Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Mawazo ya Kidini | Dondoo 297

11/07/2020

Ikiwa hatua tatu za kazi zitakadiriwa kulingana na dhana hii ya Utatu, basi ni lazima kuwe na Mungu watatu kwani kazi iliyofanywa na kila mmoja si sawa. Ikiwa yeyote miongoni mwenu anasema kwamba hakika Utatu upo, basi eleza huyu Mungu mmoja katika nafsi tatu ni nini hasa. Baba Mtakatifu ni nini? Mwana ni nini? Roho Mtakatifu ni nini? Je, Yehova ni Baba Mtakatifu? Je, Yesu ni Mwana? Basi, Roho Mtakatifu je? Je, Baba si Roho? Je, kiini cha Mwana vilevile si Roho? Je, kazi ya Yesu haikuwa ya Roho Mtakatifu? Je, kazi ya Yehova haikufanywa wakati ule na Roho sawa tu na kazi ya Yesu? Mungu Anaweza kuwa na Roho wangapi? Kulingana na maelezo yako hizi nafsi tatu, yaani, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni mmoja; kama ni hivyo, kuna Roho watatu lakini kuwa na Roho watatu kunamaanisha kuwa kuna Mungu Watatu. Hii inamaanisha kuwa hakuna Mungu Mmoja wa kweli; Mungu wa aina hii anawezaje kuwa kiini asili cha Mungu? Kama unakubali kuwa kuna Mungu mmoja tu, basi Anawezaje kuwa na Mwana na awe Baba? Je, hizi si fikra zako mwenyewe? Kuna Mungu Mmoja tu, nafsi moja katika Mungu huyu, na Roho mmoja tu wa Mungu sawa tu na ilivyoandikwa katika Biblia kwamba “Kuna tu Roho Mtakatifu mmoja na Mungu mmoja tu.” Haijalishi kama Baba na Mwana unaowazungumzia wapo, kuna Mungu mmoja tu, na kiini cha Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu mnaowaamini ni kiini cha Roho Mtakatifu. Kwa maneno mengine, Mungu ni Roho, ila Ana uwezo wa kupata Mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu na vilevile kuwa juu ya vitu vyote. Roho Wake anajumuisha kila kitu na Anapatikana kila mahala. Anaweza kuwa katika mwili na wakati ule ule akawa kote duniani. Kwa kuwa watu wanasema kwamba Mungu ndiye tu Mungu wa kweli, basi kuna Mungu mmoja, ambaye hawezi kugawanywa kwa mapenzi ya awaye yote! Mungu ni Roho mmoja tu, na nafsi moja; na huyo ni Roho wa Mungu. Ikiwa ni kama usemavyo, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, basi Hawa si watatu? Roho Mtakatifu ni kitu kimoja, Mwana ni kingine, na Baba vilevile ni kingine. Ni nafsi tatu tofauti zenye viini tofauti, iweje basi ziwe kila moja sehemu ya Mungu mmoja? Roho Mtakatifu ni Roho; hili ni rahisi kueleweka kwa wanadamu. Ikiwa ni hivyo basi, Baba ni Roho zaidi. Hajawahi kushuka kuja duniani na Hajawahi kupata mwili; Yeye ni Yehova Mungu katika mioyo ya mwanadamu, na kwa hakika Yeye vilevile ni Roho. Basi kuna uhusiano gani kati Yake na Roho Mtakatifu? Je, ni uhusiano kati ya Baba na Mwana? Au ni uhusiano kati ya Roho Mtakatifu na Roho wa Mungu? Je, kiini cha kila Roho ni sawa? Au Roho Mtakatifu ni chombo cha Baba? Hili linaweza kuelezwaje? Aidha kuna uhusiano gani kati ya Mwana na Roho Mtakatifu? Je, ni uhusiano kati ya Roho wawili au ni uhusiano kati ya mwanadamu na Roho? Haya yote ni masuala ambayo hayawezi kuelezewa! Ikiwa Wote ni Roho mmoja, basi hapawezi kuwepo na mjadala kuhusu nafsi tatu, kwani zote zinamilikiwa na Roho mmoja. Kama Zingekuwa nafsi tofauti, basi Roho Zao Zingetofautiana katika nguvu zao na kamwe hawangekuwa Roho mmoja. Hii dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni upuuzi mtupu! Hili linamweka Mungu katika vitengo na kumgawanya kuwa nafsi tatu, kila moja ikiwa na hadhi na Roho; basi Atawezaje kuwa Roho mmoja na Mungu mmoja? Hebu niambie, je, mbingu na dunia na vyote vilivyomo viliumbwa na Baba, Mwana, au na Roho Mtakatifu? Wengine husema Waliviumba kwa pamoja. Basi ni nani alimkomboa mwanadamu? Alikuwa Roho Mtakatifu, Mwana, au Baba? Wengine husema ni Mwana aliyewakomboa wanadamu. Basi Mwana ni nani katika kiini? Siye kupata mwili kwa Roho wa Mungu? Mungu aliyepata mwili anamwita Mungu aliye Mbinguni Baba katika mtazamo wa mwanadamu aliyeumbwa. Je, hufahamu kuwa Yesu alizaliwa kutokana na utungaji mimba kupitia Roho Mtakatifu. Ndani yake mna Roho Mtakatifu; lolote usemalo, Yeye bado ni mmoja na Mungu wa Mbinguni, kwani Yeye ni kupata mwili kwa Roho wa Mungu. Hili wazo la Mwana si kweli Kabisa. Ni Roho mmoja anayefanya Kazi yote; Mungu Mwenyewe pekee, yaani, Roho wa Mungu anafanya kazi Yake. Roho wa Mungu ni nani? Je, si Roho Mtakatifu? Je, si Roho Mtakatifu anayefanya kazi ndani ya Yesu? Ingekuwa kazi haikufanywa na Roho Mtakatifu (yaani Roho wa Mungu), je, kazi Yake ingemwakilisha Mungu Mwenyewe? Yesu alipomwita Mungu wa mbinguni kwa jina la Baba alipokuwa akiomba, hili lilifanywa katika mitazamo ya mwanadamu aliyeumbwa, kwa sababu Roho wa Mungu alikuwa amejivisha kama mwanadamu wa kawaida na Alikuwa na umbile la nje la mwanadamu aliyeumbwa. Hata ikiwa ndani yake mlikuwa na Roho wa Mungu, umbo Lake la nje bado lilikuwa lile la mwanadamu wa kawaida; kwa maana nyingine, Alikuwa “Mwana wa Adamu” jambo ambalo watu wote, akiwemo Yesu Mwenyewe, walilizungumzia. Na kwa sababu Anaitwa Mwana wa Adamu, Yeye ni mtu (Mwanamke au mwanamume, kwa vyovyote vile mwenye umbo la nje la mwanadamu) aliyezaliwa katika familia ya kawaida ya watu wa kawaida. Kwa hivyo, Yesu kumwita Mungu wa mbinguni kwa jina la Baba kulikuwa sawa na mlivyomwita mara ya kwanza Baba; Alifanya hivyo kutokana na mtazamo wa Mwanadamu aliyeumbwa. Je, mnakumbuka Sala ya Bwana ambayo Yesu aliwafundisha kukariri? “Baba Yetu Uliye mbinguni…” Aliwaambia wanadamu wote wamwite Mungu wa Mbinguni kwa jina la Baba. Na kwa kuwa Naye pia alimwita Baba, alifanya hivyo kutoka kwa mtazamo wa mtu aliye katika daraja moja nanyi nyote. Kwa kuwa mlimuita Mungu wa mbinguni Baba, hili linaonyesha kuwa Yesu alijichukulia kuwa katika daraja sawa nanyi, kama mwanadamu duniani aliyeteuliwa na Mungu (yaani, Mwana wa Mungu). Kama mnamwita Mungu “Baba,” je, hii si kwa sababu nyinyi ni wanadamu walioumbwa? Haijalishi Yesu alikuwa na mamlaka makubwa kiasi gani duniani, kabla ya kusulubiwa, Alikuwa tu Mwana wa Adamu, akiongozwa na Roho Mtakatifu (yaani, Mungu), Akiwa miongoni mwa viumbe wa duniani, kwani bado Alikuwa hajaikamilisha kazi Yake. Kwa hivyo, kumwita kwake Mungu wa mbinguni Baba kulikuwa tu unyenyekevu na utiifu Wake. Yeye kumwita Mungu (yaani, Roho aliye mbinguni) kwa namna ile, hata hivyo, hakudhibitishi kuwa Yeye ni Mwana wa Roho wa Mungu aliye mbinguni. Badala yake, ni kuwa mtazamo wake ni tofauti, si kwamba ni nafsi tofauti. Uwepo wa nafsi tofauti ni uongo. Kabla ya kusulubiwa kwake, Yesu alikuwa Mwana wa Adamu aliyefungwa katika udhaifu wa kimwili, na Hakuwa na mamlaka kamilifu ya Roho. Hiyo ndiyo maana Angeweza tu kutafuta mapenzi ya Mungu Baba kutoka katika mtazamo wa kiumbe. Ni kama tu Alivyoomba mara tatu huko Gethsemane: “Si kama Nitakavyo, bali kama utakavyo.” Kabla Atundikwe msalabani, Hakuwa zaidi ya Mfalme wa Wayahudi; alikuwa Kristo, Mwana wa Adamu, na wala si mwenye utukufu. Hiyo ndiyo maana, kutokana na mtazamo wa mwanadamu, Alimwita Mungu Baba. Sasa, huwezi kusema kuwa wote wamwitao Mungu Baba ni Wana. Ingekuwa kweli, basi wote si mngekuwa Mwana punde Yesu alipowafundisha Sala ya Bwana? Ikiwa bado hamjaridhika, basi niambieni hili, ni nani mmwitaye Baba? Ikiwa mnamrejelea Yesu, je, Baba ya Yesu ni nani kwenu? Baada ya Yesu kurudi mbinguni, hii dhana ya Baba na Mwana ilikoma. Hii dhana ilifaa tu kipindi ambacho Yesu alikuwa mwili; katika mazingira mengine yoyote, uhusiano ni ule wa kati ya Bwana wa uumbaji na kiumbe mnapomwita Mungu Baba. Hakuna wakati ambapo wazo hili la Utatu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu linaweza kuwa na mashiko; ni uongo ambao ni nadra kuonekana na halipo!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp