Wimbo wa Kikristo | Matamko Rasmi Juu ya Imani Katika Mungu (Music Video)

10/04/2020

Haleluya! Mwenyezi Mungu! Tunakushukuru na kukusifu!

Haleluya! Mwenyezi Mungu! Tunakuabudu Wewe milele!

Kristo ameonekana katika siku za mwisho,

Maneno Yake yanatuhukumu, kututakasa na kutubadilisha.

Yakituongoza kwenye njia sahihi, naishi maisha mapya ya kumpenda Mungu.

Ni ajabu kuuelewa ukweli,

Naacha upotovu wangu na kujisikia huru kabisa.

Dhana zangu zote zimeondoka, na uasi hauko ndani yangu tena.

Hakuna kuzurura tena, hakuna kuteseka tena.

Roho yangu imewekwa huru, na ninaimba nikimsifu Mungu.

Ninaimba nikimsifu Mungu.

Upendo wa Mungu ni wa kweli na wa thamani,

ukituongoza kwenye njia ing’aayo ya uzima.

Nimeonja upendo mtamu sana, Nitampenda Mungu daima.

Ndugu, dada, hebu tuje pamoja, bega kwa bega, pamoja kama kitu kimoja.

Kwa moyo mmoja na nia moja, tunamtumikia na kuimba sifa Zake.

Nani asiyeweza kusema kilicho moyoni mwake?

Nani asiyeweza kueleza upendo wake?

Unacheza na kumtukuza Mungu, Ninapiga makofi kando yenu.

Ninapiga makofi kando yenu.

Nyimbo zetu zimejaa upendo kwa Mungu,

kwa Mwenyezi Mungu tunafanywa upya.

Maisha yetu potovu ya zamani yameisha, ni furaha kuishi mbele za Mungu!

Kutenda ukweli kwa karibu kunatuweka huru;

tunatimiza wajibu wetu na kumletea Mungu utukufu.

Na watu wa Mungu wanafurahia maisha mapya,

tunampenda Mungu na kuishi katika mwanga.

Tumeivunja minyororo ya dunia,

tumeivunja minyororo ya familia,

tumeivunja minyororo ya mwili.

Jinsi gani ilivyo ya kupendeza kupendana!

Jinsi gani ilivyo ya kupendeza kupendana!

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ikiwa una matatizo au maswali yoyote katika imani yako, tafadhali wasiliana nasi wakati wowote.

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp