Wimbo wa Dini | Ni Watu Waaminifu Pekee Walio na Mfano wa Binadamu | God Led Me Onto the Right Path of Life

09/10/2018

I

Kwa ajili ya faida niliacha viwango vyote vya mwenendo,

na bila haya nikatumia udanganyifu kutafuta riziki yangu.

Sikujali chochote kuhusu dhamiri au maadili, chochote kuhusu uadilifu au heshima.

Niliishi tu kuridhisha tamaa na uroho wangu vilivyozidi kukua.

Kwa moyo usio na amani, nilitembea katika matope ya dhambi,

bila njia yoyote ya kuepuka giza hii isiyo na mipaka.

Utajiri wa maisha na raha za muda mfupi

hazingeweza kuficha utupu na maumivu ndani ya moyo wangu.

Ni rahisi kuandika neno "mwanadamu."

Lakini kuwa mwaminifu na mwenye kusadikika ni vigumu kuliko ngumu.

Ni nani anayeweza kuniokoa kutoka katika shimo hili la dhambi?

Ni nani anayeweza kuniokoa kutoka katika shimo hili la dhambi?

II

Sauti ya Mungu imeniongoza mbele Yake.

Leo ninaweza kumfuata Mungu na kumtumikia.

Moyo wangu umejaa utamu kutoka kwa kusoma maneno ya Mungu kila siku.

Kwa kuelewa ukweli, sasa nina kanuni za tabia za kibinadamu.

Kila kitu ninachofanya na kusema ni kulingana na maneno ya Mungu.

Kukubali uchunguzi wa Mungu katika mambo yote huufanya moyo wangu uwe mtulivu na wenye amani.

Hakuna udanganyifu, hakuna uongo, ninaishi katika nuru.

Kwa moyo ulio wazi, mimi ni mtu mwaminifu, na ninaishi kwa kudhihirisha mfano wa kibinadamu mwishowe.

Hukumu ya Mungu na kuadibu kumeniokoa,

na kuniwezesha kuzaliwa upya katika maneno ya Mungu.

Mimi nina shukrani milele kwa upendo wa Mungu na kwa wokovu wa Mungu!

Mimi nina shukrani milele kwa upendo wa Mungu na kwa wokovu wa Mungu!

Mimi nina shukrani milele kwa upendo wa Mungu na kwa wokovu wa Mungu!

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp