Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 153

23/07/2020

Mbinu ambazo Shetani anatumia kuwapotosha watu zinaletea nini binadamu? Kuna chochote chema kuzihusu? (La.) Kwanza, mwanadamu anaweza kutofautisha kati ya mema na mabaya? Unaona, katika dunia hii, awe ni mtu fulani mkubwa ama jarida fulani, yote yatasema kwamba hiki ama kile ni chema ama kibaya, si hayo ni barabara? Si hayo ni sahihi? (La.) Tathmini zao za matukio na watu ni za haki? Kuna ukweli ndani ya tathmini hizi? (La.) Je, dunia hii ama binadamu huu unatathmini vitu vyema na hasi kulingana na kiwango cha ukweli? (La.) Mbona watu hawana uwezo huo? Watu wamesoma maarifa mengi na wanajua mengi kuhusu sayansi, uwezo wao si mkubwa kutosha? Mbona hawawezi kutofautisha kati ya vitu vyema na hasi? Mbona hivi? (Kwa sababu watu hawana ukweli; sayansi na maarifa si ukweli.) Kila kitu Shetani anauletea binadamu ni uovu na upotovu na hakina ukweli, uhai, na njia. Na uovu na upotovu ambao Shetani anamletea mwanadamu, unaweza kusema kwamba Shetani ana upendo? Unaweza kusema kwamba mwanadamu ana upendo? Watu wengine wanaweza kusema: “Huko sahihi, kuna watu wengi duniani kote wanaosaidia maskini na watu wasio na makazi. Si hao ni watu wazuri? Pia kuna mashirika ya hisani ambayo yanafanya kazi nzuri, si kazi yote wanayofanya ni ya uzuri?” Kwa hivyo tunasema nini kuhusu hayo? Shetani anatumia mbinu na nadharia mbalimbali kumpotosha mwanadamu; huu upotovu wa mwanadamu ni dhana isiyo dhahiri? La, siyo dhahiri. Shetani pia anafanya vitu vingine vya utendaji, na pia anakuza mtazamo au nadharia katika dunia hii na katika jamii. Katika kila nasaba na katika kila kipindi cha historia anakuza nadharia na kuingiza baadhi ya fikira ndani ya wanadamu. Fikira na nadharia hizi polepole zinakita mizizi katika mioyo ya watu, na kisha watu wanaanza kuishi kwa nadharia na fikira hizi; si wanakuwa Shetani bila kusudi? Si watu wako kitu kimoja na Shetani? Wakati watu wamekuwa kitu kimoja na Shetani, ni nini mtazamo wao kwa Mungu mwishowe? Si ni mtazamo sawa ambao Shetani anao kwa Mungu? Hakuna anayethubutu kukubali haya, siyo? Ni ya kutisha sana! Mbona Nasema kwamba asili ya Shetani ni ovu? Hii inaamuliwa na kuchambuliwa kulingana na kile Shetani amefanya na vitu ambavyo Shetani amefichua; si bila ustahili kusema kwamba Shetani ni mwovu. Iwapo Ningesema tu kwamba Shetani ni mwovu, mngefikiri nini? Mngefikiri, “Bila shaka Shetani ni mwovu.” Hivyo nitakuuliza: “Ni kipengele kipi cha Shetani ni ovu?” Ukisema: “Shetani kumpinga Mungu ni uovu,” bado hutakuwa ukizungumza kwa uwazi. Sasa tumesema mambo maalum kwa njia hii; je, mna uelewa kuhusu maudhui maalum ya kiini cha uovu wa Shetani? (Ndiyo.) Sasa kwa kuwa mmekuwa na huu uelewa wa asili ovu ya Shetani, ni kiasi gani mnaelewa kuhusu nyinyi wenyewe? Je, mambo haya yanahusiana? (Ndiyo.) Je, uhusiano huu unawaumiza? (La.) Ni wenye msaada kwenu? (Ndiyo.) Ninaposhiriki kuhusu kiini cha utakatifu wa Mungu, ni muhimu Niwe na ushirika kuhusu kiini ovu cha shetani, ni nini maoni yako? (Ndiyo, ni muhimu.) Mbona? (Uovu wa Shetani unauweka utakatifu wa Mungu katika heshima ya juu.) Je, ndivyo ilivyo? Hii ni sahihi kidogo kwa sababu bila uovu wa Shetani, watu hawatajua kuhusu utakatifu wa Mungu; hii ni sahihi. Hata hivyo, ukisema kwamba utakatifu wa Mungu upo tu kwa sababu ya tofauti yake na uovu wa Shetani, hii ni sahihi? Hii hoja si sahihi. Utakatifu wa Mungu ni kiini kiasilia cha Mungu; hata ingawa Mungu anaufichua kupitia matendo Yake, hili bado ni onyesho asili la kiini cha Mungu na ni kiini kiasilia cha Mungu; daima kimekuwepo na ni cha Mungu Mwenyewe lakini mwanadamu hawezi kukiona. Hii ni kwa sababu mwanadamu anaishi katikati ya tabia potovu ya Shetani na chini ya ushawishi wa Shetani, na hawajui kuhusu utakatifu, sembuse maudhui maalum ya utakatifu wa Mungu. Hivyo, ni muhimu kweli kwamba tushiriki kwanza kuhusu kiini ovu cha Shetani? (Ndiyo, ni muhimu.) Unaona, tumeshiriki kuhusu vipengele vingi vya upekee wa Mungu na hatukutaja kiini cha Shetani, siyo? Watu wengine wanaweza kuonyesha baadhi ya shaka kama, “Unashiriki kuhusu Mungu Mwenyewe, mbona Unazungumza daima kuhusu jinsi Shetani anawapotosha watu na jinsi asili ya Shetani ni ovu?” Umeyaweka mapumzikoni mashaka haya? (Ndiyo.) Uliyawekaje mapumzikoni? (Kupitia ushirika wa Mungu, tulitofautisha kile ambacho ni ovu.) Wakati watu wana utambuzi wa uovu na wakati wana ufafanuzi sahihi wa uovu, wakati watu wanaweza kuona wazi maudhui maalum na udhihirisho wa uovu, chanzo na kiini cha uovu—wakati utakatifu wa Mungu unajadiliwa sasa—watu basi watatambua wazi, ama kuufahamu wazi kama utakatifu wa Mungu, kama utakatifu wa kweli. Nisipojadili uovu wa Shetani, watu wengine wataamini kimakosa kwamba kitu fulani ambacho watu wanafanya katika jamii ama miongoni mwa watu—ama kitu fulani katika dunia hii—kinaweza kuhusiana na utakatifu. Si mtazamo huu ni wa makosa? (Ndiyo.)

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp