Wimbo wa Kusifu | Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu (Music Video)

21/10/2019

Mandhari iliyochorwa katika Biblia “Amri ya Mungu kwa Adamu”

ni ya kugusa na yenye kutia moyo.

Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu,

uhusiano kati ya hao wawili ni wa ndani sana tunaanza kuhisi mshangao.

Upendo wa Mungu unaofurika umepewa mwanadamu bure;

Mwanadamu, maasumu na safi, bila ya wajibu wa kumnyima uhuru,

huishi kwa furaha kamili machoni mwa Mungu.

Mungu humtunza mtu, na mtu huishi chini ya mabawa Yake.

Yote ambayo mtu hufanya, maneno yake yote na matendo,

yamefungwa pamoja na Mungu, hayawezi kujitenga.

Kutoka wakati wa kwanza Mungu alipowaumba wanadamu,

Mungu aliwaweka chini ya uangalizi Wake.

Ni uangalizi wa aina gani huo?

Ni jukumu Lake kumlinda mtu na kumchunga mtu.

Anamtumainia mtu kuamini katika, kuamini katika na kuyatii maneno Yake.

Hiki ndicho kitu cha kwanza ambacho Mungu alikitarajia kwa wanadamu.

Akiwa na tumaini hili la kwanza, Mungu aliyasema maneno yafuatayo:

“Matunda ya kila mti wa bustani mwaweza kuyala:

Lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, msiyale,

msiyale:

kwa maana siku mtakapoyala matunda ya mti huo hakika mtakufa.”

Maneno haya rahisi, yakisimamia mapenzi ya Mungu,

yaonyesha kuwa kumjali mtu kulikuwa tayari katika moyo Wake.

Hivyo, kwa maneno haya rahisi, tunaona kilicho moyoni mwa Mungu.

Je, kuna upendo katika moyo Wake? Si kuna utunzaji na dhima?

Upendo na utunzaji wa Mungu ni jambo ambalo linaweza kuonekana na kuhisiwa.

Kama wewe ni mtu wa dhamiri na una ubinadamu,

utajihisi vuguvugu, ukitunzwa na kupendwa,

utajihisi mwenye heri na furaha.

Unapoyahisi mambo haya, utatenda vipi mintarafu ya Mungu?

Utakuwa mwaminifu Kwake?

Upendo wa staha, upendo wa staha hutakua katika moyo wako?

Moyo wako utasogea karibu na Yeye?

Kutokana na haya tunaona, jinsi upendo wa Mungu ulivyo muhimu kwa mtu.

Lakini hata muhimu zaidi kuliko hili ni kwamba

mtu anaweza kuuhisi na kuuelewa upendo wa Mungu.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp