Wimbo wa Dini | Kubali Hukumu ya Kristo wa Siku za Mwisho ili Utakaswe

26/08/2020

Unajua tu kuwa Yesu atashuka siku za mwisho,

lakini atashuka jinsi gani hasa?

Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa,

na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu,

unaweza kuufuata roho wa Mungu?

Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani,

ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu,

na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu,

lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu.

Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa?

Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila

ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi.

Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao,

na kufanywa safi kabisa,

na kupata mabadiliko ya tabia,

hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza

na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu.

Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu.

Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili,

na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati hiyo!

Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu:

umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa.

Ili uipendeze nafsi ya Mungu,

lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa.

Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila

ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi.

Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao,

na kufanywa safi kabisa,

na kupata mabadiliko ya tabia,

hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza

na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu.

Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu.

Ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu.

Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu,

kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kusimamia mwanadamu,

ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha.

Na basi wewe, mwenye dhambi aliyetoka tu kukombolewa,

huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja.

Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila

ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi.

Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao,

na kufanywa safi kabisa,

na kupata mabadiliko ya tabia,

hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza

na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu.

Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp