Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Maana ya Kuwa Mtu Halisi | Dondoo 348

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Maana ya Kuwa Mtu Halisi | Dondoo 348

115 |13/08/2020

Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ulikuwa hata umeshaamuliwa kabla zaidi Nilipoiumba dunia. Watu hawajui kwamba Nitashinda kabisa katika siku za mwisho, na pia hawajui kwamba ushahidi Wangu kumshinda Shetani ni kuwashinda walio waasi miongoni mwa binadamu. Lakini Nilikuwa Nimeshamwambia adui Yangu lilipokuwa linapambana na Mimi kwamba Nitakuwa mshindi wa wale waliokuwa wamechukuliwa na Shetani na kwa muda mrefu walikuwa watoto wa Shetani, na watumishi wake waaminifu wanaoangalia nyumba yake. Maana halisi ya shinda ni kushinda, kufedhehesha. Katika namna Waisraeli walivyoeleza, ni kushinda kabisa, kuharibu, na kumfanya mwanadamu kutoweza kunipinga zaidi. Lakini leo kama linavyotumika kati yenu binadamu, maana yake ni kushinda. Unapaswa kujua dhamira Yangu ni kuzima kabisa na kuangamiza yule mwovu kati ya binadamu, ili asiweze tena kuasi dhidi Yangu, wala kuwa na pumzi ya kupinga au kuleta fujo kwa Kazi Yangu. Hivyo, kulingana na wanadamu, ina maana ya kushinda. Haijalishi kidokezo cha neno hili, kazi Yangu ni kumshinda mwanadamu. Kwa kweli mwanadamu ni kijalizo cha usimamizi Wangu, lakini kwa usahihi zaidi, mwanadamu si kitu kingine ila ni adui Yangu. Mwanadamu ni mwovu Anayenipinga na kuniasi. Mwanadamu si mwingine ila kizazi cha yule mwovu aliyelaaniwa na Mimi. Mwanadamu si mwingine ila ukoo wa malaika mkuu ambaye alinisaliti Mimi. Mwanadamu si mwingine ila mrithi wa shetani ambaye, akiwa amekataliwa kwa dharau na Mimi kitambo, amekuwa adui Wangu asiyeweza kupatanishwa tangu wakati huo. Anga iliyo juu ya binadamu wote ni yenye giza na kuhuzunisha, bila ya hata ya dalili ya uwazi. Ulimwengu wa mwanadamu uko katika giza totoro, na wanapoishi ndani yake hakuna anayeweza kuona mkono wake mwenyewe wakati anapounyosha mbele yake na hawezi kuona jua anapoinua kichwa chake. Barabara chini ya miguu yake ni matope na imejaa mashimo makubwa, na ni mipindopindo na ya minyongo; nchi yote imejaa maiti. Na pembe za giza zimejaa mabaki ya wafu. Pembe zenye baridi na giza zimejaa magenge ya mapepo yaliyoshika makazi. Katika ubinadamu wote, magenge ya mapepo pia yanakuja na kwenda. Kizazi cha wanyama wengi sana waliojawa na uchafu wanapigana mkono kwa mkono, katika mapambano ya kikatili, na sauti inayosikika ni ya kuleta hofu moyoni. Wakati kama huo, katika dunia kama hiyo, na “paradiso ya kidunia” ya aina hii, ni wapi ambako mwanadamu huenda kutafuta bahati ya maisha? Ni wapi ambako mtu ataenda kujua hatima ya maisha yake? Mwanadamu, akiwa amekanyagwa chini ya miguu ya Shetani kwa muda mrefu, amekuwa akitenda kwa mfano wa Shetani—hata kuwa na mwili wake. Wao ni ushahidi wa kuwa shahidi wa Shetani, wa uwazi. Aina hii ya Mwanadamu, uchafu kama huu, au watoto wa familia hii ya binadamu potovu, ni jinsi gani wangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu? Utukufu Wangu unatoka wapi? Shahidi Wangu yuko wapi? Adui ambaye anasimama dhidi Yangu na kuwapotosha wanadamu tayari amewachafua wanadamu, viumbe Wangu, waliojawa na utukufu Wangu na wanaoishi kulingana na Mimi. Ameiba utukufu Wangu, na kujaza binadamu na sumu iliyojawa na ubaya wa Shetani, na maji ya matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Hapo mwanzo, Nilimuumba mwanadamu, yaani, Nilimuumba babu wa binadamu, Adamu. Alikuwa wa kugusika na mwenye umbo, na aliyejawa na uhai, aliyejawa na nguvu ya maisha, na zaidi sana, akiwa pamoja na utukufu Wangu. Hiyo ilikuwa ni siku tukufu Nilipomuumba mwanadamu. Baada ya hapo, Hawa alitengenezwa kutoka katika mwili wa Adamu, pia babu wa binadamu, na hivyo watu wa uumbaji Wangu walikuwa wamejazwa na pumzi Yangu na kujazwa na utukufu Wangu. Adamu kiasilia aliumbwa kwa mkono Wangu na alikuwa akiwasilisha umbile Langu. Hivyo maana ya asili ya “Adamu” ilipaswa kuwa kiumbe Changu kilichojaa uhai Wangu, kilichojaa utukufu Wangu, kinachoonekana katika hali nzuri, kikiwa na roho na pumzi. Alikuwa kiumbe wa pekee aliyejaliwa na roho ambayo ingeweza kuniwakilisha Mimi, kuwa na picha Yangu na kupokea pumzi Yangu. Hapo mwanzo Hawa alikuwa mtu wa pili kujazwa na pumzi Niliyekusudia kuumba, hivyo maana asili ya “Hawa” ilikuwa kiumbe cha kuendeleza utukufu Wangu, kilichojazwa na nguvu Zangu na zaidi ya hayo kilichojawa na utukufu Wangu. Hawa aliumbwa kutoka kwa Adamu, kwa hivyo alikuwa pia mfano Wangu, kwa maana yeye alikuwa mtu wa pili kuumbwa kwa mfano Wangu. Maana halisi ya “Hawa” ilikuwa kuwa kiumbe hai, aliyepewa roho, aliye katika mwili na mifupa, kuwa ushuhuda Wangu wa pili na pia picha Yangu ya pili katika mwanadamu. Walikuwa mababu wa wanadamu, hazina yake safi na ya thamani, na awali viumbe hai wanao roho. Hata hivyo mwovu alikikanyaga na kupora kizazi cha mababu wa wanadamu, na kuufunga ulimwengu wa binadamu katika giza totoro, hivi kwamba kizazi hiki hakikuamini tena katika uwepo Wangu. Kilicho cha chukizo zaidi ni kwamba mwovu anapowapotosha na kuwakanyaga watu Wangu, pia kwa ukatili akachukua utukufu Wangu, ushuhuda Wangu, nguvu Yangu Niliyowapa watu, pumzi na maisha Niliyowapulizia ndani yao, utukufu Wangu wote katika dunia ya binadamu, na juhudi zote za kuchosha Nilizowekeza katika mwanadamu. Mwanadamu hayupo tena katika mwanga, na amepoteza kila kitu Nilichompa, akiutupilia mbali utukufu Nilioweka juu yake. Wangewezaje milele kukiri kwamba Mimi ndiye Bwana wa uumbaji? Wangewezaje kuamini kuwepo Kwangu mbinguni? Wangewezaje kugundua udhihirisho wa utukufu Wangu duniani? Hawa wajukuu na vitukuu wangeweza kumchukua vipi Mungu wa mababu zao Anayeheshimiwa kama Bwana wa uumbaji? Hawa wajukuu wenye kuhurumiwa “wamewasilisha” kwa ukarimu utukufu kwa yule mwovu, mfano, na vile vile ushahidi ambao Nilikuwa nimewapa Adamu na Hawa, na maisha Niliyompa binadamu nayo ambayo wanategemea, bila kujali hata kidogo uwepo wa yule mwovu, na kumtuza utukufu Wangu wote. Je, si hiki ni chanzo cha jina la “uchafu”? Jinsi gani mwanadamu wa aina hii, mapepo mabaya, maiti inayotembea, takwimu za Shetani, maadui Wangu kama hao wana utukufu Wangu? Nami Nitauchukua tena utukufu Wangu, ushuhuda Wangu miongoni mwa wanadamu na vyote vilivyokuwa mali Yangu, Niliyokuwa Nimewapa wanadamu hapo zamani—na kumshinda mwanadamu kikamilifu. Hata hivyo unapaswa kujua, wanadamu Nilioumba walikuwa watu watakatifu na wenye mfano Wangu na utukufu Wangu. Hapo awali hawakuwa wa Shetani, wala hawakukabiliwa na kukanyagwa kwake, bali walikuwa tu udhihirisho Wangu, walikuwa huru kutokana na sumu yake. Hivyo, Naliwajulisha wanadamu wote kwamba Ninataka tu kilichoumbwa na mkono Wangu, Wapendwa Wangu walio watakatifu ambao kamwe hawajawahi kumilikiwa na mwingine yoyote. Aidha, Mimi nitakuwa na furaha nao, na kuwaona kama utukufu Wangu. Hata hivyo, Ninachotaka sio mwanadamu aliyepotoshwa na Shetani, ambaye ni wa Shetani leo, ambaye si kiumbe Changu tena. Kwa sababu Ninataka kuchukua tena utukufu Wangu katika dunia ya wanadamu, Nitashinda kikamilifu manusura waliobaki kwa wanadamu, kama ushahidi wa utukufu Wangu katika ushindi Wangu dhidi ya Shetani. Mimi huchukua tu ushahidi Wangu kama udhihirisho wa nafsi Yangu, kama kitu cha starehe Yangu. Hii ndiyo nia Yangu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi