Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hukumu Katika Siku za Mwisho | Dondoo 83
25/07/2020
Hakuna anayefaa zaidi na mwenye vigezo, kuliko Mungu mwenye mwili kwa ajili ya kuhukumu upotovu wa mwili wa mwanadamu. Ikiwa hukumu ingefanywa moja kwa moja na Roho wa Mungu, basi isingekuwa inajumuisha wote. Aidha, kazi kama hiyo itakuwa vigumu kwa mwanadamu kuikubali, maana Roho hawezi kukutana uso kwa uso na mwanadamu, na kwa sababu hii, matokeo hayawezi kuwa ya haraka, sembuse mwanadamu hataweza kuona kwa uwazi kabisa tabia ya Mungu isiyokosewa. Shetani anaweza tu kushindwa kabisa ikiwa Mungu mwenye mwili anahukumu upotovu wa mwanadamu. Kuwa sawa na mwanadamu akiwa na ubinadamu wa kawaida, Mungu mwenye mwili anaweza kumhukumu mwanadamu asiye na haki; hii ni ishara ya utakatifu Wake wa ndani na hali yake ya kutokuwa wa kawaida. Ni Mungu pekee ndiye aliyehitimu, na aliye katika nafasi ya kumhukumu mwanadamu, maana ana ukweli, na mwenye haki, na kwa hivyo Ana uwezo wa kumhukumu mwanadamu. Wale ambao hawana ukweli na haki hawafai kuwahukumu wengine. Ikiwa kazi hii ingefanywa na Roho wa Mungu, basi usingekuwa ushindi dhidi ya Shetani. Roho kiasili huwa ameinuliwa sana kuliko viumbe wenye mwili wa kufa, na Roho wa Mungu ni mtakatifu kwa asili, na anaushinda mwili. Ikiwa Roho alifanya kazi hii moja kwa moja, asingeweza kuhukumu kutotii kote kwa mwanadamu, na asingeweza kufichua hali nzima ya mwanadamu ya kutokuwa na haki. Kwa maana kazi ya hukumu pia inafanywa kwa mitazamo ya mwanadamu juu ya Mungu, na mwanadamu hajawahi kuwa na dhana yoyote juu ya Roho, na hivyo Roho hana uwezo wa kufunua hali ya mwanadamu ya kutokuwa na haki, wala kuweza kuweka wazi kabisa hali hiyo ya kutokuwa na haki. Mungu mwenye mwili ni adui wa wale wote wasiomjua. Kupitia kuhukumu dhana za mwanadamu na kumpinga Yeye, Anafunua hali yote ya kutotii ya mwanadamu. Matokeo ya kazi Yake katika mwili yapo dhahiri zaidi kuliko yale ya kazi ya Roho. Na hivyo, hukumu ya wanadamu wote haifanywi moja kwa moja na Roho, bali ni kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu mwenye mwili anaweza kuonekana na kuguswa na mwanadamu, na Mungu mwenye mwili anaweza kumshinda kabisa mwanadamu. Katika uhusiano wake na Mungu mwenye mwili, mwanadamu huwa anapiga hatua kutoka katika upinzani na kuwa mtii, kutoka katika mateso na kukubaliwa, kutoka katika mitazamo na kuwa na maarifa, na kutoka kukataliwa hadi upendo. Haya ni matokeo ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mwanadamu anaokolewa tu kwa kukubali hukumu Yake, bali hatua kwa hatua tu atamwelewa taratibu kupitia neno la mdomo Wake, ametwaliwa Naye wakati wa upinzani wake Kwake, na anapata uzima kutoka Kwake wakati wa kukubali kuadibu Kwake. Hii yote ni kazi ya Mungu mwenye mwili, na sio kazi ya Mungu katika utambulisho Wake kama Roho. Kazi iliyofanywa na Mungu mwenye mwili ni kazi kubwa sana, na ni kazi ya kina sana, na sehemu muhimu ya hatua tatu za kazi ya Mungu ni hatua mbili za kazi ya kufanyika mwili. Upotovu wa kina wa mwanadamu ni kikwazo kikubwa sana katika kazi ya Mungu mwenye mwili. Kwa umahususi, kazi inayofanywa kwa watu wa siku za mwisho ni ngumu sana, na mazingira ni ya uhasama, na tabia ya kila aina ya mwanadamu ni duni sana. Lakini mwishoni mwa kazi hii, bado itapokea matokeo mazuri, bila dosari yoyote; haya ni matokeo ya kazi ya mwili, na matokeo haya yanashawishi sana kuliko kazi ile ya Roho. Hatua tatu za kazi ya Mungu zitahitimishwa na Mungu mwenye mwili, na lazima ikamilishwe na Mungu mwenye mwili. Kazi muhimu sana imefanywa na Mungu mwenye mwili, na wokovu wa mwanadamu ni lazima ufanywe na Mungu mwenye mwili. Ingawa watu wote wanahisi kwamba Mungu mwenye mwili hahusiani na mwanadamu, kwa kweli ni kuwa mwili huu unahusiana na majaliwa na uwepo wa wanadamu wote.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video