Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 161

01/07/2020

Katika Enzi ya Neema, Yesu pia Alinena mengi na kufanya kazi nyingi. Alikuwaje tofauti na Isaya? Alikuwaje tofauti na Danieli? Je, Alikuwa nabii? Ni kwa nini inasemekana kwamba Yeye ni Kristo? Kuna tofauti gani baina yao? Wote walikuwa wanadamu walionena maneno, na maneno yao yalionekana sawa kwa wanadamu. Wote walinena na kufanya kazi. Manabii wa Agano la Kale walitoa unabii, na vivyo hivyo, pia na Yesu. Ni kwa nini iwe hivi? Tofauti hapa inapatikana katika aina ya kazi zao. Ili kutambua suala hili, huwezi kuangazia asili ya mwili na hufai kuangazia upurukushani wa maneno ya mtu. Daima ni sharti kwanza uangazie kazi ya mtu na athari inazoacha kwa mwanadamu. Unabii uliotolewa na Isaya wakati ule, haukuongeza kitu katika uzima wa mwanadamu, na ujumbe uliopokelewa na watu kama Danieli ulikuwa tu unabii na si njia ya uzima. Ingekuwa si kuonekana moja kwa moja kwa Yehova, hakuna ambaye angelifanya hiyo kazi, kwani haiwezekani kwa wanadamu. Yesu pia Alisema mengi, lakini maneno yake yalikuwa njia ya uzima ambayo kwayo mwanadamu angepata njia ya kutenda. Hii ni kusema kuwa, kwanza, Yeye Angeukimu uzima wa mwanadamu, kwa kuwa Yesu ni uzima; pili, Angeweza kuugeuza upotovu wa mwanadamu; tatu, kazi Yake ingeweza kuifuata ile ya Yehova ili kuendeleza enzi; nne, Angeweza kutambua mahitaji ya mwanadamu kwa ndani na kufahamu anachokosa mwanadamu; tano, Angeweza kuanzisha enzi mpya na kutamatisha enzi ya zamani. Ndiyo maana Anaitwa Mungu na Kristo; Yeye si tofauti na Isaya tu; bali pia na manabii wote. Chukua Isaya kama ulinganisho wa kazi za manabii. Kwanza, asingeweza kuukimu uzima wa mwanadamu; pili, asingeweza kuanzisha enzi mpya. Alikuwa akifanya kazi chini ya uongozi wa Yehova wala si kuanzisha enzi mpya. Tatu, alichokizungumza yeye mwenyewe kilikuwa nje ya ufahamu wake. Alikuwa akipata ufunuo moja kwa moja kutoka kwa Roho wa Mungu, na wengine wasingeelewa hata baada ya kuusikiliza ufunuo huo. Haya machache yanatosha kuthibitisha kuwa kazi yake haikuwa zaidi ya unabii, si zaidi ya kazi iliyofanywa kwa niaba ya Yehova. Hata hivyo asingeweza kumwakilisha Yehova kikamilifu. Alikuwa mtumishi wa Yehova, chombo katika kazi ya Yehova. Aidha alikuwa anafanya kazi katika Enzi ya Sheria tu na katika upeo wa kazi ya Yehova; hakufanya kazi nje ya Enzi ya Sheria. Kwa upande mwingine, kazi ya Yesu ilikuwa tofauti. Alivuka mipaka ya kazi ya Yehova; Alifanya kazi kama Mungu mwenye mwili na kupitia mateso ili amkomboe mwanadamu. Hii ni kusema kuwa Alifanya kazi mpya nje ya ile iliyofanywa na Yehova. Huu ulikuwa mwazo wa enzi mpya. Jambo jingine ni kuwa Aliweza kuyazungumzia mambo ambayo mwanadamu asingeweza kupata. Kazi Yake ilikuwa kazi ndani ya usimamizi wa Mungu na ilijumuisha wanadamu wote. Hakufanya kazi miongoni mwa watu wachache tu, na wala kazi yake haikuwa kuwaongoza watu wachache tu. Kuhusu jinsi Mungu Alivyopata mwili kuwa mwanadamu, jinsi Roho alivyopewa ufunuo wakati ule, na jinsi Roho alivyomshukia mwanadamu kufanya kazi, haya ni mambo ambayo mwanadamu hawezi kuona au kugusa. Haiwezekani kabisa ukweli huu kuwa thibitisho kuwa Yeye ni Mungu mwenye mwili. Kwa sababu hii, tofauti inaweza kupatikana tu kwenye maneno na kazi ya Mungu ambayo ni mambo dhahiri kwa mwanadamu. Hili tu ndilo halisi. Hii ni kwa sababu masuala ya Roho hayaonekani kwako na yanafahamika wazi na Mungu Mwenyewe peke yake, wala hata Mungu kuwa mwili hafahamu yote; unaweza kuthibitisha kama Yeye ni Mungu kutokana na kazi Aliyoifanya tu. Kutokana na kazi Yake, inaweza kuonekana kuwa, kwanza, Anaweza kufungua enzi mpya; pili, Yeye Ana uwezo wa kuyaruzuku maisha ya mwanadamu na kumwonyesha mwanadamu njia ya kufuata. Hii inatosha kuthibitisha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe. Angalau kazi Aifanyayo yaweza kumwakilisha kikamilifu Roho Mtakatifu wa Mungu na kutokana na kazi hiyo inaonekana kuwa Roho wa Mungu yupo ndani yake. Kwa kuwa kazi iliyofanywa na Mungu katika mwili ilikuwa kuanzisha enzi mpya, kuanzisha kazi mpya, na kuanzisha na kufungua mazingira mapya, haya mambo machache tu yanatosha kuthibitisha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe. Hili kwa hivyo linamtofautisha na Isaya, Danieli, na manabii wengine wakuu. Isaya, Danieli na wengine wote walikuwa ni watu walioelimika na kustaarabika vilivyo; walikuwa watu wa kipekee chini ya uongozi wa Yehova. Mwili wa Mungu mwenye mwili pia ulikuwa na utambuzi na haukupungukiwa na akili ila ubinadamu wake ulikuwa wa kawaida. Alikuwa mwanadamu wa kawaida na jicho la mwanadamu lisingeweza kubaini ubinadamu wowote wa pekee kumhusu au kugundua kitu chochote katika ubinadamu Wake tofauti na wa wale wengine. Kamwe hakuwa kabisa wa kimiujiza au wa kipekee na hakuwa na elimu ya juu, ujuzi au nadharia kupita kiasi. Maisha Aliyoyazungumzia na mienendo yake hakuipata kinadharia, kielimu, kitajriba au kupitia malezi ya kifamilia. Badala yake, ilikuwa kazi ya moja kwa moja kutoka kwa Roho pamoja na uungu kuwa mwili. Ni kwa kuwa mwanadamu ana dhana kuu kumhusu Mungu, na hasa kwa kuwa fikira hizi hutungwa kutokana na vipengele vingi visivyo yakini na kimiujiza hivi kwamba, katika macho ya mwanadamu, Mungu wa kawaida mwenye udhaifu wa kibinadamu, ambaye hawezi kutenda miujiza, kwa hakika si Mungu. Je, si hizi ni fikra potovu za mwanadamu? Mwili wa Mungu mwenye mwili usingekuwa wa kawaida, basi ingesemekanaje kwamba Alipata mwili? Kupata mwili ni kuwa wa kawaida; mwanadamu wa kawaida; Iwapo angekuwa wa kupita uwezo wa binadamu, basi Asingeweza kuwa wa kimwili. Kuthibitisha kuwa Yeye ni wa kimwili, Mungu kuwa mwili alihitaji kuwa na mwili wa kawaida. Hili lilikusudiwa kutimiza umuhimu wa kupata mwili. Hata hivyo, mambo hayakuwa hivyo kwa manabii na wanadamu. Manabii walikuwa wanadamu waliopewa vipawa na kutumiwa na Roho Mtakatifu; machoni mwa mwanadamu, ubinadamu wao ulikuwa wa hali ya juu, walitenda matendo mengi yaliyovuka mipaka ya ubinadamu wa kawaida. Kwa ajili hii mwanadamu aliwachukulia kama Mungu. Sasa ni sharti nyote mlione hili kwa uwazi zaidi, kwani limekuwa jambo ambalo liliwakanganya sana wanadamu wote katika enzi zilizopita. Aidha, kuwa mwili ndicho cha ajabu zaidi kwa vitu vyote, na Mungu katika mwili ni vigumu zaidi kukubaliwa na mwanadamu. Ninachokisema kinasaidia katika kutimiza majukumu yenu na kuelewa muujiza wa kupata mwili. Haya yote yanahusiana na usimamizi wa Mungu, kwa maono. Ufahamu wenu wa hili jambo utakuwa wa faida zaidi kwa kupata ufahamu wa ono, yaani kazi ya usimamizi. Kwa njia hii, mtafahamu zaidi pia wajibu ambao wanadamu mbalimbali wanafaa kutimiza. Japo maneno haya hayawaonyeshi njia moja kwa moja, bado ni msaada mkubwa kwa kuingia kwenu, kwa kuwa maisha yenu ya sasa yamepungukiwa sana na maono na hili litakuwa kikwazo kikubwa kwa kuingia kwenu. Kama hamjaweza kuyafahamu masuala haya, basi hakutakuwa na motisha ya kuuchochea kuingia kwenu. Na ni vipi kazi kama hii yaweza kuwawezesha kutimiza wajibu wenu vyema zaidi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp