Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Wale Wasiojifunza na Ambao Hawajui Chochote: Je, Wao Sio Wanyama? | Dondoo 331

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Wale Wasiojifunza na Ambao Hawajui Chochote: Je, Wao Sio Wanyama? | Dondoo 331

0 |28/09/2020

Mmeyapuuza mafundisho Yangu yaliyorudiwa tangu zamani. Hata mnayachukulia kuwa vitu vya kuchezea wakati hamna shughuli, na daima mnayafikiria kuwa “hirizi yenu wenyewe ya kujilinda.” Mnaposhutumiwa na Shetani, mnaomba; wakati ninyi ni hasi, mnalala; wakati mna furaha, mnakwenda huku na huko; Ninapowashutumu, mnanyenyekea mno; na mnapotengana nami, mnacheka kwa shauku. Ukiwa katika umati, hakuna mwingine mwenye hadhi kubwa kukuliko, lakini kamwe hujioni kuwa fidhuli zaidi kuwaliko wote. Daima wewe ni mwenye kiburi, aliyeridhika na mwenye maringo kukithiri. Je, “waungwana na wasichana wadogo” na “mabwana na mabibi” kama hawa wasiojua chochote na wasiojifunza kamwe wanawezaje kuyachukulia maneno Yangu kuwa hazina ya thamani? Sasa Nitaendelea kukuhoji: Umejifunza nini hasa kutoka kwa maneno na kazi Yangu katika muda mrefu kama huu? Je, hujakuwa mjanja zaidi katika udanganyifu wako? Mstaarabu zaidi katika mwili wako? Wa kawaida zaidi katika mtazamo wako Kwangu? Nakwambia waziwazi: Nimefanya kazi nyingi sana, lakini imeongeza ujasiri wako, ujasiri ambao awali ulikuwa kama ule wa panya. Hofu yako Kwangu inapunguka kila siku, kwani Mimi ni mkarimu sana, na kamwe sijauadhibu mwili wako kwa kutumia ukatili; huenda unadhani kwamba Nasema maneno makali tu—lakini kwa kawaida huwa Nakutolea tabasamu, na ni nadra ambapo Nakukaripia ana kwa ana. Aidha, Mimi husamehe udhaifu wako kila wakati, na ni kwa sababu ya hili tu ndiyo unanitendea jinsi nyoka humtendea mkulima mzuri. Napendezwa na ujuzi na ustadi wa uwezo wa mwanadamu kuchunguza sana! Kusema ukweli, leo haijalishi iwapo moyo wako una uchaji au la. Mimi sina wasiwasi wala wahaka. Lakini pia ni lazima Nikuambie hili: Wewe “mtu mwenye kipaji,” mpumbavu na usiyetaka kujifunza, hatimaye utaangamizwa na ujanja wako wenye kiburi na usio na umuhimu—ni wewe utakayeteseka na kuadibiwa. Siwezi kuwa mjinga sana kiasi cha kukuandama unapoendelea kuteseka kuzimuni, kwani Mimi silingani na wewe. Usisahau kwamba wewe ni kiumbe aliyelaaniwa na Mimi, na bado aliyefunzwa na kuokolewa na Mimi. Huna chochote Ninachoweza kutotaka kutengana nacho. Kila Nifanyapo kazi, Sizuiliwi na watu, matukio ama vitu vyovyote. Mitazamo na maoni Yangu kuwahusu wanadamu daima yamebaki yale yale. Sikupendi sana, kwani wewe ni nyongeza kwa usimamizi Wangu na huko bora kuliko kitu chochote kingine. Nakushauri hivi: Kila wakati, kumbuka kwamba wewe ni kiumbe wa Mungu tu! Unaweza kuishi nami, lakini unapaswa kujua utambulisho wako; usijione kuwa wa hadhi ya juu sana. Hata Nisipokushutumu, ama kukushughulikia, na Nakutazama kwa tabasamu, hili halithibitishi kwamba wewe unalingana na Mimi; unapaswa kujua kwamba wewe ni mmoja wa wale wanaofuatilia ukweli, sio ukweli wenyewe! Hupaswi kamwe kukoma kubadili kwa kuambatana na maneno Yangu. Huwezi kuepuka hili. Nakushauri ujaribu kujifunza jambo wakati huu muhimu, fursa hii adimu ikujapo. Usinipumbaze; Sikutaki utumie ubembelezaji kujaribu kunidanganya. Unaponitafuta, yote siyo kwa ajili Yangu, bali kwa ajili yako mwenyewe!

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi