Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 182

05/08/2020

Mungu aliviumba viumbe vyote na akaanzisha mipaka kwa ajili yao na miongoni mwao akalea aina zote za viumbe hai. Wakati Alikuwa akilea aina zote za viumbe hai, pia Aliandaa mbinu tofauti kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, hivyo unaweza kuona kwamba binadamu hawana njia moja tu kwa ajili ya kuendelea kuishi. Pia hawana aina moja tu ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi. Hapo kabla tulizungumza juu ya Mungu kuandaa aina mbalimbali za chakula na vyanzo vya maji kwa ajili ya binadamu, kitu ambacho ni muhimu sana kufanya uhai wa binadamu katika mwili kuendelea. Hata hivyo, miongoni mwa binadamu huyu, sio watu wote wanaishi kwa kula nafaka. Watu wana mbinu tofautitofauti za kuendelea kuishi kwa sababu ya tofauti za mazingira ya kijiografia na mandhari. Mbinu hizi za kuendelea kuishi zote zimeandaliwa na Mungu. Hivyo si binadamu wote wanajihusisha na kilimo. Yaani, si watu wote wanapata chakula chao kwa kulima mazao. Hii ni hoja ya tatu ambayo tutakwenda kuizungumzia. Mipaka imetengenezwa kutokana na mitindo mbalimbali ya maisha ya binadamu. Kwa hiyo ni aina nyingine ipi ya mtindo wa maisha ambayo binadamu wanayo? Ni vyanzo gani vingine vya vyakula ambavyo binadamu wanavyo? Kuna aina za msingi kadhaa:

Ya kwanza ni mtindo wa maisha wa uwindaji. Kila mmoja anajua kuhusu hilo, siyo? Watu wanaoishi kwa kuwinda wanakula nini? (Windo.) Wanakula ndege na wanyama wa mwituni. “Windo” ni neno la kisasa. Wawindaji hawaoni kwamba ni mchezo, wanaona kama chakula, kama riziki yao ya kila siku. Kwa mfano, wangepata paa. Wanapopata paa huyu ni sawa tu na mkulima kupata mazao kutoka ardhini. Mkulima hupata mazao kutoka ardhini, na anapoona mazao yake anakuwa na furaha na anahisi amani. Familia haitakuwa na njaa ya mazao ya kula. Moyo wake una amani na anahisi kuridhika. Na mwindaji pia anahisi amani na kuridhika akiangalia kile ambacho amekamata kwa sababu hana haja ya kuwa na wasiwasi tena kuhusu chakula. Kuna kitu cha kula kwa ajili ya mlo unaofuata, hakuna haja ya kuwa na njaa. Huyu ni mtu ambaye anawinda kwa ajili ya kuishi. Ni mazingira ya aina gani wanayoishi? Wengi wa wale ambao hutegemea uwindaji wanaishi katika misitu ya milima; hawalimi au kupanda mazao. Sio rahisi kupata ardhi inayolimika hapo, kwa hiyo wanaishi kwa kutegemea viumbe hai mbalimbali, aina mbalimbali za mawindo. Hii ni aina ya kwanza ya mtindo wa maisha ambao ni tofauti na ule wa watu wa kawaida.

Aina ya pili ni mtindo wa maisha wa ufugaji. Wale ambao wanafuga kwa ajili ya kuishi hawalimi, sasa wanafanya nini? Ikiwa yeyote miongoni mwenu hapa ni mtu wa Mongolia, mnaweza kuzungumza kidogo kuhusu mtindo wenu wa maisha ya kuhamahama. (Kwa sehemu kubwa, tunafuga ng’ombe na kondoo kwa ajili ya kuishi, hatulimi, na msimu wa baridi tunawachinja na kuwala mifugo wetu. Chakula chetu kinatokana haswa na nyama ya ng’ombe na nyama ya kondoo, na tunakunywa chai ya maziwa. Ingawa wafugaji wanatingwa misimu yote minne, lakini wanakula vizuri. Hawapungukiwi na maziwa, bidhaa za maziwa, au nyama.) Chakula cha msingi cha watu wa Mongolia ni kula nyama ya ng’ombe na nyama ya kondoo, kunywa maziwa ya kondoo na ng’ombe, na wanaendesha madume ya ng’ombe na farasi uwandani na upepo kwenye nywele zao, jua usoni pao. Hawana msongo wa mawazo juu ya maisha ya kisasa. Siku nzima wanaona tu upana wa wingu la bluu na tambarare za majani. Wengi wa watu wanaofuga mifugo kwa ajili ya kuishi wanaishi kwenye uwanda wa mbuga na wanaweza kuendelea na mtindo wao wa maisha ya kuhamahama kwa kizazi baada ya kizazi. Ingawa maisha katika uwanda wa mbuga ni ya upweke kidogo, pia ni maisha ya furaha. Si mtindo mbaya wa maisha!

Aina ya tatu ni mtindo wa maisha ya uvuvi. Kuna sehemu ndogo ya binadamu wanaoishi pembezoni mwa bahari au kwenye visiwa vidogo. Wamezungukwa na maji, wakikabiliana na bahari. Na kuna wengine wanaoishi kwenye mashua. Watu hawa hufanya uvuvi kwa ajili ya kuishi. Ni nini chanzo cha chakula kwa wale wanaofanya uvuvi kwa ajili ya kuishi? Ni aina zote za samaki, vyakula vya baharini, na mazao ya baharini, siyo? Wakati Hong Kong ilikuwa ni kijiji kidogo tu cha uvuvi, watu ambao waliishi pale waliweza kuvua kwa ajili ya kuishi. Hawakulima—walikwenda kuvua kila siku. Chakula chao cha msingi kilikuwa ni aina mbalimbali za samaki, na vyakula vya baharini. Mara chache waliweza kubadilishana vitu hivi na mchele, unga, na mahitaji ya kila siku. Huu ni mtindo tofauti wa maisha wa watu wanaoishi karibu na maji. Wale wanaoishi karibu na maji wanayategemea kwa ajili ya chakula chao, na uvuvi ni riziki yao. Ni chanzo cha riziki yao vilevile chanzo chao cha chakula.

Licha ya wale ambao hulima kwa ajili ya kuishi, kimsingi kuna aina tatu tofauti za mtindo wa maisha zilizotajwa hapo juu. Licha ya wale ambao wanaishi kwa kutegemea ufugaji, uvuvi, na kuwinda, idadi kubwa ya watu hulima kwa ajili ya chakula. Na watu wanaolima kwa ajili ya kuishi wanahitaji nini? Wanahitaji udongo. Wao wanategemea kupanda mazao kwa vizazi na kupata chakula chao kutoka ardhini. Haijalishi wanapanda mbogamboga, matunda au nafaka, wote wanapata mahitaji yao ya kila siku kutoka ardhini.

Masharti ya msingi kwa mitindo tofauti ya maisha ya binadamu ni yapi? Je, hayahitaji utunzaji wa msingi wa mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi? Hii ni sawa na kusema, ikiwa wawindaji wangepoteza misitu ya milima au ndege na wanyama, basi wasingekuwa tena na riziki yao. Hivyo ikiwa watu ambao wanategemea uwindaji wangepoteza milima ya misitu na wasiwe tena na ndege na wanyama, wasingekuwa tena na chanzo cha riziki yao, basi mwelekeo wa aina hiyo ya mbari ungechukua na mahali watu wa aina hii wangeelekea ni kiwango kisichojulikana, na wangeweza pia tu kutoweka. Na wale ambao wanafuga kwa ajili ya riziki yao hutegemea nini? Kile ambacho kweli wanakitegemea si mifugo yao, lakini ni mazingira ambayo mifugo wao wanaendelea kuishi—uwanda wa mbuga. Kama kusingekuwa na uwanda wa mbuga, wangelishia wapi mifugo wao? Kondoo na ng’ombe wangekula nini? Bila mifugo, watu wanaohamahama wangekuwa na riziki gani? Wasingekuwa na riziki. Bila chanzo cha riziki yao, watu hawa wangekwenda wapi? Kuendelea kuishi kungekuwa vigumu sana; wasingekuwa na maisha ya baadaye. Bila vyanzo vya maji, mito na maziwa yangekauka. Je, samaki hao wote wanaotegemea maji kwa ajili ya maisha yao wangeendelea kuwepo? Samaki hao wasingeendelea kuishi. Je, watu hao ambao wanategemea maji na samaki kwa ajili ya riziki yao wangeendelea kuishi? Ikiwa hawakuwa na chakula, ikiwa hawakuwa na chanzo cha riziki zao, watu hao wasingeweza kuendelea kuishi. Yaani, kama kuna tatizo na riziki zao au kuendelea kwao kuishi, jamii hizo zisingeendelea kuwepo. Zisingeweza kuendelea kuishi, na zingeweza kupotea, kufutiliwa mbali kutoka duniani. Na ikiwa wale ambao wanalima kwa ajili ya riziki yao wangepoteza ardhi yao, kama hawangeweza kupanda vitu, na kupata vyakula vyao kutoka kwa mimea mbalimbali, matokeo yake yangekuwa nini? Bila chakula, je, watu wasingekufa kwa njaa? Ikiwa watu wangekufa kwa njaa, je, aina hiyo ya watu isingefutiliwa mbali? Kwa hiyo hili ni kusudi la Mungu katika kudumisha mazingira mbalimbali. Mungu ana kusudi moja tu katika kudumisha mazingira mbalimbali na mifumo ya ikolojia, kudumisha viumbe hai tofautitofauti ndani ya kila mazingira—ni kulea aina zote za watu, kuwalea watu pamoja na maisha katika mazingira ya kijiografia tofautitofauti.

Ikiwa viumbe vyote vingepoteza sheria zao, visingeishi tena; ikiwa sheria za viumbe vyote zingekuwa zimepotea, basi viumbe hai miongoni mwa viumbe vyote visingeweza kuendelea. Binadamu pia wangepoteza mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo wanayategemea kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ikiwa binadamu wamepoteza hiyo yote, wasingeweza kuendelea kuishi na kuongezeka kizazi baada ya kizazi. Sababu ya binadamu kuendelea kuishi mpaka sasa ni kwa sababu Mungu amewapatia binadamu viumbe vyote kuwalea, kuwalea binadamu kwa namna tofauti. Ni kwa sababu tu Mungu anawalea binadamu kwa namna tofauti ndio maana wameendelea kuishi mpaka sasa, kwamba wameendelea kuishi hadi siku ya leo. Kwa aina hiyo ya mazingira yasiyobadilika kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo ni ya kufaa na yapo katika mpangilio, aina zote za watu duniani, aina zote za jamii zinaweza kuishi ndani ya mawanda yao husika. Hakuna anayeweza kwenda zaidi ya mawanda haya au mipaka hii kwa sababu ni Mungu ambaye ameichora. Kwa nini Mungu aichore kwa namna hii? Hii ni muhimu sana kwa binadamu wote—ni muhimu sana!

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp