Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 158

03/08/2020

Shetani hutumia mienendo ya kijamii kumpotosha mwanadamu. Hii mienendo ya kijamii ina mambo mengi. Watu wengine husema: “Je, ni kuhusu nguo tunazovaa? Je, ni kuhusu mtindo wa karibuni, vipodozi, kutengeneza nywele na chakula cha kidomo?” Je, ni kuhusu mambo haya? Hii ni sehemu ya mienendo, lakini hatutaki kuzungumzia haya hapa. Tunataka tu kuzungumza kuhusu mawazo ambayo mienendo ya kijamii inaleta kwa watu, jinsi inasababisha watu kutenda duniani, malengo ya maisha na mtazamo ambao inaleta kwa watu. Hii ni muhimu sana: inaweza kudhibiti na kushawishi hali ya akili ya mwanadamu. Moja baada ya nyingine, hii mienendo yote inabeba ushawishi mwovu unaoendelea kumpotosha mwanadamu, kumfanya kuendelea kupoteza dhamiri, ubinadamu na mantiki, na unaoshukisha maadili yao na ubora wao wa tabia zaidi na zaidi, hadi kwa kiwango ambamo tunaweza hata kusema wengi wa watu sasa hawana uadilifu, hawana ubinadamu, wala hawana dhamiri yoyote, wala akili yoyote. Hivyo mienendo hii ni ipi? Huwezi kuona mienendo hii kwa macho. Wakati upepo wa mwenendo unavuma, pengine ni idadi ndogo ya watu tu watakuwa waanzisha mitindo. Wanaanza kwa kufanya jambo la aina hii, kukubali wazo la aina hii ama mtazamo wa aina hii. Wengi wa watu, hata hivyo, katikati ya kutojua kwao, bado watazidi kuambukizwa, kufanywa wenyeji na kuvutia na aina hii ya mwenendo, hadi wote bila kujua na bila kujitolea wanamkubali, na wote wanazama na kudhibitiwa na yeye. Kwa mwanadamu ambaye si wa mwili na akili timamu, ambaye kamwe hajui ukweli, ambaye hawezi kusema tofauti kati ya vitu vyema na hasi, mienendo ya aina hii moja baada ya nyingine inawafanya wote wawe radhi kukubali mienendo hii, mtazamo wa maisha, na maadili yatokayo kwa Shetani. Wanakubali anachowaambia Shetani juu ya jinsi ya kukaribia maisha na jinsi ya kuishi ambayo Shetani “amewapa.” Hawana nguvu, wala hawana uwezo, wala ufahamu wa kupinga. Kwa hivyo hii mienendo hasa ni nini? Nimechukua mfano rahisi ambao mnaweza kuja kuelewa. Kwa mfano, watu wa kale waliendesha biashara zao kwa njia ambayo haikudanganya wazee wala vijana, na ambayo iliuza bidhaa kwa bei sawa bila kujali aliyekuwa akinunua. Je, dokezo la dhamiri na ubinadamu haliwasilishwi hapa? Wakati watu walitumia aina hii ya imani walipokuwa wakifanya biashara zao, inaonyesha kwamba bado walikuwa na baadhi ya dhamiri, baadhi ya ubinadamu wakati huo. Lakini na mahitaji ya mwanadamu ya kiasi kinachopanda daima cha pesa, watu bila kujua walikuja kupenda pesa, hupenda faida na hupenda raha zaidi na zaidi. Kwa hivyo watu walikuja kuona pesa kuwa muhimu zaidi? Wakati watu wanaona pesa kuwa muhimu zaidi, bila kujua wanapuuza sifa, umashuhuri wao, ufahari, na uadilifu wao; wanapuuza mambo haya yote, sivyo? Unapojihusisha katika biashara, unaona mtu mwingine akichukua mbinu tofauti na kutumia njia mbalimbali kuibia watu na kuwa tajiri. Ingawa pesa iliyopatwa ni faida iliyopatwa vibaya, wanakuwa tajiri zaidi na zaidi. Wanajihusisha na biashara sawa na wewe, lakini familia yao yote inafurahia maisha kukuliko, na unahisi vibaya, ukisema: “Mbona siwezi kufanya hivyo? Mbona siwezi kupata kama wapatavyo? Ni lazima nifikirie njia ya kupata pesa zaidi, kufanya biashara yangu kufanikiwa.” Kisha unafikiria hili. Kulingana na mbinu ya kawaida ya kutengeneza pesa, kutodanganya wazee wala vijana na kuuza vitu kwa bei sawa kwa wote, pesa unayotengeneza ni kwa dhamiri nzuri, lakini haiwezi kukufanya kuwa tajiri haraka. Hata hivyo, chini ya tamaa ya kutengeneza faida, kufikiria kwako kunapitia mabadiliko taratibu. Katika mabadiliko haya, kanuni zako za tabia pia zinaanza kubadilika. Wakati unamdanganya mtu kwa mara ya kwanza, unapomlaghai mtu kwa mara ya kwanza, una mashaka, ukisema “Hii ni mara ya mwisho namdanganya mtu na sitafanya hivyo tena. Siwezi kudanganya watu. Kudanganya watu kutapata tu adhabu na kutaleta majanga kwangu! Hii ni mara ya mwisho namdanganya mtu na sitafanya hivyo tena.” Unapomdanganya mtu kwa mara ya kwanza, moyo wako una aibu kiasi; hii ndiyo kazi ya dhamiri ya mwanadamu—kuwa na aibu na kukushutumu, ili ihisi kuwa siyo asili wakati unamdanganya mtu. Lakini baada ya wewe kufanikiwa kumdanganya mtu unaona kwamba sasa una pesa zaidi kuliko awali, na unafikiria mbinu hii inaweza kuwa ya manufaa sana kwako. Licha ya maumivu madogo ndani ya moyo wako, bado unahisi kujipongeza kwa mafanikio yako, na unahisi kuridhishwa kidogo na wewe mwenyewe. Kwa mara ya kwanza, unakubali tabia yako mwenyewe na unakubali uwongo wako mwenyewe. Baadaye, wakati mwanadamu amechafuliwa na kudanganywa huku, ni sawa na mtu ambaye anahusika na kamari na kisha anakuwa mchezaji kamari. Katika kutoelewa, anapenda tabia yake ya kudanganya na anaikubali. Katika kutoelewa, anachukua kudanganya kuwa tabia halali ya kibiashara, na anachukua kudanganya kuwa mbinu ya manufaa zaidi ya kusalimika kwake na maisha yake; anafikiria kwamba kwa kufanya hivi anaweza kuwa tajiri haraka. Mwanzoni mwa mchakato huu watu hawawezi kukubali tabia ya aina hii, wanadharau tabia hii na njia hii ya kufanya mambo, kisha wanajaribu tabia hii wao wenyewe, na kuijaribu kwa njia yao wenyewe, na kisha mioyo yao inaanza kubadilika polepole. Kwa hivyo mabadiliko haya ni yapi? Ni kukubali na kukiri mwenendo huu, kukiri na kukubali wazo hili lililoingizwa kwako na mwenendo wa jamii. Katika kutoelewa, unahisi kwamba usipodanganya katika biashara basi utapata hasara, kwamba usipodanganya basi utakuwa umepoteza kitu. Bila kujua, kudanganya huku kunakuwa nafsi yako, tegemeo kuu lako, na pia kunakuwa aina ya tabia ambayo ni kanuni isiyoweza kutupiliwa mbali katika maisha yako. Baada ya mwanadamu kukubali tabia hii na kufikiria huku, je, moyo wa mwanadamu unapitia mabadiliko? Moyo wako umebadilika, basi uadilifu wako umebadilika? Ubinadamu wako umebadilika? (Ndiyo.) Basi dhamiri yako imebadilika? (Ndiyo.) Uwepo wote wa mwanadamu unapitia mabadiliko bora, kutoka kwa mioyo yao hadi kwa mawazo yao, hadi kwa kiwango ambapo wanabadilika kutoka ndani hadi nje. Mabadiliko haya yanakuweka mbali na mbali zaidi kutoka kwa Mungu, na unakuwa na uafikiano zaidi na zaidi na Shetani, unakuwa sawa zaidi na zaidi na yeye.

Sasa mienendo hii ya kijamii ni rahisi kwako kuelewa. Nilichagua tu mfano rahisi, mfano unaoonekana kawaida ambao watu watakuwa wanajua. Hii mienendo ya kijamii ina ushawishi mkubwa kwa watu? (Ndiyo.) Kwa hivyo hii mienendo ya kijamii ina athari inayodhuru kwa kina kwa watu? (Ndiyo.) Athari ya kudhuru kwa kina kwa watu. Shetani hutumia moja ya mienendo hii ya kijamii baada ya nyingine kupotosha nini ya mwanadamu? (Dhamiri, akili, ubinadamu, maadili.) Nini tena? (Mtazamo wa mwanadamu wa maisha.) Je, inasababisha kuzorota polepole ndani ya watu? (Ndiyo.) Shetani hutumia hii mienendo ya kijamii kuvuta watu hatua moja baada ya nyingine hadi katika kiota cha mashetani, ili watu walionaswa katika mienendo ya kijamii bila kujua wanatetea pesa na tamaa za mwili, na pia kutetea uovu na ukatili. Punde mambo haya yameingia moyoni mwa mwanadamu, ni nini basi mwanadamu anakuwa? Mwanadamu anakuwa ibilisi Shetani! Hii ni kwa sababu ya mwelekeo kisaikolojia upi katika moyo wa mwanadamu? Ni kipi ambacho mwanadamu anatetea? Mwanadamu huanza kupenda uovu na ukatili. Hawapendi uzuri ama wema, wala hata amani. Watu hawako radhi kuishi maisha rahisi ya ubinadamu wa kawaida, lakini badala yake wanataka kufurahia hadhi ya juu na utajiri mkubwa, kufurahia raha za mwili, na kutumia juhudi zote kuridhisha miili yao, bila vizuizi, hakuna vifungo vya kuwashikilia nyuma, kwa maneno mengine kufanya chochote wanachotaka. Hivyo wakati mwanadamu ametumbukizwa katika mienendo ya aina hii, maarifa ambayo mmefunzwa yanaweza kuwasaidia kuwa huru? Je, desturi ya kitamaduni na ushirikina mnayojua yanaweza kuwasaidia kutupilia mbali hii hatari ya kutisha? Je, maadili ya desturi na sherehe za desturi ambazo mwanadamu huelewa zinaweza kumsaidia kujizuia? Chukua Fasihi Bora ya Herufi Tatu, kwa mfano. Inaweza kusaidia watu kutoa miguu yao katika mchanga unaomeza wa mienendo hii? (La, haiwezi.) Kwa njia hii, mwanadamu anakuwa mwovu zaidi na zaidi, mwenye kiburi, mwenye kushusha hadhi, mwenye ubinafsi, na mwenye kijicho. Hakuna tena upendo kati ya watu, hakuna tena upendo wowote kati ya wanafamilia, hakuna tena uelewa wowote kati ya jamaa na marafiki; mahusiano ya binadamu yamejawa ukatili. Kila mtu anataka kutumia mbinu katili kuishi miongoni mwa wanadamu wenzake; wanakamata riziki zao kwa kutumia ukatili; wanashinda vyeo vyao na kupata faida zao wenyewe kwa kutumia ukatili na wanafanya chochote watakacho kwa kutumia njia mbovu na katili. Si ubinadamu huu unatisha? (Ndiyo.) Baada ya kunisikia Nikiongea kuhusu vitu hivi sasa, hamfikiri kwamba inatisha kuishi miongoni mwa aina hii ya umati, katika dunia hii na katika mazingira, yote ambayo Shetani amepotosha? (Ndiyo.) Kwa hivyo mmewahi kujihisi kuwa wenye kusikitisha? Lazima mnaihisi kiasi sasa, siyo? (Ndiyo.) Kwa kusikiza sauti zenu, inaonekana kana kwamba mnafikiria “Shetani hutumia njia nyingi mbalimbali kumpotosha mwanadamu. Anakamata kila fursa na yupo kila mahali tunageukia. Mwanadamu bado anaweza kuokolewa?” Mwanadamu bado anaweza kuokolewa? Wanadamu wanaweza kujiokoa? (La.) Je, Mfalme Mkuu wa Jade anaweza kumwokoa mwanadamu? Je, Confucius anaweza kumwokoa mwanadamu? Je, Guanyin Bodhisattva anaweza kumwokoa mwanadamu? (La.) Kwa hivyo ni nani anayeweza kumwokoa mwanadamu? (Mungu.) Watu wengine, hata hivyo, wataibua katika mioyo yao maswali kama: “Shetani anatudhuru kwa kiasi kikubwa sana, kwa hasira sana basi hatuna matumaini ya kuishi, wala imani katika kuishi. Sote tunaishi miongoni mwa upotovu na kila mtu anampinga Mungu hata hivyo, na sasa mioyo yetu imezama chini kadri iwezavyo. Kwa hivyo wakati Shetani anatupotosha, Mungu yuko wapi? Mungu anafanya nini? Chochote Mungu anatufanyia kamwe hatukihisi!” Watu wengine bila kuepukika wanahisi kuhuzunika na bila kuepukika wanahisi kuvunjika moyo kiasi. Kwenu, hisia hii ni ya kina sana kwa sababu vyote ambavyo Nimekuwa nikisema vimekuwa kuwafanya watu kuja kuelewa polepole, kuhisi zaidi na zaidi kwamba hawana matumaini, kuhisi zaidi na zaidi kwamba wameachwa na Mungu. Lakini usijali. Mada yetu ya kushiriki leo, “uovu wa Shetani,” siyo dhamira yetu ya kweli. Kuongea kuhusu kiini cha utakatifu wa Mungu, hata hivyo, lazima kwanza tuongee kuhusu jinsi Shetani anampotosha mwanadamu na uovu wa Shetani ili kuifanya kuwa wazi zaidi kwa watu mwanadamu sasa yuko katika hali ya aina gani. Lengo moja la kuongea juu ya hili ni kuruhusu watu kujua uovu wa Shetani, ilhali jingine ni kuwaruhusu watu kuelewa kwa kina zaidi utakatifu ni nini.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp