Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 177

18/08/2020

Hapo mwanzo, tulizungumza kuhusu mazingira ya kuishi ya wanadamu na kile Mungu alifanya, alitayarisha, na kushughulikia kwa ajili ya mazingira haya, na vilevile mahusiano kati ya vitu vyote ambavyo Mungu aliwatayarishia wanadamu na jinsi Mungu alishughulikia mahusiano haya yote kuzuia vitu vyote kuleta madhara kwa wanadamu. Mungu pia alitatua athari hasi katika mazingira ya wanadamu zilizosababishwa na vitu mbalimbali vya asili ambavyo vinaletwa na mambo yote, Akaruhusu vitu vyote kuongeza hadi upeo shughuli za vitu hivyo, na Akawaletea wanadamu mazingira ya kufaa na vitu vyote vya asili vyenye manufaa, kuwawezesha wanadamu kuwa wepesi kubadilika kwa mazingira hayo na kuendelea na mfuatano wa kuzaa na wa maisha kwa kawaida. Kilichofuata kilikuwa chakula kilichohitajika na mwili wa mwanadamu—chakula cha kila siku na kinywaji. Hii pia ni hali muhimu ya kuendelea kuishi kwa mwanadamu. Hiyo ni kusema, mwili wa mwanadamu hauwezi kuishi tu kwa kupumua, kuwa na mwangaza wa jua au upepo pekee, au halijoto za kufaa tu. Wanahitaji pia kujaza matumbo yao. Vitu hivi vya kujaza matumbo yao vyote vimetayarishwa pia na Mungu kwa ajili ya wanadamu—hiki ni chanzo cha chakula cha wanadamu. Baada ya kuona mazao haya ya fahari na mengi—vyanzo vya chakula cha wanadamu na kinywaji—unaweza kusema kwamba Mungu ni chanzo cha kupeana wanadamu na vitu vyote? (Ndiyo.) Ikiwa Mungu angeumba tu miti na nyasi au hata viumbe mbalimbali vyenye uhai Alipoumba vitu vyote, na wanadamu hawangekula chochote kati ya hivyo, je, wanadamu wangeweza kuendelea kuishi hadi wakati huu? Na je, viumbe mbalimbali vyenye uhai na mimea miongoni mwa vitu vyote ambavyo Mungu aliumba vingekuwa vya ng’ombe na kondoo kula, au vya pundamilia, paa na aina nyingine mbalimbali za wanyama—kwa mfano, simba wale chakula kama pundamilia na paa, chui wakubwa wenye milia wale chakula kama wanakondoo na nguruwe—lakini kusiwe na hata kitu kimoja cha kufaa wanadamu kula? Je, hilo lingefaulu? Halingefaulu. Wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi. Na je, wanadamu wangekula tu majani ya miti? Hilo lingefaulu? Matumbo ya wanadamu hayangeweza kustahimili. Huwezi kujua usipojaribu, lakini mara unapofanya hivyo utajua vizuri sana. Basi ungeweza kula nyasi ambayo kondoo hutayarishiwa? Huenda ikawa sawa ukijaribu kidogo tu, lakini ukiendelea kula kwa muda mrefu, hutadumu kwa muda mrefu. Na hata kuna vitu vingine ambavyo vinaweza kuliwa na wanyama, lakini wanadamu wakivila watapata sumu. Kuna vitu vingine vyenye sumu ambavyo wanyama wanaweza kuvila bila kuathiriwa, lakini wanadamu hawawezi kufanya vivyo hivyo. Kwa maneno mengine, Mungu aliwaumba wanadamu, hivyo Mungu anajua vizuri sana kanuni na muundo wa mwili wa mwanadamu na wanachohitaji wanadamu. Mungu ana hakika kamili kuhusu sehemu na vijenzi vyake, na inachohitaji, vilevile jinsi sehemu za ndani ya mwili wa mwanadamu hufanya kazi, hufyonza, huondosha, na kuvunjavunja kemikali mwilini. Watu hawana hakika kuhusu hili na wakati mwingine hula na kujaliza bila kujua. Wao hujaliza kupita kiasi na mwisho husababisha kutolingana nguvu. Ukila na kufurahia vitu hivi alivyokutayarishia Mungu kwa kawaida, hutakuwa na shida yoyote. Hata kama wakati mwingine una hali mbaya ya moyo na una ukwamaji wa damu, haidhuru. Unahitaji tu kula aina fulani ya mmea na ukwamaji utatatuliwa. Mungu ametayarisha vitu hivi vyote. Kwa hivyo, machoni mwa Mungu, wanadamu wako juu zaidi ya kiumbe chochote chengine chenye uhai. Mungu alitayarishia kila aina ya mimea mazingira ya kuishi na Akatayarishia kila aina ya wanyama chakula na mazingira ya kuishi, lakini mahitaji ya wanadamu pekee kwa mazingira yao ya kuishi ndiyo makali zaidi na yasiyostahamili kutotunzwa. La sivyo, wanadamu hawangeweza kuendelea kukua na kuzaa na kuishi kwa kawaida. Mungu anajua hili vizuri zaidi moyoni Mwake. Mungu alipofanya hili, alilipa umuhimu zaidi kuliko kitu chengine chochote. Labda huwezi kuhisi umuhimu wa kitu fulani kisicho na maana unachokiona na kufurahia au kitu unachohisi ulizaliwa nacho na unaweza kufurahia, lakini Mungu alikuwa tayari amekutayarishia zamani sana kwa hekima Yake. Mungu ameondoa na kutatua kwa kiwango kikubwa zaidi iwezekanavyo vipengele vyote hasi visivyofaa kwa wanadamu na vinavyoweza kudhuru mwili wa mwanadamu. Nini ambacho hiki kinaweka wazi? Je, kinahakikisha mtazamo wa Mungu kwa wanadamu Alipowaumba wakati huu? Mtazamo huo ulikuwa upi? Mtazamo wa Mungu ulikuwa wa msimamo na maana kubwa, na Hakustahimili kuingilia kati kwa vipengele au hali au nguvu zozote za adui isipokuwa Mungu. Kutokana na hili, unaweza kuona mtazamo wa Mungu alipoumba wanadamu na katika usimamizi Wake wa wanadamu wakati huu. Mtazamo wa Mungu ni upi? Kupitia kwa mazingira ya kuishi na kuendelea kuishi ambayo wanadamu wanafurahia pamoja na chakula chao cha kila siku na kinywaji na mahitaji ya kila siku, tunaweza kuona mtazamo wa Mungu wa wajibu kwao wanadamu ambao Anao tangu Awaumbe, na vilevile uamuzi wa Mungu wa kuwaokoa wanadamu wakati huu. Je, tunaweza kuona uhalisi wa Mungu kupitia kwa haya yote? Tunaweza kuona ustaajabishaji wa Mungu? Tunaweza kuona kutoweza kueleweka kwa Mungu? Tunaweza kuona kudura ya Mungu? Mungu anatumia tu njia Zake za uweza na hekima kuwapa wanadamu wote, na vilevile kuvipa vitu vyote. Licha ya hayo, baada ya Mimi kusema mengi sana, mnaweza kusema kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote? (Ndiyo.) Hili ni hakika. Je, mna shaka yoyote? (La.) Upeanaji wa Mungu wa vitu vyote ni wa kutosha kuonyesha kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote, kwa sababu Yeye ni chanzo cha upeanaji ambao umewezesha vitu vyote kuwepo, kuishi, kuzaa, na kuendelea. Mbali na Mungu hakuna mwingine. Mungu hupeana mahitaji yote ya vitu vyote na mahitaji yote ya wanadamu, bila kujali iwapo ni hitaji la msingi kabisa, wanachohitaji watu kila siku, au upeanaji wa ukweli kwa roho za watu. Kutokana na mitazamo yote, inapofikia utambulisho wa Mungu na hadhi Yake kwa wanadamu, ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Hili ni sahihi? (Ndiyo.) Yaani, Mungu ni Mtawala, Bwana, na Mpaji wa dunia hii yakinifu ambayo watu wanaweza kuona kwa macho yao na kuhisi. Kwa wanadamu, je, huu si utambulisho wa Mungu? Hii ni kweli kabisa. Hivyo unapoona ndege wakiruka angani, unapaswa kujua kwamba Mungu aliumba vitu vinavyoweza kuruka. Lakini kuna viumbe vyenye uhai vinavyoogelea majini, navyo pia huendelea kuishi kwa njia mbalimbali. Miti na mimea inayoishi ndani ya udongo huchipuka katika majira ya kuchipuka na huzaa matunda na kupoteza majani katika majira ya kupukutika kwa majani, na ifikapo wakati wa majira ya baridi majani yote huwa yameanguka na kupitia katika majira ya baridi. Hiyo ni njia yao ya kuendelea kuishi. Mungu aliumba vitu vyote, na kila kimojawapo huishi kupitia taratibu mbalimbali na njia mbalimbali na hutumia mbinu mbalimbali kuonyesha nguvu zake na taratibu ya maisha. Haijalishi ni mbinu gani, yote iko chini ya utawala wa Mungu. Ni nini kusudi la Mungu la kutawala taratibu zote mbalimbali za maisha na viumbe vyenye uhai? Je, ni kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu? (Ndiyo.) Anadhibiti sheria zote za maisha kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hii inaonyesha hasa vile kuendelea kuishi kwa wanadamu ni muhimu kwa Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp