Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 164

26/07/2020

Sasa uelewa wenu wa utambuzi kuhusu kiini cha Mungu bado unahitaji kipindi cha muda mrefu kujifunza, kuthibitisha, kuhisi na kuipitia, hadi siku moja mtajua utakatifu wa Mungu kutoka katikati ya moyo wenu kuwa kiini cha Mungu ambacho hakina dosari, upendo wa Mungu usio na ubinafsi, kwamba haya yote Mungu humpa mwanadamu hayana ubinafsi, na mtakuja kujua ya kwamba utakatifu wa Mungu hauna dosari wala haushutumiki. Hivi viini vya Mungu si maneno tu ambayo Yeye hutumia kuonyesha utambulisho Wake, bali Mungu hutumia kiini Chake kwa kimya na kwa dhati kushughulika na kila mtu. Kwa maneno mengine, kiini cha Mungu si tupu, wala si cha nadharia au mafundisho ya dini na hakika si aina ya maarifa. Si aina ya elimu kwa mwanadamu, lakini badala yake ni ufunuo wa kweli wa matendo ya Mungu mwenyewe na ni kiini ambacho kimefichuliwa cha kile Mungu anacho na alicho. Binadamu anapaswa kujua kiini hiki na kukifahamu, kwa kuwa kila kitu Mungu hufanya na kila neno Yeye husema ni la thamani kubwa na umuhimu mkubwa kwa kila mtu. Unapokuja kuelewa utakatifu wa Mungu, basi unaweza kweli kumwamini Mungu; unapokuja kuelewa utakatifu wa Mungu, basi unaweza kweli kutambua maana halisi ya maneno haya “Mungu Mwenyewe, wa Kipekee.” Hutafikiria tena kwamba unaweza kuchagua kutembea njia zingine, na hutakuwa tena radhi kusaliti kila kitu ambacho Mungu amekupangia. Kwa sababu kiini cha Mungu ni takatifu, hiyo ina maana kwamba kupitia tu Mungu ndipo unaweza kutembea njia yenye kung’aa na sahihi katika maisha; ni kupitia tu Mungu unaweza kujua maana ya maisha, ni tu kupitia Mungu unaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha halisi, kumiliki ukweli, kujua ukweli, na ni kupitia tu Mungu unaweza kupata maisha kutoka kwa kweli. Ni Mungu Mwenyewe tu anaweza kukusaidia kuepuka maovu na kukuokoa kutoka kwa madhara na udhibiti wa Shetani. Kando na Mungu, hakuna mtu au kitu kinaweza kukuokoa kutoka kwa bahari ya mateso, ili usiteseke tena: Hili linaamuliwa na kiini cha Mungu. Ni Mungu Mwenyewe tu hukuokoa bila ubinafsi wowote, ni Mungu pekee anayehusika na maisha yako ya baadaye, na hatima yako na maisha yako, na Yeye anapanga mambo yote kwa ajili yako. Hili ni jambo ambalo hakuna kitu ambacho kimeumbwa au hakijaumbwa kinaweza kutimiza. Kwa sababu hakuna kitu ambacho kimeumbwa au hakijaumbwa kina kiini cha Mungu kama hiki, hakuna mtu au kitu kina uwezo wa kukuokoa au kukuongoza wewe. Huu ndio umuhimu wa kiini cha Mungu kwa mwanadamu. Labda mnahisi kuwa maneno haya Niliyoyasema yanaweza kweli kusaidia kimsingi katika kanuni. Lakini kama wewe unafuatilia ukweli, kama wewe unapenda ukweli, katika uzoefu wako wa baada ya hapa maneno haya hayataleta tu mabadiliko katika hatima yako, lakini zaidi ya hayo yatakuleta kwa njia sahihi ya maisha.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp