Wimbo wa Kikristo | Ni Muumba Pekee Anayemhurumia Binadamu Huyu (Kiitikio cha sauti ya Kike)

02/09/2018

Muumba yuko miongoni mwa binadamu siku zote,

kwamba siku zote Anazungumza na binadamu na uumbaji mzima,

na kwamba Anatekeleza matendo mapya, kila siku.

Hali Yake halisi na tabia vyote vimeelezewa katika mazungumzo Yake na binadamu;

fikira na mawazo Yake vyote vinafichuliwa kabisa kwenye matendo Yake haya;

Anaandamana na kufuatilia mwanadamu siku zote.

Anaongea kimyakimya kwa mwanadamu na uumbaji wote kwa maneno Yake ya kimyakimya:

Mimi niko juu ya ulimwengu, na Mimi nimo miongoni mwa uumbaji Wangu.

Ninawaangalia; Ninawasubiri; Niko kando yao….

Muumba pekee ndiye aliye na huruma kwa wanadamu hawa.

Muumba pekee ndiye anayeonyesha mwanadamu huyu huruma na huba.

Muumba pekee ndiye anayeshikilia huba ya kweli, isiyovunjika kwa mwanadamu huyu.

Vilevile, Muumba pekee ndiye anayeweza kumpa huruma mwanadamu huyu

na kufurahia viumbe vyake vyote.

Moyo wake waruka na kuumia kwa kila matendo ya mwanadamu:

Ameghadhibishwa, dhikishwa, na kuhuzunishwa juu ya maovu na kupotoka kwa binadamu;

Ameshukuru, amefurahia, amekuwa mwenye kusamehe na mwenye kushangilia

kutokana na kutubu na kuamini kwa binadamu;

kila mojawapo ya fikira na mawazo Yake vyote vipo juu ya na vinazungukia mwanadamu;

kile Alicho na anacho vyote vinaonyeshwa kwa uzima au kwa minajili ya mwanadamu;

uzima wa hisia Zake vyote vimeingiliana na uwepo wa mwanadamu.

Kwa minajili ya mwanadamu, Anasafiri na kuzungukazunguka;

kwa utaratibu Anatoa kila sehemu ya maisha Yake;

Anajitolea kila dakika na sekunde ya maisha Yake….

Hajawahi kujua namna ya kuyahurumia maisha Yake,

ilhali siku zote Amehurumia na kufurahia mwanadamu ambaye Yeye Mwenyewe aliumba….

Anatoa kila kitu Alichonacho kwa ubinadamu huu….

Yeye anatoa huruma na uvumilivu Wake bila masharti na bila matarajio ya kufidiwa.

Anafanya hivi tu ili mwanadamu aweze kuendelea kuwepo mbele ya macho Yake,

kupokea toleo Lake la maisha;

Anafanya hivi tu ili mwanadamu siku moja aweze kunyenyekea mbele Yake

na kutambua kwamba Yeye ni yule anayetosheleza kuwepo kwa binadamu

na kuruzuku maisha ya viumbe vyote.

Muumba pekee ndiye aliye na huruma kwa wanadamu hawa.

Muumba pekee ndiye anayeonyesha mwanadamu huyu huruma na huba.

Muumba pekee ndiye anayeshikilia huba ya kweli, isiyovunjika kwa mwanadamu huyu,

huba ya kweli, isiyovunjika kwa mwanadamu huyu.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp