Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 360

21/10/2020

Mtu yeyote anaweza kutumia maneno na vitendo vyake wenyewe kuwakilisha tabia yake halisi. Sura hii ya kweli bila shaka ni asili yake. Kama wewe ni mtu anayeongea bila kuwa dhahiri, basi una asili mbovu. Kama asili yako ni yenye hila sana, basi namna ambayo unafanya mambo ni janja na laghai sana, nawe unafanya iwe rahisi sana kwa watu kulaghaiwa nawe. Kama asili yako ni mbovu sana, huenda maneno yako ni mazuri kusikiliza, lakini vitendo vyako haviwezi kuficha njia zako mbovu. Kama asili yako ni vivu sana, basi kila kitu unachosema vyote vinalenga kukwepa lawama na wajibu wa uzembe na uvivu wako, na vitendo vyako vitakuwa vya polepole sana na vizembe, na vizuri sana katika kuuficha ukweli. Kama asili yako ni yenye uwezo wa kuhisi maono ya wengine sana, basi maneno yako yatakuwa yenye busara na hatua zako pia zitalingana sana na ukweli. Kama asili yako ni aminifu sana, basi maneno yako lazima yawe ya dhati na namna ambayo unafanya mambo lazima iwe yenye kuhusika na mambo halisi, bila mengi ya kufanya bwana wako asikuamini. Kama asili yako ni yenye tamaa sana au ni yenye tamaa ya fedha, basi moyo wako mara nyingi utajazwa na mambo haya na utafanya baadhi ya mambo yaliyopotoka bila kukusudia, mambo maovu ambayo hufanya iwe vigumu kwa watu kusahau na zaidi ya hayo yatawaudhi. Kama Nilivyosema, kama una asili ya usaliti basi ni kujinasua kutoka kwake kwa nadra sana. Msiamini kuwa hivyo ndivyo ilivyo kwamba hamna asili ya usaliti kwa sababu hamjamkosea mtu yeyote. Kama hivyo ndivyo unavyofikiri basi unachukiza sana. Maneno ambayo Nimenena kila wakati yamewalenga watu wote, sio tu mtu mmoja au aina ya mtu. Kwa sababu tu hujanisaliti Mimi kwa jambo moja haithibitishi kwamba huwezi kunisaliti katika jambo lolote jingine. Baadhi ya watu hupoteza imani yao katika kuutafuta ukweli wakati wa kipingamizi katika ndoa zao. Baadhi ya watu huwacha wajibu wao wa kuwa waaminifu Kwangu wakati wa kuvunjika kwa familia. Baadhi ya watu huniacha kwa ajili ya kutafuta wakati wa furaha na msisimko. Baadhi ya watu afadhali waanguke katika korongo lenye giza kuliko kuishi katika mwanga na kupata furaha ya kazi ya Roho Mtakatifu. Baadhi ya watu hupuuza ushauri wa marafiki kwa ajili ya kuridhisha tamaa zao kwa ajili ya mali, na hata sasa hawawezi kuyakubali makosa yao na kugeuka. Baadhi ya watu huishi tu kwa muda chini ya jina Langu ili wapate ulinzi Wangu, wakati wengine hujitolea tu kidogo kwa sababu wameyashikilia maisha na wanahofu kifo. Si vitendo hivi na vingine viovu na zaidi ya hayo visivyofaa tabia tu ambazo watu wamenisaliti kwa muda mrefu ndani ya mioyo yao? Bila shaka, Najua usaliti wa watu haukuwa umepangwa mapema, lakini ni ufunuo wa kimaumbile wa asili zao. Hakuna mtu anayetaka kunisaliti, na zaidi ya hayo hakuna mtu aliye na furaha kwa sababu amefanya kitu kunisaliti. Kinyume chake, wanatetemeka kwa hofu, sivyo? Hivyo mnafikiri kuhusu jinsi mnavyoweza kuzikomboa saliti hizi, na jinsi mnavyoweza kubadili hali ya sasa?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp