Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 138

26/09/2020

Amri ya Yehova Mungu kwa Mwanadamu

Mwa 2:15-17 Naye Yehova Mungu akamchukua mtu huyo, na kumweka ndani ya bustani ya Edeni ili ailime na kuihifadhi. Yehova Mungu akamwamrisha mtu huyo, akisema, Unaweza kula kwa uhuru matunda kutoka miti yote ya bustani: Lakini kutoka mti wa maarifa ya mema na maovu, usiyale: kwa kuwa katika siku ambapo utakula matunda kutoka mti huo bila shaka utakufa.

Nyoka Anamshawishi Mwanamke

Mwa 3:1-5 Sasa nyoka alikuwa mwenye hila kuliko wanyama wote wa mwitu ambao Yehova Mungu alikuwa amewaumba. Naye akamwambia mwanamke, Naam, Mungu amesema, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Naye mwanamke akamwambia nyoka, Tunaweza kula matunda ya miti katika bustani: Mungu amesema, Lakini msile wala kuyagusa matunda ya mti ulio katikati ya bustani, msije mkafa. Naye nyoka akamwambia mwanamke, Bila shaka hamtakufa: Kwa kuwa Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, macho yenu yatafunuliwa, nanyi mtakuwa kama miungu, mkijua mema na maovu.

Hivi vifungu viwili ni dondoo kutoka kwa kitabu kipi cha Biblia? (Mwanzo.) Je, nyinyi nyote mnavijua vifungu hivi viwili? Hiki ni kitu kilichofanyika mwanzoni wakati binadamu kwanza aliumbwa; lilikuwa ni tukio halisi. Kwanza hebu tuangalie ni amri ya aina gani ambayo Yehova Mungu aliwapa Adamu na Hawa, kwani yaliyomo katika amri hii ni muhimu sana kwa mada yetu ya leo. “Yehova Mungu akamwamrisha mtu huyo, akisema….” Endelea kusoma kifungu kifuatacho. (“Unaweza kula kwa uhuru matunda kutoka miti yote ya bustani: Lakini kutoka mti wa maarifa ya mema na maovu, usiyale: kwa kuwa katika siku ambapo utakula matunda kutoka mti huo bila shaka utakufa.”) Amri ya Mungu kwa mwanadamu katika kifungu hiki ina nini? Kwanza, Mungu anamwambia mwanadamu kile anachoweza kula, yakiwa ni matunda ya miti ya aina nyingi. Hakuna hatari na hakuna sumu, yote yanaweza kulika na kulika atakavyo mtu, bila wasiwasi wowote. Hii ni sehemu moja. Sehemu nyingine ni onyo. Onyo hili linamwambia mwanadamu mti ambao hawezi kula tunda kutoka—lazima asile tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Nini itafanyika akifanya hivyo? Mungu alimwambia mwanadamu: Ukilila hakika utakufa. Maneno haya yanaeleweka kwa urahisi? (Ndiyo.) Iwapo Mungu angekwambia jambo hili lakini hukuelewa kwa nini, ungelichukulia kama kanuni ama amri ya kufuatwa? Linapaswa kufuatwa, sivyo? Lakini iwapo mwanadamu anaweza ama hawezi kulifuata, maneno ya Mungu hayaachi shaka. Mungu alimwambia mwanadamu kwa uwazi kabisa kile anachoweza kula na kile asichoweza, na kile kitakachofanyika akila kile hapaswi kula. Umeona tabia yoyote ya Mungu katika haya maneno machache ambayo Alisema? Haya maneno ya Mungu ni ya ukweli? Kuna udanganyifu wowote? Kuna uongo wowote? (La.) Kuna chochote kinachotisha? (La.) Mungu kwa uaminifu, kwa kweli, kwa dhati Alimwambia mwanadamu kile anachoweza kula na kile asichoweza kula, wazi na dhahiri. Kuna maana iliyofichwa katika maneno haya? Maneno haya yanaeleweka kwa urahisi? Je, kuna haja yoyote ya dhana? (La.) Hakuna haja ya kukisia, sivyo? Maana yake ni wazi kwa mtazamo mmoja, na unaelewa punde tu unapoyaona. Ni wazi kabisa. Yaani, kile Mungu anataka kusema na Anachotaka kuonyesha kinatoka katika moyo Wake. Mambo ambayo Mungu anaonyesha ni safi, yanaeleweka kwa urahisi na ni wazi. Hakuna nia za siri ama maana zilizofichwa. Alizungumza moja kwa moja na mwanadamu, Akimwambia kile anachoweza kula na kile asichoweza kula. Hivyo ni kusema, kupitia maneno haya ya Mungu mwanadamu anaweza kuona kwamba moyo wa Mungu ni angavu, kwamba moyo wa Mungu ni wa kweli. Hakuna uwongo kabisa hapa, kukwambia kwamba huwezi kula kile kinacholika ama kukwambia “Ifanye na uone kitakachofanyika” na vitu ambavyo huwezi kula. Anamaanisha jambo hili? (La.) La. Chochote afikiriacho Mungu katika moyo Wake ndicho Anachosema. Nikisema Mungu ni mtakatifu kwa sababu Anaonyesha na kujifichua Mwenyewe ndani ya maneno haya kwa njia hii, unaweza kuhisi kana kwamba Nimefanya jambo lisilokuwa kubwa ama Nimenyoosha ufasiri Wangu mbali kiasi. Kama ni hivyo, usijali, hatujamaliza bado.

Hebu tuzungumze kuhusu “Nyoka Anamshawishi Mwanamke.” Nyoka ni nani? (Shetani.) Shetani anashikilia jukumu la foili katika mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na ni jukumu ambalo hatuwezi kosa kutaja wakati tunaposhiriki utakatifu wa Mungu. Mbona Nasema hivi? Iwapo hujui uovu na upotovu wa Shetani ama asili ya Shetani, basi huna njia ya kumtambua, wala huwezi kujua utakatifu kweli ni nini. Katika mkanganyiko, watu wanaamini kwamba kile anachofanya shetani ni chema, kwa sababu wanaishi ndani ya aina hii ya tabia potovu. Bila foili, bila chochote cha kulinganisha nacho, huwezi basi kujua utakatifu ni nini, hivyo basi ni lazima mada hii itajwe hapa. Hatujatoa mada hii ghafla kutoka mahali popote, ila badala yake kupitia maneno na matendo yake tutaona jinsi Shetani anavyotenda, jinsi anavyopotosha binadamu, aina ya asili yake na jinsi uso wake ulivyo. Basi mwanamke huyu alimwambia nini nyoka? Mwanamke alimweleza nyoka kile Yehova Mungu alikuwa amemwambia. Kwa kufuata alichosema, alikuwa amethibitisha uhalali wa yote ambayo Mungu alikuwa amemwambia? Hangeweza kuthibitisha haya, angeweza? Kama mtu ambaye alikuwa ameumbwa karibuni, hakuwa na uwezo wa kutambua mema kutoka kwa maovu, wala hakuwa na uwezo wa kufahamu chochote karibu naye. Kwa kutathmini maneno aliyomwambia nyoka hakuwa amethibitisha maneno ya Mungu kuwa kweli katika moyo wake; huu ulikuwa mtazamo wake. Hivyo wakati nyoka aliona kwamba mwanamke huyo hakuwa na mtazamo wa uhakika kwa maneno ya Mungu, alisema: “Bila shaka hamtakufa: Kwa kuwa Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, macho yenu yatafunuliwa, nanyi mtakuwa kama miungu, mkijua mema na maovu.” Kuna chochote kibaya na maneno haya? (Ndiyo.) Ni nini kibaya? Mlipomaliza kusoma sentensi hii, mlipata hisia ya nia za nyoka? (Ndiyo.) Nyoka ana nia gani? (Kumjaribu mwanadamu kufanya dhambi.) Anataka kumjaribu mwanamke huyu kumfanya aache kusikiza maneno ya Mungu, lakini Je, aliongea moja kwa moja? (La.) Hakuongea moja kwa moja, kwa hivyo tunaweza kusema kwamba ana ujanja sana. Anaonyesha maana yake kwa njia ya udanganyifu na ya kukwepa ili kufikia malengo anayonuia ambayo anaficha kutoka kwa mwanadamu ndani yake—huu ndio ujanja wa nyoka. Shetani amewahi kuzungumza na kutenda hivi. Anasema “sio kwa uhakika,” bila kuthibitisha kwa njia moja au nyingine. Lakini baada ya kusikia haya, moyo wa huyu mwanamke mjinga uliguswa? (Ndiyo.) Nyoka alifurahia kwa sababu maneno yake yalikuwa na matokeo yaliyotarajiwa—hii ilikuwa nia ya ujanja ya Nyoka. Zaidi ya hayo, kwa kuahidi matokeo ambayo mwanadamu aliamini kuwa mema, alimshawishi, akisema, “siku mtakayokula matunda ya mti huo, macho yenu yatafunuliwa.” Hivyo mwanamke anafikiria: “Kufumbuliwa macho yangu ni jambo zuri!” Bado nyoka kisha anazungumza maneno ambayo binadamu anaamini kuwa mazuri zaidi, maneno yasiyojulikana na mwanadamu, maneno yaliyo na nguvu kubwa ya majaribu juu ya wale wanaoyasikia: “nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na maovu.” Je, maneno haya hayamvutii mwanadamu sana? Ni kama mtu kukwambia: “Uso wako una umbo zuri. Ni mfupi kidogo katika daraja la pua, lakini ukiirekebisha, utakuwa mrembo wa kupindukia!” Kwa mtu ambaye hajawahi kutaka kufanya upasuaji wa mapambo, moyo wake utaguswa kusikia maneno haya? (Ndiyo.) Kwa hivyo maneno haya ni ya kushawishi? Ushawishi huu unakuvutia? Ni wa kujaribu? (Ndiyo.) Je, Mungu husema mambo kama haya? Kulikuwa na dokezo lolote la haya katika maneno ya Mungu tuliyoyaangalia sasa hivi? (La.) Mbona? Je, Mungu husema Anachofikiria katika moyo Wake? Mwanadamu anaweza kuona moyo wa Mungu kupitia maneno Yake? (Ndiyo.) Lakini wakati nyoka alikuwa amesema maneno haya kwa mwanamke, uliweza kuona moyo wake? (La.) Na kwa sababu ya ujinga wa mwanadamu, walishawishiwa kwa urahisi na maneno ya nyoka, walishikwa kwa urahisi, waliongozwa kwa urahisi. Hivyo uliweza kuona nia za Shetani? Uliweza kuona madhumuni nyuma ya kile alichosema? Uliweza kuona njama na mpango wake wa ujanja? (La.) Ni aina gani ya tabia inayowakilishwa na njia ya mazungumzo ya Shetani? Ni aina gani ya kiini ulichoona ndani ya Shetani kupitia maneno haya? Je, ni mwenye kudhuru kwa siri? Pengine juujuu anakupa tabasamu ama kutofichua maonyesho yoyote. Lakini katika moyo wake anahesabu jinsi ya kufikia lengo lake, na ni lengo hili ambalo huwezi kuliona. Kisha unashawishiwa na ahadi zote anazokupa, manufaa yote anayozungumzia. Unayaona kuwa mazuri, na unahisi kwamba kile anachosema ni cha kufaa zaidi, kikubwa zaidi kuliko asemacho Mungu. Wakati haya yanafanyika, je, mwanadamu basi hawi mfungwa mtiifu? (Ndiyo.) Basi mbinu hizi zinazotumiwa na Shetani si za kikatili? Unajikubali kuzama chini. Bila ya Shetani kusongeza kidole, kwa sentensi hizi mbili unafurahia kumfuata na kumtii. Lengo lake limefikiwa. Nia hii si ya husuda? Huu sio uso wa kimsingi kabisa wa Shetani? Kutoka kwa maneno ya Shetani, mwanadamu anaweza kuona nia zake za husuda, kuona uso wake wenye sura mbaya na kiini chake. Sivyo? (Ndiyo.) Kwa kulinganisha sentensi hizi, bila uchambuzi pengine unaweza kuhisi kana kwamba maneno ya Yehova Mungu ni ya kuchusha, ya kawaida na ya wote, kwamba hayastahili kuhangaikiwa kuusifu uaminifu wa Mungu. Tunapochukua maneno ya Shetani na uso wake wenye sura mbaya na kuvitumia kama foili, hata hivyo, je, haya maneno ya Mungu yanabeba uzito mwingi kwa watu wa leo? (Ndiyo.) Kupitia foili hii, mwanadamu anaweza kuhisi kutokuwa na dosari kwa Mungu. Niko sahihi Nikisema hivi? (Ndiyo.) Kila neno analosema Shetani pamoja na nia zake, malengo yake na jinsi anavyoongea—yote yamepotoshwa. Ni nini sifa muhimu ya njia yake ya kuzungumza? Anatumia maneno yasiyo dhahiri kukushawishi bila kukuruhusu kumwona, wala hakuruhusu kutambua lengo lake ni nini; anakuacha uchukue chambo, akikufanya umsifu na kuimba uzuri wake. Hii siyo hila ya daima ya Shetani? (Ndiyo.)

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp