Christian Testimony Video | Baada ya Kubadilishwa na Mtu Mwingine (Swahili Subtitles)

02/11/2020

Mhusika mkuu katika Baada ya Kubadilishwa na Mtu Mwingine anaanza kufanya wajibu wake kwa bidii baada ya kuchaguliwa kama kiongozi wa kanisa na kazi ya kanisa inaanza kupata mafanikio polepole. Kufumba na kufumbua, anaanza kuridhika sana, kujionyesha katika mikutano na ushirika na kujaribu kuwafanya wengine wamstahi. Anawashushia hadhi hata wafanyakazi wenzake na anajiinua. Mwishowe, anaachishwa wajibu wake kwa sababu anafuatilia jina na hadhi kwa uthabiti, amepoteza kazi ya Roho Mtakatifu na hana uwezo wa kufanya kazi yoyote ya vitendo. Baada ya kupoteza cheo chake, anazama katika mateso makubwa na usafishaji. Kwa kuhukumiwa na kuadibiwa na maneno ya Mungu, anaona kiini cha kufuatilia sifa na hadhi waziwazi na anakuja kuelewa njia ya imani yenye mafanikio ni ipi. Je, anajifunza mambo yapi mengine na anabadilikaje vingine baada ya kuachishwa wajibu? Utajua utakapotazama Baada ya Kubadilishwa na Mtu Mwingine.

Tazama zaidi

Ikiwa una matatizo au maswali yoyote katika imani yako, tafadhali wasiliana nasi wakati wowote.

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp