Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hukumu Katika Siku za Mwisho | Dondoo 85

22/10/2020

Ingawa maneno Yangu yanaweza kuwa makali, yote yanasemwa kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, kwa kuwa Ninazungumza tu maneno na sio kuuadhibu mwili wa mwanadamu. Maneno haya humsababisha mwanadamu kuishi katika nuru, kujua kwamba mwanga upo, kujua kwamba mwanga ni wa thamani, hata zaidi kujua jinsi maneno haya yalivyo na manufaa kwa mtu, na kujua kwamba Mungu ni wokovu. Ingawa Nimesema maneno mengi ya kuadibu na hukumu, hayajafanywa kwako katika vitendo. Nimekuja kufanya kazi Yangu, kuzungumza maneno Yangu na, ingawa maneno Yangu yanaweza kuwa magumu, yanasemwa kwa hukumu ya upotovu na uasi wako. Madhumuni Yangu ya kufanya hili yanabaki kumwokoa mtu kutoka kwa utawala wa Shetani, kutumia maneno Yangu ili kumwokoa mwanadamu; Kusudi Langu sio kumdhuru mwanadamu kwa maneno Yangu. Maneno Yangu ni makali ili matokeo yaweze kupatikana kutoka katika Kazi Yangu. Ni katika kufanya kazi kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kujijua na anaweza kujitenga mbali na tabia yake ya uasi. Umuhimu mkubwa zaidi wa kazi ya maneno ni kuwaruhusu watu kuweza kutia katika matendo ukweli baada ya kuuelewa ukweli, kutimiza mabadiliko katika tabia yao, na kutimiza maarifa kuhusu wao wenyewe na kazi ya Mungu. Mbinu za kufanya kazi tu kupitia kwa kuongea ndizo zinazoweza kuleta mawasiliano kuhusu uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu, maneno tu ndiyo yanayoweza kuelezea ukweli. Kufanya kazi kwa njia hii ndiyo mbinu bora zaidi ya kumshinda mwanadamu; mbali na matamko ya maneno, hakuna mbinu nyingine inayoweza kumpatia mwanadamu uelewa wa wazi zaidi wa ukweli na kazi ya Mungu, na hivyo basi katika awamu Yake ya mwisho ya kazi, Mungu anazungumza naye mwanadamu ili kuweza kuwa wazi kwa mwanadamu kuhusu ukweli na siri zote ambazo haelewi, na hivyo basi kumruhusu kufaidi njia ya kweli na uzima kutoka kwa Mungu na kisha kutosheleza mapenzi ya Mungu. Madhumuni ya kazi ya Mungu juu ya mwanadamu ni ili aweze kukidhi mapenzi ya Mungu na yote yamefanywa kumwokoa mwanadamu, kwa hivyo wakati wa wokovu wake wa mwanadamu Yeye hafanyi kazi ya kumwadibu mtu. Wakati wa wokovu wa mwanadamu, Mungu haadhibu maovu au kulipa mema, wala Yeye hafunui hatima ya aina zote za watu. Badala yake, ni baada tu ya hatua ya mwisho ya kazi Yake kukamilishwa ndipo basi Atafanya kazi ya kuadhibu maovu na kulipa mazuri, na kisha basi ndipo Atafunua mwisho wa aina zote za watu. Wale ambao wanaadhibiwa hakika hawataweza kuokolewa, wakati wale waliookolewa watakuwa wale ambao wamepata wokovu wa Mungu wakati wa wokovu Wake wa mwanadamu. Wakati wa kazi ya Mungu ya wokovu, wale wote ambao wanaweza kuokolewa wataokolewa kwa upeo wa juu zaidi, hakuna hata mmoja wao atakayeachwa, kwa kuwa kusudi la kazi ya Mungu ni kumwokoa mwanadamu. Wote ambao, wakati wa wokovu wa Mungu wa mwanadamu, hawawezi kufikia mabadiliko katika tabia zao, wote ambao hawawezi kumtii Mungu kabisa, wote watakuwa walengwa wa adhabu. Hatua hii ya kazi—kazi ya maneno—humwekea wazi mwanadamu njia na siri zote ambazo haelewi, ili mwanadamu aweze kuelewa mapenzi ya Mungu na mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu, ili aweze kuwa katika ile hali ya kutia katika matendo maneno ya Mungu na kutimiza mabadiliko hayo katika tabia yake. Mungu huyatumia maneno tu kufanya kazi Yake, na hawaadhibu watu kwa sababu ni waasi kidogo, kwa sababu sasa ndio wakati wa kazi ya wokovu. Kama kila mtu ambaye alikuwa muasi angeadhibiwa, basi hakuna mtu ambaye angepata fursa ya kuokolewa; wote wangeadhibiwa na kuanguka kuzimuni. Kusudi la maneno ya yanayomhukumu mtu ni kumwezesha kujitambua na kumtii Mungu; sio kwao kuadhibiwa kwa njia ya hukumu ya maneno. Wakati wa kazi ya maneno, watu wengi watafunua uasi wao na kutotii kwao, na wataweka wazi kutotii kwao kwa Mungu mwenye mwili. Lakini Yeye hatawaadhibu watu hawa wote kwa sababu ya hili, badala yake Atawatupa kando wale ambao wamepotoka kabisa na ambao hawawezi kuokolewa. Atautoa mwili wao kwa Shetani, na katika hali kadhaa, kumaliza mwili wao. Wale ambao wanaachwa wataendelea kufuata na kupitia kushughulikiwa na kupogolewa. Ikiwa wanapofuata hawawezi kukubali kushughulikiwa na kupogolewa na wanazidi kupotoka, basi watu hawa watapoteza nafasi zao za wokovu. Kila mtu ambaye amekubali ushindi wa maneno atakuwa na nafasi nzuri ya wokovu. Wokovu wa Mungu wa kila mmoja wa watu hawa huwaonyesha upole Wake mkubwa, kumaanisha kwamba wanaonyeshwa uvumilivu mkubwa. Mradi watu warudi kutokakatika njia mbaya, mradi kama waweze kutubu, basi Mungu atawapa fursa ya kupata wokovu wake. Watu wanapoasi dhidi ya Mungu kwanza, Mungu hana hamu ya kuwaua, lakini badala yake Anafanya yote Anayoweza kuwaokoa. Ikiwa mtu kwa kweli hana nafasi ya wokovu, basi Mungu atamtupa pembeni. Kwamba Mungu si mwepesi wa kumwadhibu mtu ni kwa sababu Anataka kuwaokoa wale wote ambao wanaweza kuokolewa. Yeye huwahukumu, huwapa nuru na kuwaongoza watu tu kwa maneno, na Hatumii fimbo kuwaua. Kutumia maneno kuwaokoa watu ni kusudi na umuhimu wa hatua ya mwisho ya kazi.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp