ya kutembelea njia iliyoongozwa na Yesu. Ilikuwa tu baada ya Yesu kuongoza njia ndipo walipopata uzoefu wa maneno aliyoyasema Yesu, na njia aliyoiongoza; kutoka hapa walipata mazoefu mengi, na kuziandika nyaraka, Na hivyo, uzoefu wa mwanadamu sio sawa na kazi Ya Mungu, na kazi ya Mungu sio sawa na maarifa yalivyoelezwa na dhana na uzoefu wa mwanadamu. Nimesema, tena na tena, kuwa leo Ninaongoza njia mpya, na kufanya kazi mpya, na kazi na matamshi Yangu ni tofauti na yale ya Yohana na wale manabii wengine wote. Kamwe, Sijawahi pata uzoefu kwanza, na kisha kuyazungumzia kwenu—hiyo sio ukweli hata kidogo. Kama ingekuwa hivyo, haingewachelewesha kitambo sana? Zamani, maarifa waliyoyazungumzia wengi yalipandishwa cheo pia, lakini maneno yao yote yalisemwa tu kulingana na hayo ya wanaoitwa takwimu wa kiroho. Hawakuiongoza njia, lakini walitoka kwa uzoefu wao, walitoka kwa walichokiona, na kwa maarifa yao. Zingine zilikuwa dhana zao, na mengine yalikuwa mazoefu waliyofupisha. Leo, asili ya kazi Yangu ni tofauti kabisa na yao. Sijapata uzoefu wa kuongozwa na wengine, wala Sijakubali kukamilishwa na wengine. Zaidi ya hayo, yote Nimesema na kushiriki ni tofauti na yale ya wengine, na hayajawahi kuzungumzwa na mwengine yeyote. Leo, bila kujali ninyi ni nani, kazi yenu inafanywa kulingana na maneno Nisemayo. Bila haya matamshi na kazi, nani angeweza kupata uzoefu wa mambo haya (majaribu ya watendaji huduma, nyakati za kuadibu…), na nani ataweza kuzungumzia maarifa kama haya? Kweli huna uwezo wa kuona haya? Bila kujali hatua ya kazi, punde tu maneno Yangu yasemwapo, mnaanza kushiriki kulingana na maneno Yangu, na kufanya kazi kulingana nayo, na sio njia ambayo yeyote kati yenu amefikiria. Baada ya kuja mbali hivi, huna uwezo wa kuona swali wazi na rahisi hivi? Sio njia iliyowazwa na yeyote, wala haijalinganishwa na mtu yeyote wa kiroho. Ni njia mpya, na hata maneno mengi yaliyosemwa mara kwanza na Yesu hayatumiki tena. Ninachozungumza ni kazi ya kufungua enzi mpya, na ni kazi inayosimama peke yake; kazi Nifanyayo, na maneno Nizungumzayo, yote ni mapya. Si hii ndiyo kazi mpya ya leo? Kazi ya Yesu pia ilikuwa hivi. Kazi Yake pia ilikuwa tofauti na hizo za watu wengine hekaluni, na pia ilitofautiana na kazi za Mafarisayo, na wala haikufanana na zilizofanywa na watu wote wa Israeli. Baada ya kuishuhudia, watu walishindwa kuamua: Kweli ilifanywa na Mungu? Yesu hakuzingatia sheria ya Yehova; Alipokuja kumfunza mwanadamu, yote Aliyoyanena yalikuwa mapya na tofauti na yale yaliyosemwa na watakatifu wa zamani na manabii wa Agano la Kale, na kwa sababu hii, watu walisalia bila uhakika. Hii ndiyo humfanya mwanadamu kuwa mgumu sana kushughulika naye. Kabla ya kukubali hii hatua mpya ya kazi, njia ambayo wengi wenu walitembelea ilikuwa ya kutenda na kuingia katika msingi wa watu hao wa kiroho. Lakini leo, kazi Ninayoifanya ni tofauti sana, na hivyo hamna uwezo wa kuamua kama ni sawa ama sio. Sijalishwi na njia uliyopitia mbeleni, wala Sijali ulikula chakula cha nani, ama uliyemchukua kama “babako.” Sababu Nimekuja na kuleta kazi mpya ya kumwongoza mwanadamu, wote wanaonifuata lazima watende kulingana na Ninachosema. Bila kujali jinsi ulivyotoka “familia” ya nguvu, lazima unifuate, hupaswi kutenda kulingana na mazoea yako ya awali, “Baba wa kambo” wako anapaswa kushuka nawe unapaswa kuja mbele ya Mungu wako kupata mgao wako halali. Uzima wako wote umo mikononi Mwangu, nawe hupaswi kuwa na imani kipofu nyingi kwa baba wako wa kambo, hawezi kukutawala kabisa. Kazi ya leo inasimama peke yake. Yote Nisemayo leo ni wazi hayajalinganishwa na msingi wa zamani; ni mwanzo mpya, na ukisema kuwa umetengenezwa na mkono wa mwanadamu, basi wewe ni mmoja wa wale ambao hawawezi tibiwa upofu wao!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp