Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani | Dondoo 320

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani | Dondoo 320

120 |05/07/2020

Nawathamini sana wale wasioweka shaka kuhusu wengine na kuwapenda sana wale wanaokubali ukweli kwa urahisi; kwa aina hizi mbili za wanadamu Ninaonyesha utunzaji mkubwa, kwani machoni Mwangu wao ni waaminifu. Kama una ujanja mwingi, basi utakuwa na moyo uliolindwa na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote. Kwa sababu hii, imani yako Kwangu inajengwa kwa msingi wa shaka. Imani kama hii ni moja ambayo kamwe Sitaitambua. Bila imani ya kweli, basi upendo wenu uko mbali na upendo wa kweli. Na mkiwa hata na shaka na Mungu na kuwa na kisio juu Yake kwa kutaka, basi nyinyi bila shaka ni wanadamu wajanja zaidi. Mnakisia iwapo Mungu anaweza kuwa kama mwanadamu: mwenye dhambi isiyosameheka, mwenye tabia ndogo ndogo, asiye na haki na mantiki, aliyekosa hisia ya wema, anayechukua hatua za ubaya, udanganyifu na ujanja, na pia anayefurahishwa na uovu na giza, na kadhalika. Si sababu ambayo mwanadamu ana mawazo kama haya sababu mwanadamu hana hata ufahamu mdogo wa Mungu? Imani kama hii ni sawa na dhambi! Zaidi ya hayo, kuna hata wale wanaoamini kwamba Sifurahishwi na yeyote isipokuwa wale wanaojirairai na kujipendekeza, na kwamba wale wasiojua chochote kuhusu mambo kama haya watakuwa wasio maarufu na hawataweza kuhifadhi nafasi yao kwa nyumba ya Mungu. Je, haya ndiyo maarifa ambayo mmepata kwa miaka hii yote mingi? Ni haya ndiyo mliyoyapata? Na ufahamu wenu kunihusu ni mbali tu na kutoelewa kama huu; mengi zaidi, kuna kufuru kwenu dhidi ya Roho wa Mungu na kuitukana Mbingu. Hii ndiyo maana Ninasema kwamba imani kama yenu itawasababisha tu kupotea mbali na Mimi na kukuwa na upingamizi mkubwa dhidi Yangu. Kwa miaka mingi ya kazi, mmeona ukweli mwingi, lakini mnajua kile masikio Yangu yamesikia? Ni wangapi kati yenu walio tayari kukubali ukweli? Nyote mnaamini kwamba mko tayari kulipa gharama ya ukweli, lakini ni wangapi walioteseka kweli kwa ajili ya ukweli? Yote yaliyo ndani ya mioyo yenu ni uovu, na hivyo mnaamini kwamba yeyote, bila kujali ni nani, ni mjanja na mhalifu. Hata mnaamini kwamba Mungu mwenye mwili angekuwa binadamu wa kawaida: bila moyo wa ukarimu na upendo wema. Zaidi ya hayo, mnaamini kwamba tabia ya adabu na yenye huruma, asili ya ukarimu iko kwa Mungu wa mbinguni pekee. Na mnaamini kwamba mtakatifu kama huyu hayuko, na kwamba giza na uovu tu ndio unaotawala duniani, ilhali Mungu tu ni lengo tukufu ambalo mwanadamu anaweka matumaini, na umbo la hadithi aliyetungwa na mwanadamu. Ndani ya akili zenu, Mungu aliye mbinguni ni mnyoofu sana, mwenye haki, na mkubwa, anayestahili ibada na upendezewaji, lakini Mungu aliye duniani ni mbadala tu na chombo cha Mungu aliye mbinguni. Mnaamini Mungu huyu hawezi kuwa sawa na Mungu wa mbinguni, na hata zaidi hawezi kutajwa kwa pumzi moja na Yeye. Ikujapo kwa ukubwa na heshima ya Mungu, ni mali ya utukufu wa Mungu aliye mbinguni, lakini ikujapo kwa tabia na upotovu wa mwanadamu, vinahusishwa na Mungu aliye duniani. Mungu aliye mbinguni daima ni mkuu, ilhali Mungu wa duniani daima ni asiye na maana, mdhaifu na asiyejimudu. Mungu aliye mbinguni hatolewi kwa hisia, kwa haki tu, ilhali Mungu aliye duniani ana nia ya kibinafsi na hana haki na mantiki yoyote. Mungu aliye mbinguni hana udanganyifu hata kidogo na daima ni mwaminifu, ilhali Mungu wa duniani daima ana upande wa danganyifu. Mungu aliye mbinguni anampenda sana mwanadamu, ilhali Mungu wa duaniani anamjali mwanadamu isivyotosha, hata kumpuuza kabisa. Ufahamu huu usio sahihi umewekwa kwa muda mrefu kwa mioyo yenu na unaweza pia kuendelezwa mbele katika siku za usoni. Mnachukulia matendo yote ya Kristo kwa upande wa wasio wema na kuhukumu kazi Yake yote na utambulisho Wake na kiini Chake kwa mtazamo wa waovu. Mmefanya kosa kubwa sana na kufanya kile ambacho hakijawahi kufanywa na wale kabla yenu. Hiyo ni, mnamtumikia tu Mungu mkuu aliye mbinguni na taji juu ya kichwa Chake na hammshughulikii kamwe Mungu mnayemchukulia kuwa asiye na maana kabisa na hivyo kuwa ghaibu. Hii siyo dhambi yenu? Huu sio mfano halisi wa kosa lenu dhidi ya tabia ya Mungu? Mnamwabudu sana Mungu aliye mbinguni. Mnapenda sana takwimu wakuu na kuheshimu walio na ufasaha mkubwa. Mnaamrishwa kwa furaha na Mungu Anayewapa kiasi kidogo cha utajiri, na mnakonda tu kwa sababu ya Mungu Anayeweza kutimiza tamaa zenu zote. Yule tu msiyemwabudu ni Mungu huyu asiye mkuu; Chombo chenu tu cha chuki ni ushirikiano na huyu Mungu ambaye hakuna mwanadamu anayeweza kumchukulia kuwa mkuu. Kitu pekee ambacho hamko tayari kufanya ni kumtumikia huyu Mungu ambaye hajawahi kuwapa senti moja, na Yule tu msiyemtamani ni huyu Mungu asiyependeza. Mungu kama huyu hawezi kuwawezesha kupanua upeo wenu wa macho, kuhisi kana kwamba mmepata hazina, ama hata kutimiza mnachotaka. Mbona, basi, mnamfuata? Mmefikiria kuhusu swali hili? Mnachofanya hakimkosei tu huyu Kristo, lakini muhimu zaidi, kinamkosea Mungu aliye mbinguni. Nadhani kwamba haya siyo madhumuni ya imani yenu kwa Mungu!

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi