Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 166

22/07/2020

Je, unaielewa hoja kuu kuhusu kuifahamu tabia ya haki ya Mungu? Unaweza kuwa na mengi ya kusema kuhusu uzoefu wako kuhusiana na hili, lakini kuna hoja chache ambazo Napaswa kukuambia. Kuielewa tabia ya haki ya Mungu, kwanza mtu anapaswa kuelewa hisia za Mungu: kile Anachokichukia, kile Anachokichukia kabisa, kile Anachokipenda, ni nani ambaye Anamvumilia, ambaye Anamrehemu, na ni aina gani ya mtu anayepokea rehema hiyo. Hii ni hoja ya msingi kufahamu. Aidha, mtu anapaswa kuelewa kwamba haijalishi Mungu ni mwenye upendo kiasi gani, haijalishi ni Mwenye rehema na upendo kiasi gani kwa watu, Mungu hamvumilii mtu yeyote anayekosea hali na nafasi Yake, wala Hamvumilii mtu yeyote anayekosea heshima Yake. Ingawa Mungu anawapenda watu, Hawadekezi. Anawapatia watu upendo Wake, rehema Yake, na uvumilivu Wake, lakini hajawahi kuwakuwadia; Ana kanuni Zake na mipaka Yake. Bila kujali ni kwa kiwango gani umeuhisi upendo wa Mungu ndani yako, bila kujali upendo huo ni wa kina kiasi gani, hupaswi kamwe kumtendea Mungu kama ambavyo ungemtendea mtu mwingine. Ingawa ni kweli kwamba Mungu anawachukulia watu kama wako karibu Naye, ikiwa mtu anamwangalia Mungu kama mtu mwingine, kana kwamba ni kiumbe mwingine wa uumbaji, kama rafiki au kama kitu cha kuabudu, Mungu atawaficha uso Wake na kuwatelekeza. Hii ndiyo tabia Yake, na hamvumilii mtu yeyote anayemchukulia kiholela katika suala hili. Hivyo mara nyingi tabia ya Mungu inasemwa katika neno Lake: Haijalishi umesafiri njia nyingi kiasi gani, umefanya kazi kubwa kiasi gani au umevumilia kiasi gani kwa ajili ya Mungu, mara tu unapoikosea tabia ya Mungu, Atamlipa kila mmoja wenu kulingana na kile ulichokifanya. Je, mmeiona? (Ndiyo, tumeiona.) Hii ina maana kwamba Mungu anaweza kuwaona watu kama wapo karibu na Yeye, lakini watu hawapaswi kumchukulia Mungu kama rafiki au ndugu. Usimchukulie Mungu kama rafiki yako. Haijalishi ni upendo kiasi gani umepokea kutoka Kwake, haijalishi Amekuvumilia kwa kiasi gani, hupaswi kabisa kumchukulia Mungu kama rafiki tu. Hii ndiyo tabia ya haki ya Mungu. Unaelewa, sio? Je, kuna haja ya Mimi kusema zaidi kuhusu hili? Je, una uelewa wowote wa awali kuhusiana na suala hili? Kwa ujumla, hili ndilo kosa rahisi sana ambalo watu wanafanya bila kujali kama wanaelewa mafundisho, au kama hawajafikiria chochote kuyahusu hapo awali. Watu wanapomkosea Mungu, inaweza isiwe kwa tukio moja, au kitu kimoja walichokisema, bali ni kwa sababu ya mtazamo walionao na hali waliyomo. Hili ni jambo la kutisha sana. Baadhi ya watu wanaamini kwamba wana uelewa juu ya Mungu, kwamba wanamjua, hata wanaweza kufanya baadhi ya mambo ambayo yanaweza kumpendeza Mungu. Wanaanza kuhisi wako sawa na Mungu na kwamba kwa werevu wamekuwa na urafiki na Mungu. Aina hizi za hisia sio sahihi kabisa. Ikiwa huna uelewa wa kina juu ya hili, ikiwa huelewi vizuri hili, basi ni rahisi sana kumkosea Mungu na kukosea tabia Yake ya haki. Unalielewa hili sasa, siyo? (Ndiyo.) Je, tabia ya haki ya Mungu sio ya kipekee? Je, ni sawa na utu wa binadamu? Je, ni sawa na tabia binafsi za mwanadamu? Sivyo kabisa, sio? (Ndiyo.) Hivyo, hupaswi kusahau kwamba haijalishi ni kwa namna gani Mungu anawachukulia watu, haijalishi ni namna gani Anafikiri juu ya watu, nafasi, tabia na hadhi ya Mungu kamwe havibadiliki. Kwa binadamu, Mungu siku zote ni Bwana wa wote na Muumbaji.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp