Wimbo wa Kikristo | Ni Mungu tu Ana Njia ya Uzima
01/08/2020
Njia ya uzima si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kuwa nacho;
si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kuipata kwa urahisi.
Kwani uzima unatoka tu kwa Mungu,
ni Mungu Mwenyewe pekee Aliye na kiini cha uzima,
ni Mungu pekee aliye na njia ya uzima.
Hivyo ni Mungu pekee ndiye chanzo cha uzima,
na kisima cha maji ya uzima kinachotiririka milele,
na kisima cha maji ya uzima kinachotiririka milele.
Tangu uumbaji wa dunia,
Mungu amefanya kazi nyingi ambazo zinahusisha umuhimu wa maisha,
zinazoletea mwanadamu uzima;
Amelipa gharama kubwa ili mwanadamu apate uzima.
Kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele;
Yeye ndiye njia ambayo kwayo mwanadamu hupata ufufuo.
Mungu hajakosa kamwe kuwa katika moyo wa mwanadamu,
Kila wakati Anaishi kati ya mwanadamu.
Yeye ni nguvu inayoendesha kuishi kwao, na msingi wa uwepo wao;
Yeye ni amana tajiri kwa mwanadamu kuishi kwa kumtegemea.
Anafanya mwanadamu kuzaliwa tena,
na kuwafanya waishi kwa nguvu katika majukumu yao tofauti.
Kwa sababu ya mamlaka Yake na nguvu Yake ya maisha isiokosa,
mwanadamu ameishi kizazi baada ya kizazi,
Mamlaka ya maisha ya Mungu yanamsaidia mwanadamu bila kukoma;
Mungu amelipa gharama ambayo hakuna mwanadamu wa kawaida amewahi kulipa.
Mungu amelipa gharama ambayo hakuna mwanadamu wa kawaida amewahi kulipa.
Nguvu ya maisha ya Mungu inatawala juu ya mamlaka yote; na inazidi nguvu zote.
Maisha Yake ni ya milele, mamlaka Yake ni ya ajabu.
Hakuna kiumbe yeyote aliyeumbwa anayeweza kushinda nguvu ya maisha Yake,
ambayo ipo na inaangaza nuru inayong’aa wakati wowote ama mahali,
wakati wowote ama mahali.
Mbingu, dunia inaweza kubadilika sana, maisha ya Mungu hayabadiliki kamwe.
Vitu vyote vimeenda, lakini maisha ya Mungu bado ipo,
kwani Mungu ni chanzo na asili ya uwepo wa vitu vyote,
asili ya uwepo wa vitu vyote.
kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video