Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Amri za Enzi Mpya | Dondoo 243

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Amri za Enzi Mpya | Dondoo 243

105 |22/07/2020

Kuwa watu lazima wafuate majukumu mengi wanayostahili kuyatekeleza. Hili ndilo watu wanalopaswa kufuata, na wanalostahili kufanya. Mruhusu Roho Mtakatifu afanye linalostahili kufanywa na Roho Mtakatifu; mwanadamu hawezi kulichangia lolote. Mwanadamu sharti ashike yale ambayo lazima yatendwe na mwanadamu, ambayo hayana uhusiano na Roho Mtakatifu. Si lolote bali lile ambalo lazima litendwe na mwanadamu, na lazima lifuatwe kama amri, kama ufuasi wa sheria za Agano la Kale. Ingawa sasa si Enzi ya Sheria, bado kuna maneno mengi yanayolingana na Enzi ya Sheria ambayo yanahitaji kufuatwa, na hayatendwi tu kwa kutegemea kuguswa na Roho Mtakatifu, lakini ni yale yanayostahili kufuatwa na wanadamu. Kwa mfano: Hupaswi kuihukumu kazi ya Mungu wa vitendo. Hupaswi kumpinga mtu anayeshuhudiwa na Mungu. Mbele za Mungu, utahifadhi nafasi yako, na hutakuwa mwovu. Matamshi yako yanapaswa yawe wastani, na maneno yako na matendo yako yanapaswa kufuata mpangilio wa mwanadamu aliyeshuhudiwa na Mungu. Unapaswa kuheshimu ushuhuda wa Mungu. Usipuuze kazi ya Mungu wala maneno kutoka kinywa chake. Usiige sauti na malengo ya matamshi ya Mungu. Kwa nje, usifanye lolote linalodhihirisha kumpinga mtu anayeshuhudiwa na Mungu. Haya na mengine ndiyo yanayopaswa kufuatwa na kila mmoja. Katika kila enzi, Mungu hutaja amri nyingi zinazoambatana na amri na zinazopaswa kufuatwa na mwanadamu. Kupitia hili, anazuia tabia ya mwanadamu, na kugundua ukweli wake. Tazama maneno “Onyesha heshima kwa baba na mama yako” kutoka kwa nyakati za Agano la Kale, kwa mfano. Maneno haya hayatumiki hivi leo; wakati huo, yalizuia tabia zingine za mwanadamu tu, yalitumika kuonyesha uaminifu wa imani ya mwanadamu kwa Mungu, na yalikuwa alama ya wale waliomwamini Mungu. Ingawa sasa ni Enzi ya Ufalme, bado kuna amri nyingi ambazo mwanadamu lazima azifuate. Amri za kale hazitumiki; leo, kuna mazoea mengi, mwafaka kwa mwanaadamu kutekeleza, na ambayo ni muhimu. Hayahusiani na kazi ya Roho Mtakatifu na lazima yatendwe na mwanadamu.

Katika Enzi ya Neema, mazoea mengi ya Enzi ya Sheria yaliondolewa kwa sababu sheria hizi hazikufaa hasa kazi ya wakati huo. Baada ya kuondolewa, mazoea mengi yaliwekwa ambayo yalifaa enzi hiyo, na ambayo yamekuwa amri nyingi za sasa. Mungu wa leo alipokuja, kanuni hizi zilitupiliwa mbali, na hazikuhitajika kufuatwa tena, na mazoea mengi ambayo yalifaa kazi ya wakati huu yakawekwa. Leo, mazoea haya si kanuni, lakini ili kuwa na athari; ni mazuri kwa ajili ya leo—na kesho, pengine, yatakuwa kanuni. Kwa ujumla, unafaa kufuata yale ambayo yatafanikisha kazi ya leo. Usizingatie kesho: Yanayofanywa leo ni kwa ajili ya leo. Pengine kesho kutakuwa na mazoea mazuri ambayo utahitajika kutekeleza—lakini usizingatie hayo sana, yafuate yanayofaa kufuatwa leo ili uepuke kumpinga Mungu. Leo, hakuna lolote muhimu analopaswa kufuata mwanadamu zaidi ya yafuatayo: Usimdanganye au kumficha Mungu lolote lililoko mbele ya macho yako. Usizungumze uchafu ama matamshi ya kiburi mbele ya Mungu aliye mbele yako. Usimdanganye Mungu mbele ya macho yako kwa maneno mazuri wala kwa maneno ya kuridhisha ili uweze kujipatia uaminifu Wake. Usitende bila heshima mbele za Mungu. Tii yote yatokayo kinywani mwa Mungu, wala usikatae, usipinge, ama kusaili maneno Yake. Usitafsiri unavyoona kuwa sawa, maneno yanayonenwa kutoka kinywani mwa Mungu. Chunga ulimi wako ili usikutie katika mtego wa hila danganyifu za yule mwovu. Unapaswa kulinda nyayo zako ili kuepuka kupita mipaka uliyowekewa na Mungu. Kufanya hivyo kutakufanya uzungumze maneno ya majivuno na yenye fahari kuu kulingana na mtazamo wa Mungu, na hivyo kufanya uchukiwe na Mungu. Usirudierudie maneno kutoka kinywa cha Mungu ovyoovyo, usije ukadhihakiwa na wengine na kufanywa kuwa mjinga na mapepo. Tii kazi yote ya Mungu wa leo. Hata ikiwa hauifahamu, usiihukumu; unachoweza kufanya ni kutafuta na kushiriki. Hakuna mtu atapatendea dhambi mahali pa Mungu pa asili. Huwezi kufanya lolote ila kumhudumia Mungu wa leo kwa mtazamo wa mwanadamu. Huwezi kumfunza Mungu wa leo kwa mtazamo wa mwanadamu—kufanya hivyo ni kupotoka. Hakuna anayeweza kusimama kwa niaba ya mtu aliyeshuhudiwa na Mungu; katika maneno yako, matendo, na mawazo yako ya ndani, unasimama katika nafasi ya mwanadamu. Hili ni la kufuatwa, ni wajibu wa mwanadamu, hakuna anayeweza kulibadilisha, na kufanya hivyo ni ukiukaji wa amri za utawala. Inapaswa kukumbukwa na kila mtu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi