Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 170
04/09/2020
Tabia yote ya Mungu imefichuliwa katika mpango wote wa uongozi wa miaka elfu sita. Haikufichuliwa tu katika Enzi ya Neema, ni katika Enzi ya Sheria tu, na zaidi ya hayo, ni katika wakati huu wa siku za mwisho. Kazi iliyofanywa katika siku za mwisho inawakilisha hukumu, ghadhabu na kuadibu. Kazi ifanywayo katika siku za mwisho haiwezi kuwekwa mbadala wa kazi ya Enzi ya Sheria ama ile ya Enzi ya Neema. Ingawa, hatua zote tatu zinaungana kuwa kitu kimoja na yote ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Kawaida, utekelezaji wa kazi hizi umegawanyishwa katika enzi tofauti. Kazi iliyofanywa katika siku za mwisho inaleta kila kitu mpaka tamati; ile iliyofanywa katika Enzi ya Sheria ilikuwa ya mwanzo; na ile iliyofanywa katika Enzi ya Neema ilikuwa ya ukombozi. Na kuhusu maono ya kazi katika mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita, hakuna anayeweza kupata ufahamu au kuelewa. Maono kama hayo yamebaki kuwa mafumbo kila wakati. Katika siku za mwisho, kazi ya neno pekee inafanyika ili kuukaribisha Wakati wa Ufalme lakini haiwakilishi enzi zile zingine. Siku za mwisho sio zaidi ya siku za mwisho na sio zaidi ya Enzi ya Ufalme, na haziwakilishi Enzi ya Neema au Enzi ya Sheria. Siku za mwisho ni wakati ambapo kazi zote ndani ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita inafichuliwa kwenu. Huku ndiko kufunuliwa kwa siri hiyo. Mafumbo kama hayo hayawezi kufichuliwa na mwanadamu yeyote. Haijalishi mwanadamu ana maarifa makubwa ya Biblia vipi, yanabaki tu kuwa maneno na si kitu zaidi, kwani mwanadamu haelewi kiini cha Biblia. Mwanadamu anaposoma Biblia, anaweza kupokea baadhi ya ukweli, kueleza baadhi ya maneno ama kuchunguza vifungu maarufu na nukuu, lakini hatawahi kuwa na uwezo wa kunasua maana iliyoko katika maneno hayo, kwani yote aonayo mwanadamu ni maneno yaliyokufa pekee, sio matendo ya kazi ya Yehova na Yesu, na mwanadamu hawezi kufumbua mafumbo ya kazi ya aina hiyo. Kwa hivyo, fumbo la mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita ni fumbo kuu, iliyofichwa zaidi na isiyoshawishika kwa mwanadamu. Hakuna anayeweza kuelewa moja kwa moja mapenzi ya Mungu, ama, Mungu Mwenyewe aeleze na kumfichulia mwanadamu, vinginevyo, yatabaki kuwa mafumbo milele kwa mwanadamu na kubaki mafumbo yaliyofungwa milele. Usiwajali wale walio katika ulimwengu wa kidini; kama hamngeambiwa leo, pia nyinyi hamngeweza kuelewa. Kazi hii ya miaka elfu sita ni ya fumbo zaidi kuliko unabii wote wa manabii. Ni fumbo kuu zaidi tangu uumbaji, na hakuna nabii wa awali ambaye amewahi kuweza kulielewa, kwani fumbo hili hufumbuliwa tu katika enzi ya mwisho na kamwe halijawahi kufichuliwa hapo awali. Mkielewa fumbo hili na muweze kulipokea kwa ukamilifu, wale watu wote wa kidini watashindwa kwa fumbo hili. Hili pekee ndilo kuu zaidi ya maono, lile ambalo mwanadamu hutamani sana kulielewa lakini pia lile ambalo si wazi zaidi kwake. Mlipokuwa katika Enzi ya Neema, hamkujua kazi ambayo ilifanywa na Yesu wala ile ambayo ilifanywa na Yehova. Watu hawakuelewa chochote kuhusu kwa nini Yehova alitangaza sheria, kwa nini Aliwaambia watu wazitii sheria au kwa nini ilikuwa lazima kwa hekalu kujengwa, na sembuse watu kuelewa kwa nini Waisraeli waliongozwa kutoka Misri hadi jangwani na kisha hadi Kanaani. Ni mpaka siku hii ndipo mambo haya yamefichuliwa.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video