Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 185

Vyovyote vile uelewa juu ya Mungu ulivyo mkubwa katika mioyo ya watu, unaamua nafasi kubwa kiasi gani Anachukua katika mioyo yao. Vyovyote vile kiwango cha maarifa ya Mungu kilivyo katika mioyo yao ndivyo kwa kiwango kikubwa Mungu alivyo katika mioyo yao. Ikiwa Mungu unayemfahamu yupo tupu na ni yule asiye yakini, basi yule Mungu unayemwamini pia ni tupu na ni yule asiye yakini. Ikiwa Mungu unayemfahamu anaishia ndani ya mipaka ya mawanda yako, basi Mungu wako ni Mungu mdogo kweli na hajaunganishwa na Mungu wa kweli. Kwa hiyo, kuyajua matendo ya Mungu, kuujua uhalisi wa Mungu na uweza Wake, kuujua utambulisho wa kweli wa Mungu Mwenyewe, kujua kile Anacho na alicho kujua kile Alichokuonyesha miongoni mwa vitu vyote—haya ni muhimu sana kwa kila mtu anayetafuta maarifa ya Mungu. Haya yana uhusiano wa moja kwa moja na iwapo watu wanaweza kuingia kwa uhalisi wa ukweli. Ikiwa unauwekea mipaka uelewa wako juu ya Mungu katika maneno tu, ikiwa unauwekea mipaka uelewa wako mdogo tu, Neema ya Mungu unayoihesabu, au shuhuda zako ndogo kwa Mungu, basi Ninasema kwamba yule Mungu unayemwamini si Mungu wa kweli kabisa. Kabisa si Mungu Mwenyewe wa kweli, na inaweza pia kusemwa kuwa Mungu unayemwamini si Mungu. Hii ni kwa sababu Mungu ambaye Ninamzungumzia ni yule ambaye Anatawala kila kitu, ambaye Anatembea miongoni mwa kila kitu, ambaye Anasimamia kila kitu. Yeye ndiye Anashikilia majaliwa ya binadamu wote—ambaye anashikilia majaliwa ya kila kitu. Kazi na matendo ya Mungu ambaye Ninamzungumzia hayaishii kwa sehemu ndogo tu ya watu. Yaani, haiishii tu kwa watu tu ambao sasa wanamfuata. Matendo Yake yameonyeshwa miongoni mwa vitu vyote, katika vitu vyote kuendelea kuishi, na katika sheria za mabadiliko ya vitu vyote.

Kama huwezi kuona au kutambua matendo yoyote ya Mungu kati ya vitu vyote, basi huwezi kutoa ushuhuda kwa matendo Yake yoyote. Ikiwa huwezi kuwa na ushuhuda wowote kwa Mungu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya huyo anayeitwa Mungu mdogo ambaye unamfahamu, Mungu huyo ambaye anaishia kwenye mipaka ya mawazo yako tu, na yupo ndani ya akili yako finyu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya aina hiyo ya Mungu, basi Mungu hataisifu imani yako. Unapokuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu, ikiwa unatumia tu jinsi unavyofurahia neema ya Mungu, kukubali adhabu na kurudi Kwake, na kufurahia baraka Zake katika ushuhuda wako Kwake, ambao kwa kiasi kikubwa hautoshi na hauwezi kumridhisha. Ikiwa unataka kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu kwa namna ambayo inakubaliana na mapenzi Yake, kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe wa kweli, basi unapaswa kuona kile Mungu anacho na alicho kutokana na matendo Yake. Unapaswa kuona mamlaka ya Mungu kutoka katika udhibiti Wake wa kila kitu, na kuona ukweli wa jinsi Anavyowakimu binadamu wote. Ikiwa unakiri tu kwamba chakula chako cha kila siku na kinywaji na mahitaji yako katika maisha yanatoka kwa Mungu, lakini huoni ukweli kwamba Mungu anawakimu binadamu wote kwa njia ya vitu vyote, kwamba anawaongoza binadamu wote kwa njia ya utawala Wake wa vitu vyote, basi hutaweza kamwe kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu. Sasa unaelewa yote haya, sio? Lengo Langu ni nini kusema yote haya? Iko hivyo ili usiweze kulichukulia hili kirahisi, ili msiamini kwamba mada hizi Nilizozizungumzia hazina uhusiano na kuingia kwenu binafsi katika maisha, na ili msichukue mada hizi kama tu aina ya maarifa au mafundisho. Ikiwa unasikiliza ukiwa na mtazamo kama huo, hutapata kitu hata kimoja. Utapoteza fursa kubwa hii ya kumjua Mungu.

Lengo Langu la kuzungumza juu ya mambo haya yote ni nini? Lengo langu ni kuwafanya watu wamjue Mungu, kuwafanya watu waelewe matendo halisi ya Mungu. Mara utakapomuelewa Mungu na ukaelewa matendo Yake, ni baada ya hapo tu ndipo utakuwa na fursa au uwezekano wa kumjua Mungu. Kwa mfano, ikiwa unataka kumwelewa mtu, ni jinsi gani unaweza kumwelewa? Je, inaweza kuwa kupitia kuangalia umbo lao la nje? Je, inaweza kuwa kupitia kile wanachokivaa, jinsi wanavyovaa? Je, inaweza kuwa ni kupitia kuangalia jinsi wanavyotembea? Je, inaweza kuwa ni kupitia kuangalia mawanda ya maarifa yao? (Hapana.) Kwa hiyo unamwelewaje mtu? Unafanya hukumu kupitia maneno na tabia ya mtu, kupitia mawazo zake, kupitia kile anachokionyesha na kile anachokifichua. Hivyo ndivyo unavyomjua mtu, unavyomwelewa mtu. Kwa njia ile ile, ikiwa mnahitaji kumjua Mungu, ikiwa mnataka kuelewa upande Wake wa vitendo, upande Wake wa kweli, mnapaswa kumjua Yeye kupitia matendo Yake na kupitika kila kitu halisi Anachofanya. Hii ndiyo njia bora zaidi na ndiyo njia pekee.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp