Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 407
02/10/2020
Katika uzoefu wako unaona kuwa moja ya masuala muhimu zaidi ni kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Ni suala ambalo linahusu maisha ya kiroho ya watu, na kuendelea kwa maisha yao. Ni kama tu moyo wako uko na amani mbele za Mungu ndio kutafuta kwako ukweli na mabadiliko katika tabia yako kutazaa matunda. Kwa sababu unakuja ukiwa na mizigo mbele za Mungu na huwa unahisi kila mara kuwa unapungukiwa kiasi kikubwa, kwamba kuna ukweli mwingi ambao unahitaji kujua, uhalisi mwingi unaohitaji kupitia, na kwamba unapaswa kujali kikamilifu kuhusu mapenzi ya Mungu—mambo haya kila mara huwa mawazoni mwako, ni kana kwamba yamekufinyia chini sana kiasi kwamba huwezi kupumua, na hivyo unahisi mzito wa moyo (lakini sio kwa hali hasi). Ni watu wa aina hii pekee ndio wanastahili kukubali kupata nuru ya maneno ya Mungu na kuguswa na Roho wa Mungu. Ni kwa sababu ya mzigo wao, kwa sababu ni wenye moyo mzito, na, inaweza kusemwa, kwa sababu ya gharama ambayo wamelipa na mateso ambayo wamepitia mbele ya Mungu ndio wanapata nuru na mwangaza wa Mungu, kwa kuwa Mungu hamtendei yeyote kwa upendeleo. Yeye huwa mwenye haki kila mara katika kuwatendea watu, lakini Yeye sio holela katika kuwakimu watu, na hawapi bila masharti. Huu ni upande mmoja wa tabia Yake yenye haki. Katika maisha halisi, watu wengi bado hawajaufikia ulimwengu wa aina hii. Kwa kiwango cha chini zaidi, mioyo yao bado haijamgeukia Mungu kikamilifu, na hivyo bado hakujakuwa na mabadiliko yoyote makubwa katika tabia ya maisha yao. Hii ni kwa sababu wanaishi tu kati ya neema ya Mungu, na bado hawajapata kazi ya Roho Mtakatifu. Vigezo vya Mungu kuwatumia watu ni kama ifuatavyo: Mioyo yao inamgeukia Mungu, wanasumbuliwa na maneno ya Mungu, wanakuwa na mioyo ya kutamani, na wako na azimio la kutafuta ukweli. Ni watu wa aina hii tu ndio wanaoweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu na mara kwa mara wapate nuru na mwangaza. Watu ambao Mungu huwatumia huonekana kwa nje kama watu wasio na akili na kama wasio na uhusiano wa kawaida na wengine, ingawa wao huzungumza na adabu, hawazungumzi kiholela, na wanaweza daima kuwa na moyo uliotulia mbele ya Mungu. Lakini ni mtu wa aina hiyo tu ndiye anatosha kutumiwa na Roho Mtakatifu. Mtu huyu asiye na akili anayezungumziwa na Mungu huonekana kama asiye na uhusiano wa kawaida na wengine, na hana upendo wa kuelekea nje au matendo ya juu juu, lakini anapokuwa akieleza mambo ya kiroho anaweza kufungua roho yake na kwa kujinyima awatolee wengine mwangaza na nuru ambayo amepata kutoka kwa uzoefu wake wa hakika mbele za Mungu. Hivi ndivyo anavyodhihirisha upendo wake kwa Mungu na kuridhisha mapenzi ya Mungu. Wengine wote wanapokuwa wanamkashifu na kumdhihaki, ana uwezo wa kutoelekezwa na watu wa nje, matukio, au vitu, na bado anaweza kutulia mbele za Mungu. Mtu wa aina hii inavyooneka yuko na utambuzi wake mwenyewe wa pekee. Bila kujali wengine, moyo wake kamwe haumwachi Mungu. Wengine wanapokuwa wakizungumza kwa furaha na kwa vichekesho, moyo wake bado unasalia mbele za Mungu, kutafakari neno la Mungu au kusali kwa kimya kwa Mungu aliye moyoni mwake, akitafuta makusudi ya Mungu. Kamwe hawatilii maanani udumishaji wa uhusiano wa kawaida na wengine. Mtu wa aina hii inavyoonekana hana falsafa ya maisha. Kwa nje, mtu huyu ni mchangamfu, anayependwa, asiye na hatia, lakini pia anamiliki hisia ya utulivu. Huu ni mfano wa mtu ambaye Mungu anamtumia. Mambo kama falsafa ya kuishi au “mantiki ya kawaida” hayawezi kufanya kazi kwa mtu wa aina hii; mtu wa aina hii ameutoa moyo wake wote kwa neno la Mungu, ambaye anaonekana kuwa na Mungu tu katika moyo wake. Hii ni aina ya mtu ambaye Mungu anamrejelea kama mtu “bila mantiki,” naye tu ni mtu ambaye anatumiwa na Mungu. Alama ya mtu ambaye anatumiwa na Mungu ni: Haijalishi ni lini au wapi, moyo wake daima uko mbele za Mungu, na haijalishi jinsi gani wengine ni wenye anasa, jinsi gani wanavyoshiriki katika tamaa, wanajiingiza katika anasa za kimwili—moyo wake kamwe haumwachi Mungu, naye hafuatani na umati. Aina hii ya mtu pekee ndiye anafaa kwa ajili ya matumizi ya Mungu, naye hasa ni yule ambaye amekamilika na Roho Mtakatifu. Ikiwa huwezi kufikia hatua hii, basi hustahili kupatwa na Mungu, ili kukamilishwa na Roho Mtakatifu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video