Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kazi na Kuonekana kwa Mungu | Dondoo 47

27/09/2020

Kanisa la Filadelfia limechukua umbo, na hili limesababishwa kabisa na neema na rehema za Mungu. Watakatifu wameleta upendo wao wa Mungu mbele na kamwe hawakuyumbayumba kutoka kwa njia yao ya kiroho. Kuwa imara katika imani kwamba Mungu mmoja wa kweli Amekuwa mwili, ya kwamba Yeye ndiye Mkuu wa ulimwengu Ambaye hutawala vitu vyote—hii imethibitishwa na Roho Mtakatifu na ni ushahidi thabiti! Kamwe hauwezi kubadilika!

Eh, Mwenyezi Mungu! Leo Umefungua macho yetu ya kiroho, kuwaruhusu vipofu kuona, viwete kutembea, wenye ukoma kuponywa. Umefungua dirisha la mbinguni na tumeona siri za dunia ya kiroho. Maneno Yako matakatifu yametujaza sisi, na Umetuokoa kutoka kwa ubinadamu potovu uletwao na Shetani. Hii ni kazi Yako kuu na rehema Yako kubwa sana. Sisi ni mashahidi Wako!

Umekuwa mnyenyekevu na kufichika katika kimya kwa muda mrefu. Wewe umepitia ufufuo na mateso ya msalaba; Wewe umejua furaha na huzuni ya maisha ya binadamu pamoja na mateso na dhiki. Wewe umepitia na kuonja maumivu ya dunia ya binadamu, na Wewe umetelekezwa na enzi. Mungu mwenye mwili ni Mungu Mwenyewe. Wewe umetuokoa kutoka kwa lundo la samadi kwa ajili ya mapenzi ya Mungu na umetushikilia kwa mkono Wako wa kulia; neema Yako imepeanwa huru kwetu sisi. Unafanya juhudi za ukarimu kuingiza maisha Yako ndani yetu; gharama Ulilolipa kwa damu Yako, jasho, na machozi imekuwa katika watakatifu. Sisi ndio matokeo ya juhudi Zako zenye bidii, sisi ndio gharama Unayolipa.

Eh, Mwenyezi Mungu! Ni kwa sababu ya upendo Wako na rehema, haki Yako na uadhama, utakatifu Wako na unyenyekevu kwamba watu wote wanapaswa kutii mbele Yako na kukuabudu Wewe daima dawamu.

Leo Umefanya kamili makanisa yote—kanisa la Filadelfia—ambayo ni matunda ya miaka 6,000 ya mpango Wako wa usimamizi. Sasa watakatifu kwa unyenyekevu wanaweza kuwa watiifu mbele Yako; wao wameunganishwa pamoja katika roho na kuandama pamoja katika upendo. Wao wameunganishwa kwa chanzo cha chemchemi ya maji. Maji ya uhai ya maisha huenda bila mwisho na husafisha na kutakasa uchafu wote na taka katika kanisa, kwa mara nyingine tena yakitakasa hekalu Lako. Tumemjua Mungu wa ukweli wa vitendo, tumetembea ndani ya maneno Yake, tumetambua shughuli zetu na wajibu wetu wenyewe, na kufanya kila kitu tunachoweza kutumia kila rasilmali yetu kwa ajili ya kanisa. Tunapaswa kuchukua kila muda kuwa kimya mbele Yako na kutilia maanani kazi ya Roho Mtakatifu ili mapenzi Yako yasizuiwe ndani yetu. Miongoni mwa watakatifu kuna upendano, na nguvu za wengine zitafidia dosari za wengine. Tembea katika roho kila muda na upate nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu; fahamu ukweli na uuweke katika vitendo mara moja; kuwa sawa na nuru mpya na kufuata nyayo za Mungu.

Shirikiana kwa utendaji na Mungu; kumruhusu Yeye Achukue uongozi ni kutembea pamoja naye. Mawazo yetu yote wenyewe, fikira na maoni, mitego yetu yote ya kimwili, hutokomea kama moshi. Tunamruhusu Mungu Atawale katika roho zetu, kutembea naye na kupata uwezo unaozidi sana wa mwanadamu, kushinda ulimwengu, na roho zetu huruka kwa uhuru na kufikia ufunguliwaji; haya ni matokeo ya Mwenyezi Mungu kuwa Mfalme. Tunawezaje kukosa kucheza ngoma na kuimba sifa, kutoa sifa zetu, na kutoa nyimbo mpya?

Kweli kuna njia nyingi za kumsifu Mungu: kuliita jina Lake, kukaribia karibu na Yeye, kumfikiria Yeye, kuomba kwa kusoma, na kuwa na ushirika, kuzingatia, kutafakari, na sala, na pia kuna nyimbo za sifa. Katika aina hizi za sifa kuna raha, na kuna kupakwa mafuta; kuna nguvu katika sifa na pia kuna mzigo. Kuna imani katika sifa, na kuna utambuzi mpya.

Shirikiana na Mungu kwa utendaji, tumikia kwa uratibu na kuwa moja, yakidhi mapenzi ya Mwenyezi Mungu, harakisha kuwa mwili mtakatifu wa kiroho, kanyaga Shetani, na kumaliza hatima yake. Kanisa la Filadelfia limechukuliwa kwenda mbinguni mbele ya Mungu na linajidhihirisha katika utukufu wa Mungu.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp