Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Mawazo ya Kidini | Dondoo 298

05/07/2020

Hili laweza kuwakumbusha watu maneno ya Mungu kutoka katika kitabu cha Mwanzo: “Na tumuumbe mwanadamu katika sura yetu, kwa mfanano wetu” (Mwanzo 1:26). Ikichukuliwa kuwa Mungu anasema “na tumtengeneze” mtu kwa mfano “wetu,” basi “tu-” inaashiria wawili au wengi; na kwa kuwa anataja “tu-” basi hakuna tu Mungu mmoja. Kwa njia hii, mwanadamu alianza kufikiria udhahania wa nafsi bayana, na kutokana na maneno haya kulitokea dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Basi, Baba anafananaje? Je, Mwana anafananaje? Na Roho Mtakatifu anafananaje? Yawezekana kuwa mwanadamu wa leo aliumbwa kwa mfano wa mtu mmoja aliyeunganishwa pamoja kutoka kwa nafsi tatu? Je, sura ya mwanadamu inafanana na ile ya Baba, Mwana, au Roho Mtakatifu? Mwanadamu ni mfano wa nani katika nafsi za Mungu? Mawazo ya mwanadamu ni ya kimakosa na upuuzi! Yanaweza tu Kumgawanya Mungu kuwa Mungu kadhaa. Wakati Musa aliandika kitabu cha Mwanzo, ni baada ya wanadamu kuumbwa baada ya uumbaji wa dunia. Mwanzo kabisa, dunia ilipoanza, Musa hakuwepo. Ni hadi baadaye kabisa ndipo Musa aliandika Biblia, basi angejuaje alichokinena Mungu kutoka mbinguni? Hakuwa na ufahamu wowote jinsi Mungu alivyoumba ulimwengu. Katika Agano la Kale la Biblia, hapakutajwa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, ni Mungu mmoja tu wa kweli, Yehova, akiifanya kazi yake nchini Israeli. Anaitwa majina tofauti kadri enzi zinavyobadilika, ila hili haliwezi kuthibitisha kuwa kila jina linarejelea mtu tofauti. Ingekuwa hivi, basi je, si kungekuwa na nafsi nyingi sana katika Mungu? Kilichoandikwa katika Agano la Kale ni kazi ya Yehova, hatua ya kazi ya Mungu Mwenyewe tangu mwanzo wa Enzi ya Sheria. Ilikuwa ni kazi ya Mungu, ambapo Alinena, ilikuwa, na Alipoamuru, ilitendeka. Hakuna hata wakati mmoja ambapo Yehova alisema kuwa alikuwa Baba aliyekuja kufanya kazi, wala Hakutabiri kuja kwa Mwana kuwakomboa wanadamu. Wakati wa Yesu ulipowadia, ilisemekana tu kwamba Mungu alikuwa Ameupata mwili kuwakomboa wanadamu, si kwamba ni Mwana aliyekuwa amekuja. Kwa sababu enzi hazifanani na kazi ambayo Mungu Mwenyewe hufanya vilevile inatofautiana, Anapaswa kufanya kazi Yake katika milki tofauti, kwa njia hii utambulisho Alionao vilevile unatofautiana. Mwanadamu anaamini kwamba Yehova ndiye Baba ya Yesu, ila hili halijakiriwa na Yesu ambaye alisema: “Hatukubainishwa kamwe kama Baba na Mwana; Mimi na Baba aliye Mbinguni ni kitu kimoja. Baba yu ndani Yangu Nami ni ndani Yake; wanadamu wanapomwona Mwana, wanamwona Baba.” Baada ya yote kusemwa, iwe Baba au Mwana, Wao ni Roho mmoja, Hawajagawanywa kuwa nafsi tofautitofauti. Mara tu wanadamu wanapojaribu kueleza, mambo hutatizwa na wazo la nafsi tofauti, na vilevile na uhusiano kati ya Baba, Mwana na Roho. Mwanadamu akizungumzia nafsi tofauti, je, hili halimfanyi Mungu kuwa kitu? Mwanadamu hata zaidi huziorodhesha nafsi hizi kama nafsi ya kwanza, ya pili, na ya tatu; haya yote ni mawazo ya mwanadamu yasiyofaa kurejelewa, hayana uhalisi kabisa! Ukimwuliza: “Kuna Mungu wangapi?” atasema kuwa Mungu ni Utatu Mtakatifu wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu: Yule mmoja wa kweli. Ukiuliza tena: “Baba ni nani?” atasema: “Baba ni Roho wa Mungu aliye mbinguni; anatawala kila kitu, na kiongozi wa mbinguni.” “Je, Yehova ni Roho?” Atasema: “Ndiyo!” Ukimuuliza tena, “Mwana ni nani?” atasema kuwa Yesu ndiye Mwana, bila shaka. “Basi kisa cha Yesu ni kipi? Alitoka wapi?” Atasema: “Yesu alizaliwa na Maria kupitia kwa utungaji mimba wa Roho Mtakatifu.” “Je, kiini Chake si Roho vilevile? Je, kazi Yake si kiwakilishi cha Roho Mtakatifu? Yehova ni Roho, vivyo hivyo na kiini cha Yesu. Sasa katika siku za mwisho, bila shaka ni Roho Anayeendelea kufanya Kazi; Wangewezaje kuwa nafsi tofauti? Je, si Roho wa Mungu anafanya kazi ya Roho kutoka katika mitazamo tofauti?” Kwa hivyo, hakuna tofauti bayana kati ya nafsi. Yesu alipatikana kwa utungaji mimba wa Roho Mtakatifu, na bila shaka, Kazi Yake hasa ilikuwa ile ya Roho Mtakatifu. Katika hatua ya kwanza ya kazi iliyofanywa na Yehova, Hakuwa mwili au kuonekana kwa mwanadamu. Kwa hivyo mwanadamu hakuona uso Wake. Haijalishi Alikuwa mashuhuri au mrefu kiasi gani, bado Alikuwa Roho, Mungu Mwenyewe aliyemuumba mwanadamu mwanzoni. Yaani, alikuwa Roho wa Mungu. Aliponena na wanadamu kutoka mawinguni, alikuwa Roho tu. Hakuna hata mmoja aliyeuona Uso wake; ni katika Enzi ya Neema tu ambapo Roho wa Mungu alikuwa mwili na Alipata mwili kule Uyahudi ndipo mwanadamu aliona sura ya kupata mwili kama Myahudi. Hisia ya Yehova haingeweza kuhisika. Hata hivyo, Alipatikana kwa utungaji mimba wa Roho Mtakatifu, yaani, Alipatikana kwa utungaji mimba wa Roho wa Yehova Mwenyewe, na Yesu bado alizaliwa kama mfano halisi wa Roho wa Mungu. Alichokiona mwanadamu mwanzoni kilikuwa ni Roho Mtakatifu Akimshukia Yesu kama njiwa; Hakuwa Roho mwenye upekee kwa Yesu tu, badala yake alikuwa Roho Mtakatifu. Basi roho wa Yesu anaweza kutenganishwa na Roho Mtakatifu? Ikiwa Yesu ni Yesu, Mwana, na Roho Mtakatifu ni Roho Mtakatifu, basi wangewezaje kuwa kitu kimoja? Ingekuwa hivyo kazi isingefanywa. Roho ndani ya Yesu, Roho aliye mbinguni, na Roho wa Yehova wote ni mmoja. Anaweza kuitwa Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu, Roho aliyezidishwa mara saba, na Roho mwenye vyote. Roho wa Mungu mwenyewe anaweza kufanya kazi nyingi. Ana uwezo wa kuumba na kuiangamiza dunia kwa kuleta mafuriko duniani; Anaweza kuwakomboa wanadamu, aidha, kuwashinda na kuwaangamiza wanadamu wote. Kazi hii yote inafanywa na Mungu Mwenyewe na haiwezi kufanywa na yeyote katika nafsi za Mungu kwa niaba Yake. Roho Wake anaweza kuitwa Yehova na Yesu, na vilevile mwenye Uweza. Yeye ni Bwana na Kristo. Anaweza pia kuwa Mwana wa Adamu. Yuko mbinguni na vilevile duniani; Yuko juu ya dunia na pia miongoni mwa umati. Yeye tu ndiye Bwana wa Mbingu na dunia! Tangu wakati wa uumbaji hadi sasa, kazi hii imekuwa ikifanywa na Roho wa Mungu Mwenyewe. Iwe ni kazi mbinguni au katika mwili, yote hufanywa na Roho Wake Mwenyewe. Viumbe wote, wawe mbinguni au duniani, wamo katika kiganja cha mkono Wake wenye nguvu; yote hii ni kazi ya Mungu na haiwezi kufanywa na yeyote kwa niaba Yake. Mbinguni Yeye ni Roho na vilevile Mungu Mwenyewe; miongoni mwa wanadamu, Yeye ni mwili ila anaendelea kuwa Mungu Mwenyewe. Japo Anaweza kuitwa mamia ya maelfu ya majina, Yeye bado ni Mungu Mwenyewe, na kazi yote ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho Wake. Ukombozi wa wanadamu wote kupitia kwa kusulubiwa Kwake ilikuwa kazi ya moja kwa moja ya Roho Wake, na vilevile tangazo kwa mataifa yote na nchi zote wakati wa siku za mwisho. Wakati wote Mungu anaweza kuitwa mwenye uweza na Mungu mmoja wa kweli, Mungu Mwenyewe mwenye vyote. Nafsi bayana hazipo, aidha dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu haipo! Kuna Mungu mmoja mbinguni na duniani!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp