Swahili Christian Testimony Video | Kuondokana na Minyororo ya Utumwa

12/07/2020

Babake mhusika mkuu alikuwa muumini kwa miaka mingi. Alifanya wajibu wake wa kushiriki injili kwa uaminifu na aliweza kuteseka na kulipa gharama. Hata hivyo, hakufuatilia ukweli, lakini badala yake alifuatilia umaarufu, faida, na hadhi. Alieneza mfarakano kati ya kina ndugu, na hata akapita mipaka na kuwatenga na kuwashambulia wengine, na hivyo kuvuruga sana maisha ya kanisa na kuingia katika uzima kwa kina ndugu. Ushirika na msaada ulitolewa kwake mara nyingi, lakini hakuwahi kutubu. Kupitia maneno ya Mungu, mhusika mkuu anakuja kutambua kuwa baba yake ni mtu mwovu ambaye amechoshwa na ukweli na anachukia ukweli, na kwamba anapaswa kufukuzwa kanisani. Hata hivyo, anazuiwa na hisia zake na hathubutu kumfunua au kumripoti. Anatafuta ukweli kupitia kusoma maneno ya Mungu na anaona asili, hatari, na athari za kutenda kutokana na mhemuko. Anaondokana na utumwa wa hisia zake za kibinafsi na anaweza kujizoeza kupenda kile ambacho Mungu anapenda na kuchukia kile ambacho Mungu anachukia, na anafichua tabia mbovu ya baba yake. Maisha ya kanisa yanabadilika na kuwa mazuri baada ya kufukuzwa kwake, yakiwa bila vurugu ya mtu mwovu.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp