Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 226

10/08/2020

Natumia mamlaka Yangu duniani, Nikidhihirisha kazi Yangu yote. Yote yaliyo katika kazi Yangu yanajitokeza duniani; mwanadamu hajawahi, duniani, kuweza kuufahamu mwendo Wangu mbinguni, wala kutafakari kabisa mizunguko na njia za Roho Wangu. Wanadamu wengi wanaelewa tu maelezo madogo yaliyo nje ya roho, bila kuweza kuelewa hali halisi ya roho. Matakwa Yangu kwa binadamu hayatoki kwa Mimi wa mbinguni Nisiye dhahiri, ama kwa Mimi wa dunia Nisiyekadiriwa: Natoa matakwa ya kufaa kulingana na kimo cha mwanadamu. Sijawahi kumweka yeyote kwa matatizo, wala Sijawahi “kukamua damu ya mtu yeyote” ili kujiridhisha: Inaweza kuwa kwamba matakwa Yangu yamezuiwa na masharti haya pekee? Kwa viumbe lukuki duniani, ni yupi asiyetii tabia za maneno yaliyo mdomoni Mwangu? Ni yupi kati ya viumbe hawa, wanaokuja mbele Yangu, hajachomwa kabisa kupitia maneno Yangu na moto Wangu unaochoma? Ni yupi kati ya viumbe hawa anayethubutu kujigamba mbele Yangu? Ni yupi kati ya viumbe hawa hainami mbele Yangu? Mimi ni Mungu anayelazimisha tu ukimya kwa viumbe? Kwa mambo lukuki katika uumbaji, Nachagua yale yanaoridhisha nia Yangu; kwa wanadamu lukuki, Nawachagua wale wanaotunza roho Yangu. Nachagua bora zaidi kwa nyota zote, hivyo Naongeza mwangaza hafifu kwa ufalme Wangu. Natembea duniani, Nikitawanya harufu Yangu nzuri kila mahali, nami Naacha umbo Langu kila mahali. Kila pahali panatingika kwa mvumo wa sauti Yangu. Watu kila mahali wanadumu kwa hamu ya mambo waliyozea ya urembo wa mandhari ya jana, kwani binadamu wote wanakumbuka siku za nyuma …

Binadamu wote wanatamani kuona uso Wangu, lakini Nishukapo Mwenyewe duniani, wote wanakirihishwa na ujio Wangu, wote wanaufukuza mwangaza usije, kana kwamba Mimi ni adui ya mwanadamu mbinguni. Mwanadamu ananisalimu na mwangaza wa kujikinga machoni mwake, na daima anabaki katika tahadhari, akihofia sana kwamba Naweza kuwa na mipango mingine kwake. Kwa sababu binadamu wananiona kama rafiki asiyejulikana, wanahisi kwamba Nina nia ya kuwaua bila kujali. Katika macho ya mwanadamu, Mimi ni adui wa mauti. Baada ya kuonja joto Langu katikati ya msiba, mwanadamu hata hivyo bado hafahamu pendo Langu, na bado ameamua kunifukuza na kunikaidi. Mbali na kujinufaisha na yeye kuwa katika hali hii ili kuchukua hatua dhidi yake, Namfunika mwanadamu na joto la kumbatio, Najaza mdomo wake na utamu, na kuweka chakula anachohitaji tumboni mwake. Lakini, wakati hasira Yangu ya ghadhabu inapotingiza milima na mito, Sitamtawaza mwanadamu aina mbalimbali za msaada, kwa sababu ya woga wake. Wakati huu, Nitakuwa na ghadhabu, Nikiwanyima viumbe hai fursa ya kutubu na, kuachana na matumaini yote ya mwanadamu, Nitasambaza adhabu anayostahili sana. Wakati huu, radi na umeme vinang’aa ghafla na kunguruma, kama mawimbi ya bahari yakisonga kwa hasira, kama milima elfu kumi ikigonga chini. Kwa ajili ya uasi wake, mwanadamu anaangushwa na radi na umeme, viumbe wengine wanafutwa katika milipuko ya radi na umeme, ulimwengu mzima unazorota ghafla katika machafuko, na uumbaji huwezi kupata pumzi muhimu ya uhai. Majeshi lukuki ya binadamu hayawezi kutoroka kishindo cha radi, katikati ya nuru ya ghafla ya umeme, wanadamu, makundi mengi sana, wanaanguka ndani ya mto unaobubujika haraka, kutokomezwa na mafuriko yanayotiririka chini kutoka milima. Ghafla, katika pahala pa mwanadamu pa kimbilio panakutana dunia ya wanadamu. Maiti wanasongasonga juu ya bahari. Binadamu wote wanaenda mbali nami kwa sababu ya ghadhabu Yangu, kwani mwanadamu amekosa dhidi ya kiini cha Roho Wangu, uasi wake umenichukiza Mimi. Lakini, mahali ambapo hakuna maji, wanadamu wengine bado wanafurahia, wakicheka na kuimba, ahadi ambazo Nimewapa.

Binadamu wote wanapotulia, Natoa kimulimuli cha mwangaza mbele ya macho yao. Hapo, wanadamu wanakuwa na uwazi wa akili na uangavu wa jicho, na wanakoma kuwa na nia ya kukimya; hivyo, hisia ya kiroho inakusanywa ndani ya mioyo yao mara moja. Wakati huu, binadamu wote wanafufuka. Wakiweka kando malalamiko yao, wanadamu wote wanakuja mbele Yangu, baada ya kushinda nafasi nyingine ya kusalimika kupitia maneno Ninayotangaza. Hii ni kwa sababu wanadamu wote wanataka kuishi duniani. Lakini nani miongoni mwao amewahi kuwa na nia ya kuishi kwa ajili Yangu? Nani miongoni mwao amewahi kufichua mambo mazuri ndani yake kunipa furaha? Nani miongoni mwao amewahi kugundua harufu ya kuvutia Kwangu? Wanadamu wameumbwa kwa vitu hafifu na visivyotakaswa: Nje, wanaonekana kuangaza macho, lakini kwa nafsi zao muhimu hawanipendi kwa dhati, kwa sababu ndani ya nafasi ya kina cha moyo wa binadamu hakujawahi kuwa hata na kiasi kidogo cha Mimi. Mwanadamu anakosa sana: Kumlinganisha nami Mwenyewe, ingeonekana kwamba tuko mbali sana kama dunia kutoka kwa mbingu. Lakini, hata hivyo, Simshambulii mwanadamu katika sehemu zake dhaifu na zenye kasoro, wala Simcheki kudharau upungufu wake. Mikono Yangu imekuwa ikifanya kazi duniani kwa maelfu ya miaka, na wakati huo wote macho Yangu yamelinda binadamu wote. Lakini Sijawahi kuchukulia mzaha maisha ya binadamu hata mmoja kana kwamba ni kitu cha kuchezea. Nachunguza damu ya moyo wa mwanadamu, nami Naelewa bei ambayo amelipa. Anaposimama mbele Yangu, Sitamani kujinufaisha na kutokuwa na ulinzi kwa mwanadamu ili kumwadibu, wala kumtawaza vitu visivyohitajika. Badala yake, Nimemtunza tu mwanadamu, na kumpa mwanadamu, wakati huu wote. Kwa hivyo, yote anayofurahia mwanadamu ni neema Yangu, yote ni fadhila inayotoka kwa mkono Wangu. Kwa sababu Niko duniani, mwanadamu hajawahi lazimika kuteseka mateso ya njaa. Badala yake, Namruhusu mwanadamu kupokea kutoka mikono Yangu mambo ambayo anaweza kufurahia, na kumruhusu mwanadamu kuishi ndani ya baraka Zangu. Je, wanadamu wote hawaishi chini ya kuadibu Kwangu? Kama vile milima inavyoshikilia ndani ya vina vyao mambo ya mengi na wingi, na maji katika ukubwa wake vitu vya kufurahisha, je, watu wanaoishi ndani ya maneno Yangu leo wanavyo, hata zaidi, chakula wanachopenda na kuonja? Niko duniani, na mwanadamu anafurahia baraka Zangu duniani. Niachapo dunia nyuma, ambapo ndipo pia kazi Yangu itafika ukamilishaji wake, wakati huo, wanadamu hawatapata tena hisani yoyote kutoka Kwangu kwa sababu ya udhaifu wao.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp