Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 555

26/09/2020

Kukamilishwa na Mungu hakuwezi kuwa kukamilishwa kupitia kwa kula na kunywa neno la Mungu tu. Aina hii ya uzoefu inaegemea upande mmoja sana na haijumuishi pande zote; inamzuia binadamu katika uwezo mdogo sana. Kwa hiyo, binadamu hukosa chakula cha kiroho kinachohitajiwa zaidi. Kama mtapenda kukamilishwa na Mungu, lazima mjifunze kupitia mambo yote na kupatiwa nuru katika yote mnayoyapitia. Kila unapokumbwa na kitu, kiwe kizuri au kibaya, unafaa kufaidi kutoka katika kitu hicho na hakifai kukufanya ukae tu. Haijalishi ni nini, unafaa kuweza kukitilia maanani kwa kusimama upande wa Mungu, na wala si kuchambua au kukisoma kutoka kwa mtazamo wa binadamu (huku ni kupotoka katika hali unayopitia). Kama hivi ndivyo utakavyopitia mambo katika maisha yako, basi moyo wako utazidiwa na mizigo ya maisha yako; utaishi siku zote katika mwanga wa uso wa Mungu na hutaweza kupotoka kwa urahisi katika matendo yako. Binadamu wa aina hii ana matarajio makubwa. Kunazo fursa nyingi za kukamilishwa na Mungu. Yote haya yanategemea kama ni nyinyi ndinyi mnaompenda Mungu kwa kweli na kama mnalo azimio la kukamilishwa na Mungu, kupatwa na Mungu, na kupokea baraka na urithi Wake. Haitakubalika kwenu kuwa na azimio tu. Lazima muwe na maarifa mengi, vinginevyo siku zote mtapotoka katika matendo yenu. Mungu yuko radhi kumkamilisha kila mmoja wenu. Kama ilivyo sasa, ingawa wengi tayari wamekubali kazi ya Mungu kwa muda mwingi, wamejiwekea mipaka ya kufurahia tu neema ya Mungu na wako radhi tu kupokea tulizo fulani la mwili kutoka Kwake. Hawako radhi kupokea ufunuo zaidi na wa kiwango cha juu zaidi, hali ambayo inaonyesha kwamba moyo wa binadamu ungali nje siku zote. Ingawa kazi ya binadamu, huduma yake, na moyo wake wa upendo kwa Mungu vyote vina kasoro chache zaidi, kuhusiana na kiini cha binadamu na kufikiria kwake kusiko na nuru, binadamu bado daima hutafuta amani na furaha ya mwili, na huwa hajali masharti na makusudio ya Mungu katika kumkamilisha binadamu ni yapi. Kwa hivyo maisha ya wengi yangali machafu na yaliyooza, bila dalili zozote za mabadiliko. Yeye hasa haichukilii imani katika Mungu kama suala lenye umuhimu. Badala yake, ni kana kwamba anayo imani tu kwa ajili ya binadamu mwengine, akitenda bila ukweli au kujitolea, na akiishi tu kwa vile viwango vya chini zaidi vya maisha, akiendelea kuwepo tu bila kusudi lolote. Wachache ndio wanaotafuta kuingia ndani ya neno la Mungu katika mambo yote, huku wakifaidi mambo mengi ya kusitawisha, wakiwa wenye utajiri mkubwa zaidi katika nyumba ya Mungu siku hii, na wakipokea baraka zaidi za Mungu. Kama unatafuta kukamilishwa na Mungu katika mambo yote na unaweza kurithi ahadi za Mungu hapa ulimwenguni; kama unatafuta kupatiwa nuru na Mungu katika mambo yote na huiruhusu miaka kuyoyoma tu huku ukiwa umezubaa, hii ndiyo njia inayostahili kuingia kwa bidii. Ni kupitia kwa njia hii tu ndipo unastahili na unafaa kukamilishwa na Mungu. Wewe ndiwe kweli unayetafuta kukamilishwa na Mungu? Wewe ndiwe kweli uliye mwenye bidii katika mambo yote? Unayo roho sawa ya upendo kwa Mungu kama Petro? Unayo hiari ya kumpenda Mungu kama Yesu alivyofanya? Umekuwa na imani katika Yesu kwa miaka mingi; umeona namna Yesu alivyompenda Mungu? Yesu ndiye kweli unayemwamini? Unamwamini Mungu wa matendo wa siku hii; umeona namna ambavyo Mungu wa matendo katika mwili anavyompenda Mungu kule mbinguni? Unayo imani katika Bwana Yesu Kristo; hiyo ni kwa sababu kusulubishwa kwa Yesu ili kuwakomboa wanadamu na miujiza Aliyoifanya vyote kwa ujumla ni ukweli unaokubaliwa. Hata hivyo, imani ya mwanadamu haitokani na maarifa na ufahamu wa kweli wa Yesu Kristo. Unaamini tu katika jina la Yesu lakini huna imani katika Roho Wake, kwani hujali kuhusu namna Yesu alivyompenda Mungu. Imani yako katika Mungu ni changa sana. Ingawa umekuwa na imani katika Yesu kwa miaka mingi, hujui namna ya kumpenda Mungu. Je, jambo hili halikufanyi kuwa mjinga mkubwa zaidi kote ulimwenguni? Hii inaonyesha kwamba kwa miaka mingi umekila chakula cha Bwana Yesu Kristo bure. Simpendi tu binadamu wa aina hii, Naamini kwamba pia Bwana Yesu Kristo, ambaye unamwabudu, hampendi. Mtu wa aina hii anawezaje kukamilishwa? Huaibiki? Huhisi aibu? Bado unao ujasiri wa kumkabili Bwana Yesu Kristo? Je, nyinyi nyote mnaelewa maana ya maneno Yangu?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

God Only Perfects Those Who Truly Love Him

1

If you wish to be perfected by God, learn to experience everything now, whether it’s good or bad. Learn to be enlightened in all you face. From it you must benefit. If you wish to be perfected by God, don’t ever let it make you be passive. Stand on the side of God, that’s how you should consider it. Don’t you study it from the perspective of man. If you wish to be perfected by God, try this manner of experience now, and your heart will be burdened for life, you’ll always live in the light of His presence, won’t easily deviate in your practice. And great prospects will open up for you. There are so many opportunities to be perfected by God, if you truly love Him. There are so many possibilities to be perfected by God, if you are determined to be gained and perfected by Him, to receive His blessing and His inheritance.

2

If you wish to be perfected by God, it’s no use to only have resolution; that is never enough. To avoid mistakes in your practice, knowledge is what you need. Most people have limited themselves to merely basking in God’s grace now. What they do want to receive is only some fleshly comforts from Him, not higher revelations. This shows their heart is still on the outside. They don’t care if they can be made perfect. Their lives are decadent and vulgar. They just get by with the bare minimum, adrift in a purposeless existence, without achieving the slightest change. There are so many opportunities to be perfected by God, if you truly love Him. There are so many possibilities to be perfected by God, if you are determined to be gained and perfected by Him, to receive His blessing and His inheritance.

3

So few seek to enter God’s word in what they face to gain more enriching things, to become ones of greater wealth in His house and receive more of His blessings. There are so many opportunities to be perfected by God, if you truly love Him. There are so many possibilities to be perfected by God, if you are determined to be gained and perfected by Him, to receive His blessing and His inheritance. There are so many opportunities to be perfected by God.

from Follow the Lamb and Sing New Songs

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp