Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 437

26/09/2020

Maisha ya kanisa ni aina ya maisha tu ambapo watu hukutana kufurahia maneno ya Mungu, na huchukua tu kipande kidogo cha maisha ya mtu. Iwapo maisha halisi ya watu yangekuwa kama maisha yao ya kanisani—ikiwemo maisha ya kawaida ya kiroho, kufurahia maneno ya Mungu kwa kawaida, kuomba na kuwa karibu na Mungu kwa kawaida, kuishi maisha halisi ambapo kila kitu kinatekelezwa kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu, kuishi maisha halisi ambapo kila kitu kinatekelezwa kwa mujibu wa ukweli, kuishi maisha halisi ya kutekeleza maombi na kuwa kimya mbele ya Mungu, ya kufanya mazoezi ya kuimba nyimbo za kidini na kucheza, maisha kama haya tu yangemleta mtu katika maisha ya maneno ya Mungu. Watu wengi sana hulenga tu masaa kadhaa ya maisha yao ya kanisa bila “kutunza” maisha yao nje ya masaa hayo, kana kwamba hayahusiki nao. Pia kunao watu wengi ambao huingia tu katika maisha ya watakatifu wanapokula na kunywa maneno ya Mungu, wakiimba nyimbo za kidini au wakiomba, kisha hurejelea nafsi zao za kale nje ya nyakati hizo. Maisha kama hayo hayawezi kubadili watu, na hayatawaruhusu kumjua Mungu. Katika kumwamini Mungu, iwapo mwanadamu anataka mabadiliko kwa tabia yake mwenyewe, basi lazima asijitenge na maisha halisi. Katika maisha halisi, lazima ujijue mwenyewe, ujitelekeze mwenyewe, utende ukweli, na vilevile kujifunza kanuni, maarifa ya kawaida na masharti ya kujiendesha katika mambo yote kabla ya wewe kuweza kutimiza mabadiliko ya polepole. Iwapo utalenga tu ujuzi katika nadharia na kuishi tu katika sherehe za dini bila ya kuingia ndani ya uhalisi, bila kuingia kwenye maisha halisi, basi hutaweza kamwe kuingia katika uhalisi, hutaweza kujijua mwenyewe, kuujua ukweli, au kumjua Mungu, na utakuwa kipofu na mjinga milele. Kazi ya Mungu ya kuwaokoa watu sio kuwaruhusu waishi maisha ya kawaida ya binadamu baada ya kipindi cha muda mfupi, na wala sio ili kubadili mawazo na mafundisho yao yasiyo sahihi. Badala yake, kusudi Lake ni kubadili tabia za zamani za watu, kubadilisha kikamilifu njia yao ya zamani ya maisha, na kubadilisha njia zao zote za mawazo na mtazamo wa akili zilizopitwa na wakati. Kulenga tu maisha ya kanisa pekee hakuwezi kubadili mazoea ya kale ya watu au kubadili njia za kale walizoishi kwa muda mrefu. Lolote litokealo, watu hawapaswi kujitenga na maisha halisi. Mungu anauliza kwamba watu waishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida katika maisha halisi, sio tu katika maisha ya kanisani; kwamba waishi kwa kudhihirisha ukweli katika maisha halisi, sio tu katika maisha ya kanisani; kwamba watimize majukumu yao katika maisha halisi, sio tu katika maisha ya kanisani. Ili kuingia katika uhalisi, mtu lazima apindue vitu vyote kuelekea maisha halisi. Iwapo waumini katika Mungu, watu hawawezi kuja kujijua kupitia kuingia katika maisha halisi, na ikiwa hawawezi kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida katika maisha halisi, watashindwa. Wale wanaomkaidi Mungu wote ni watu ambao hawawezi kuingia katika maisha halisi. Wote ni watu wanaozungumza kuhusu ubinadamu lakini wanaishi kwa kudhihirisha asili ya pepo mbaya. Wote ni watu wanaozungumza kuhusu ukweli lakini wanaishi kwa kudhihirisha kanuni badala yake. Wale wasioweza kuishi kwa kudhihirisha ukweli katika maisha halisi ni wale wanaoamini katika Mungu lakini wanachukiwa na kukataliwa na Yeye. Lazima ufanye mazoezi ya kuingia kwako katika maisha halisi, ujue upungufu wako mwenyewe, ukaidi na upumbavu, na ujue ubinadamu wako usio wa kawaida na udhaifu. Kwa njia hiyo, ufahamu wako wote utaambatanishwa ndani ya hali yako halisi na ugumu. Ni aina hii ya ufahamu pekee ndiyo ya kweli na inaweza kukufanya ushike kwa hakika hali yako mwenyewe na ufanikishe mabadiliko ya tabia yako.

Sasa kwa vile kukamilishwa kwa mwanadamu kumeanza rasmi, mtu lazima aingie katika maisha halisi. Kwa hivyo, ili kutimiza mabadiliko, lazima mtu aanzie kwa kuingia katika maisha halisi, na kubadilika kidogo kidogo. Ukihepa maisha ya kawaida ya binadamu na kuongea tu kuhusu mambo ya kiroho, basi mambo hugeuka makavu na bapa, hugeuka yasiyo ya uhalisi, na mtu angebadilika vipi? Sasa unaambiwa uingie katika maisha halisi kufanya mazoezi, ili uweze kuweka msingi wa kuingia katika uzoefu wa kweli. Hii ni mojawapo ya mambo ambayo mtu anapaswa kufanya. Kazi ya Roho Mtakatifu hasa ni kuongoza, ilhali iliyosalia hutegemea utendaji wa watu na kuingia. Kila mmoja anaweza kufikia kuingia katika maisha halisi kwa njia mbalimbali, kiasi kwamba wanaweza kumleta Mungu katika maisha halisi, na kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida halisi. Haya tu ndiyo maisha yenye maana!

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp