Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Maneno kwa Vijana na kwa Wazee | Dondoo 344

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Maneno kwa Vijana na kwa Wazee | Dondoo 344

67 |05/10/2020

Ingawa kazi Yangu ni yenye msaada mkubwa kwenu sana, maneno Yangu daima hushindwa kuwashawishi na kutofanikiwa ndani yenu. Ni vigumu kupata chombo cha kukamilishwa na Mimi na leo karibu Nimepoteza tumaini kwenu. Nimetafuta kati yenu kwa miaka kadhaa lakini ni vigumu kupata msiri. Ninahisi kama Sina imani ya kuendelea kufanya kazi ndani yenu, na Sina upendo kuendelea kuwapenda. Hili ni kwa sababu Nilikuwa Nimechukizwa kitambo na yale mafanikio yenu madogo ya kusikitisha; ni kana kwamba Sikuwahi kuzungumza kati yenu na Sikuwahi kufanya kazi ndani yenu. Mafanikio yenu yanachafua moyo sana—daima mmetiwa fedheha na karibu hamna thamani yoyote. Kwa nadra Ninapata mfano wa mwanadamu ndani yenu au kusikia harufu ya mwanadamu. Iko wapi harufu yenu mpya? Iko wapi gharama ambayo mmelipa kwa miaka mingi, na matokeo yako wapi? Hamjawahi kuyapata? Kazi Yangu sasa ina asili mpya, mwanzo mpya. Ninaenda kutekeleza mipango mikubwa na Ninataka kutekeleza kazi kubwa, ilhali bado mnavingirika katika matope kama hapo awali, kuishi katika maji machafu ya zamani, na kwa utendaji hamjatupa mashaka yenu ya awali. Kwa hivyo, bado hamjapata chochote kutoka kwa maneno Yangu. Bado hamjatupa pahali penu pa awali pa matope na maji machafu, na mnayajua maneno Yangu tu, lakini kwa kweli hamjaingia katika eneo la uhuru wa maneno Yangu, hivyo maneno Yangu hayajawahi kufunguliwa kwenu, na yako kama kitabu cha unabii ambacho kimefungwa kwa maelfu ya miaka. Ninaonekana kwenu katika maisha yenu lakini daima hamjui, na hamnitambui hata. Takriban nusu ya maneno Ninayoyasema ni hukumu ya nyinyi, na hayo hufanikisha tu nusu ya athari ambayo yanapaswa kufanikisha, ambayo ni kutia hofu kuu ndano yenu. Nusu iliyobaki ni maneno ya kuwafundisha kuhusu maisha na jinsi ya kutenda, lakini ni kana kwamba hayapo kwenu, na kana kwamba nyinyi mnasikiliza maneno ya watoto wanaocheza, ambayo daima nyinyi huyatolea tabasamu iliyofichwa, na kisha hakuna kitu kinachofanywa. Hamjawahi kujishughulisha na mambo haya; daima mmefuata matendo Yangu kutokana na udadisi wenu ili kwamba sasa mmeanguka gizani na hamwezi kuuona mwanga—mnalia kwa huruma gizani. Kile Ninachotaka ni utiifu wenu, utiifu wenu usio na masharti na hata zaidi, Nahitaji kwamba muwe na hakika kabisa juu ya kila kitu Ninachosema. Hampaswi kukubali mtazamo wa kutokujali na hasa hampaswi kuuvumilia kwa kuchagua, ni wazi kwamba nyinyi daima hamjali maneno Yangu na kazi Yangu. Kazi Yangu inafanywa katikati yenu na Nimewapa maneno Yangu mengi, lakini mkinilaghai kwa njia hii, Ninaweza tu kutoa bure kile ambacho hamjapata na hamjatia katika vitendo kwa familia za Mataifa. Ni nini kati ya uumbaji hakipo mikononi Mwangu? Wengi wa wale kati yenu ni wa “wa miaka mingi sana” na hamna nguvu ya kukubali aina hii ya kazi Yangu. Nyinyi ni kama ndege wa Hanhao, mnaishi kwa shida, na hamjawahi kuyachukulia maneno Yangu kwa uzito. Vijana ni bure sana na wanajifurahisha sana na hata zaidi wanaipuuza kazi Yangu. Hawahisi kufurahia vyakula vitamu vya karamu Yangu; Wao ni kama ndege mdogo ambaye ameruka nje ya tundu lake kwenda mbali kabisa. Je, wazee na vijana wa aina hii wanawezaje kuwa na manufaa Kwangu?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi