Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu | Dondoo 128

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu | Dondoo 128

81 |06/08/2020

Mungu amekuja duniani kufanya kazi yake miongoni mwa watu, kujifichua mwenyewe kwa mwanadamu na kumruhusu mwanadamu kumtazamia; je, hili ni jambo dogo? Ni kweli ni kuu! Si kama jinsi mwanadamu anafikiria kwamba Mungu amekuja ili mwanadamu aweze kumtazamia, ili mwanadamu aweze kuelewa kwamba Mungu ni wa ukweli na wala si yule asiye yakini ama tupu, na ya kuwa Mungu ni wa fahari lakini pia mnyenyekevu. Je, inawezekana kuwa rahisi hivyo? Ni hasa kwa sababu Shetani amepotosha mwili wa mwanadamu, na mwanadamu ndiye Mungu anakusudia kuokoa, ya kuwa Mungu ni sharti achukue mwili ili afanye vita na Shetani na binafsi kumchunga mwanadamu. Hii pekee ndiyo yenye manufaa kwa kazi yake. Miili miwili hiyo iliyopatwa na Mungu imekuwepo ili imshinde Shetani, na imekuwepo ili imuokoe mwanadamu kwa ubora. Hayo ni kwa sababu mwili unaofanya vita na Shetani inaweza tu kuwa Mungu, iwe ni Roho wa Mungu au ni Mungu aliyepata mwili. Kwa kifupi, mwili unaofanya vita na Shetani hauwezi kuwa ni malaika, na wala kuwa mwanadamu, ambaye amepotoshwa na Shetani. Malaika hawana nguvu ya kuifanya, na mwanadamu ni dhaifu hata zaidi. Kwa hivyo, ikiwa Mungu anataka kufanya kazi katika maisha ya mwanadamu, kama Yeye anataka kuja binafsi duniani kumfinyanga mwanadamu, basi ni lazima Yeye binafsi awe mwili, hivyo ni kusema, lazima binafsi Apate mwili, na utambulisho wa asili na kazi ambayo ni lazima afanye, aje miongoni mwa wanadamu na kumwokoa mwanadamu binafsi. La sivyo, kama ingekuwa ni Roho wa Mungu au mwanadamu ndiye aliyefanya kazi hii, basi vita hivi daima vingeweza kushindwa kutimiza matokeo yake, na kamwe havingelikwisha. Wakati Mungu anakuwa mwili ili binafsi aende kwa vita dhidi ya Shetani miongoni mwa watu ndipo mwanadamu anapata nafasi ya wokovu. Aidha, ndipo tu Shetani anaaibishwa, na kuwachwa bila nafasi zozote za kutumia au mipango yoyote ya kutekeleza. Kazi inayofanywa na Mungu aliyepata mwili haiwezi kutimizwa na Roho wa Mungu, na hata zaidi haiwezi kufanywa na mtu yeyote mwenye mwili kwa niaba ya Mungu, kwa kuwa kazi ambayo Yeye hufanya ni kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, na ili kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Kama mwanadamu angeshiriki katika vita, yeye tu angelikimbia kwa huzuni ya kuvurugwa, na hangekuwa na uwezo wa kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Angekuwa hana uwezo wa kumwokoa mwanadamu msalabani, ama wa kushinda uasi wote wa mwanadamu, lakini tu angeweza kufanya kazi kidogo ya zamani kwa mujibu wa kanuni, au pengine kazi ambayo haihusiani na kushindwa kwa Shetani. Kwa hivyo, mbona ujisumbue? Kuna umuhimu gani ya kazi ambayo haiwezi kumpata mwanadamu, ama hata kumshinda Shetani? Na kwa hivyo, vita dhidi ya Shetani vinaweza kufanywa na Mungu mwenyewe, na haviwezi kufanywa na mwanadamu. Jukumu la mwanadamu ni kutii na kufuata, kwa kuwa mwanadamu hana uwezo wa kufanya kazi ya kuanzisha kipindi kipya, wala, zaidi ya hayo, anaweza kutekeleza kazi ya kupambana na Shetani. Mwanadamu anaweza tu kumtosheleza Muumba chini ya uongozi wa Mungu Mwenyewe, ambapo Shetani hushindiwa; hili ndilo jambo pekee ambalo mwanadamu anaweza kulitenda. Na kwa hivyo, kila wakati vita vipya vinapoanza, kila wakati kazi ya enzi mpya inapoanza, kazi hii inafanywa na Mungu binafsi, ambapo kupitia kazi hiyo Yeye huongoza enzi nzima, na kufungua njia mpya kwa ajili ya wanadamu wote. Pambazuko la kila enzi mpya ni mwanzo mpya katika vita na Shetani, ambapo kupitia hiyo mwanadamu anaingia akiwa mpya zaidi, ulimwengu wa kupendeza zaidi na enzi mpya ambayo inaongozwa na Mungu Mwenyewe. Mwanadamu ni bwana wa vitu vyote, lakini wote ambao wamepatwa watakuwa matunda ya vita dhidi ya Shetani. Shetani ndiye mpotoshaji wa vitu vyote, na ndiye mshindwa katika mwisho wa vita vyote, na pia ndiye atakayeadhibiwa kufuatia vita hivi. Miongoni mwa Mungu, mwanadamu na Shetani, ni Shetani pekee ndiye atachukiwa na kukataliwa. Wale waliopatwa na Shetani lakini hawarejeshwi na Mungu, wakati huo huo, watakuwa wale ambao watapokea adhabu kwa niaba ya Shetani. Kati ya hawa watatu, Mungu pekee ndiye anapaswa kuabudiwa na vitu vyote. Wale waliopotoshwa na Shetani lakini wanarejeshwa na Mungu na wale wanaofuata njia ya Mungu, wakati huo huo, wanakuwa wale ambao watapokea ahadi ya Mungu na kuhukumu wale waovu kwa niaba ya Mungu. Bila shaka Mungu atakuwa mshindi na Shetani bila shaka atashindwa, lakini miongoni mwa wanadamu kuna wale watakaoshinda na wale watakaoshindwa. Wale ambao watashinda ni wale wa Mshindi na wale ambao watashindwa ni wale wa mshindwa; huu ni uainishaji wa kila mmoja kufuatana na aina, na ni matokeo ya mwisho ya kazi yote ya Mungu, na pia ni lengo la kazi yote ya Mungu, na kamwe haitabadilika. Msingi wa kazi kuu wa mpango wa usimamizi wa Mungu unalenga wokovu wa mwanadamu, na Mungu anakuwa mwili kimsingi kwa ajili ya msingi huu, kwa ajili ya kazi hii, na ili kumshinda Shetani. Mara ya kwanza Mungu kuwa mwili ilikuwa ili kumshinda Shetani: Yeye binafsi akawa mwili, na akasulubiwa msalabani binafsi, ili kukamilisha kazi ya vita vya kwanza, ambayo ilikuwa kazi ya ukombozi wa mwanadamu. Aidha, awamu hii ya kazi ilifanywa na Mungu binafsi, ambaye amekuwa mwili ili kufanya kazi yake miongoni mwa wanadamu, ili kusema neno lake binafsi na kumwezesha mwanadamu kumwona. Bila shaka, ni hakika kwamba Yeye hufanya kazi nyingine njiani, lakini sababu kuu ya kufanya kazi yake binafsi ni ili kumshinda Shetani, kushinda wanadamu wote, na kuwapata hawa watu. Na kwa hivyo, kazi ya Mungu kuwa na mwili ni jambo kuu kweli. Kama kusudi lake lilikuwa tu kumwonyesha mwanadamu kuwa Mungu ni mnyenyekevu na aliyefichika, na kuwa Mungu ni wa ukweli, kama ingelikuwa ni kwa ajili ya kufanya kazi hii, basi hakungekuwa na haja ya kuwa mwili. Hata kama Mungu hakuwa mwili, yeye angefichua unyenyekevu na usiri wake, ukuu wake na utakatifu, kwa mwanadamu moja kwa moja, lakini mambo kama hayo hayana uhusiano wowote na usimamizi wa mwanadamu. Mambo kama hayo hayana uwezo wa kumwokoa mwanadamu au kumfanya awe kamili, na hata hayawezi kumshinda Shetani. Kama kushindwa kwa Shetani kungehusisha Roho tu akipigana vita dhidi ya roho, basi kazi kama hii ingekuwa na thamani ndogo ya ukweli; haingeweza kumpata mwanadamu na ingeharibu hatima na matarajio ya mwanadamu. Kwa hivyo, kazi ya Mungu leo ni moja ambayo ina umuhimu kupindukia. Sio hivyo ili kwamba mwanadamu aweze kumwona, au ili macho ya mwanadamu yaweze kufunguliwa, au ili ampe msukumo kiasi na kutiwa moyo; kazi kama hii haina umuhimu. Kama unaweza tu kuongea kwa hekima ya sampuli hii, basi inathibitisha kuwa wewe haujui umuhimu wa ukweli wa Mungu kupata mwili.

Umetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi