Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Waovu Hakika Wataadhibiwa | Dondoo 329

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Waovu Hakika Wataadhibiwa | Dondoo 329

0 |20/08/2020

Hapo awali, Mungu Alipokuwa mbinguni, mwanadamu alijaribu kumdanganya Mungu kwa matendo yake; leo, Mungu Amekuja miongoni mwa mwanadamu —hakuna anayejua ni kwa muda upi—ilhali mwanadamu bado anapitia mizunguko kwa ajili ya Mungu, na kujaribu kumdanganya Mungu. Je, mwanadamu yuko nyuma kwa fikira zake? Ndivyo ilivyokuwa na Yuda: Kabla Yesu aje, Yuda angewadanganya ndugu zake, na hata Yesu alipokuja, bado hakubadilika; hakuwa na maarifa yoyote ya Yesu, na mwishowe alimsaliti Yesu. Je, ilikuwa kwa sababu hakumfahamu Mungu? Kama leo bado hamumfahamu Mungu, basi utakuwa Yuda, na msiba wa tanzia ya usulubishaji wa Yesu katika Enzi ya Neema, maelfu ya miaka iliyopita, utarudiwa tena. Je, hamuyaamini hayo? Ni ukweli mtupu! Siku hizi watu wanatoka katika hali hiyo—Naweza kuwa Ninayasema haya mapema—na watu wa aina hii wanachukua nafasi ya Yuda. Sizungumzi bila kujali, bali ni kulingana na ukweli—na unapaswa kuamini. Ingawa watu wengi wanajifanya kuwa wanyenyekevu, katika mioyo yao hakuna kingine ila kidimbwi cha maji yanayonuka. Sasa, wengi katika kanisa wako vile. Mnafikiri Sijui lolote; leo, Roho Wangu ananiongoza na kunitolea ushuhuda. Unafikiri kwamba Sijui lolote? Je, mnafikiri Sielewi fikira zenu za ujanja katika nyoyo zenu na vitu vilivyowekwa katika nyoyo zenu? Je, Mungu hudanganywa kwa njia rahisi vile? Je unafikiri kwamba unaweza kumtendea vile unavyotaka? Hapo zamani Nilikuwa na wasiwasi kwamba mlikuwa mmefungwa, na hivyo Nikaendelea kuwapa uhuru, lakini hakuna aliyetambua kuwa Nilikuwa mzuri kwao. Niliwapa inchi moja na wakachukua maili. Ulizana wenyewe kwa wenyewe: Sijajishughulika na yeyote, na Sijakuwa na haraka ya kumkaripia yeyote—ilhali Sina tashwishi juu ya motisha na dhana za mwanadamu. Je, unafikiri Mungu Mwenyewe ambaye Mungu Anamtolea ushuhuda ni mjinga? Iwapo ni hivyo basi Nitasema wewe ni kipofu sana. Sitakulaumu, na basi wacha tuone utakavyopotoka. Hebu tuone iwapo ujanja wako utakuokoa, ama iwapo kujaribu uwezavyo kumpenda Mungu kutakuokoa. Leo, Sitakushutumu; hebu tungoje mpaka wakati wa Mungu tuone Atakavyokuadhibu. Sina wakati wa kupoteza kufanya maongezi yasiyo muhimu, na sina nia ya kuchelewesha kazi Yangu kuu kwa ajili yako, buu kama wewe hufai kuchukua muda wa Mungu Akikushugulikia—kwa hivyo wacha tuone kiwango utakachojiendekeza. Watu kama hao hawafuati ufahamu wa Mungu hata kidogo, na hawana upendo wowote kwa Mungu, ilhali wanataka kuitwa wenye haki na Mungu—je huu si utani? Kwa sababu kuna idadi ndogo ya watu walio waaminifu, Mimi sijishughulishi na kingine ila kumpa mwanadamu uhai. Nitakamilisha tu kile kilichohitajika kukamilika leo, na baadaye, adhabu italetwa kwa kila mmoja kulingana na tabia yake. Nimesema kile Ninachopaswa kusema, kwa sababu hii ndio kazi Ninayoifanya. Ninafanya kile Ninachopaswa kufanya, ila Sifanyi Nisichopaswa kufanya, ilhali Natumai kwamba utatumia muda mwingi kwa kutafakari: Kiwango gani hasa cha ufahamu wako wa Mungu ni wa kweli? Je wewe ni mmoja wa wale ambao wamemsulubisha Yesu msalabani tena? Mwisho, Ninasema hivi: Ole wao wamsulubishao Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi