Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 361

06/10/2020

Asili ya mwanadamu ni tofauti kabisa na kiini Changu, kwa sababu asili potovu ya mwanadamu hutoka kwa Shetani kabisa; asili ya mwanadamu imetengenezwa na kupotoshwa na Shetani. Yaani, mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa uovu na ubaya wake. Mwanadamu hakui katika ulimwengu wa ukweli au mazingira matakatifu, sembuse mwanadamu kuishi katika nuru. Kwa hiyo, haiwezekani kwa mtu yeyote kuwa na ukweli ndani ya asili yake tangu wakati wa kuzaliwa, sembuse mtu kuweza kuzaliwa na kiini kinachomwogopa na kumtii Mungu. Badala yake, watu wana asili ambayo humpinga na kumwasi Mungu, na haipendi ukweli. Asili hii ndilo tatizo Ninalotaka kujadili—usaliti. Usaliti ndicho chanzo cha kila mtu kumpinga Mungu. Hili ni tatizo ambalo linapatikana ndani ya mwanadamu tu, na sio ndani Yangu. Wengine watauliza: Kwa kuwa watu wote wanaishi ulimwenguni jinsi tu Kristo aishivyo, mbona watu wote wana asili ambazo zinamsaliti Mungu, ilhali Kristo hana asili hiyo? Hili ni tatizo ambalo lazima muelezwe wazi.

Msingi wa uwepo wa wanadamu ni kuzaliwa upya kwa nafsi tena na tena. Kwa maneno mengine, kila mtu hupata maisha ya kibinadamu katika mwili nafsi yake inapozaliwa upya. Baada ya mwili wa mtu kuzaliwa, maisha yake huendelea hadi mwili unapofikia vikomo vyake hatimaye, ambao ndio wakati wa mwisho, wakati nafsi inapoliacha ganda lake. Utaratibu huu hujirudia tena na tena, nafsi ya mtu ikija na kwenda mara kwa mara, na kwa hiyo uwepo wa wanadamu unadumishwa. Maisha ya mwili pia ni maisha ya nafsi ya mwanadamu, na nafsi ya mwanadamu hukimu uwepo wa mwili wa mwanadamu. Hiyo ni kusema, maisha ya kila mtu hutoka kwenye nafsi yake, na maisha hayana asili katika mwili. Kwa hiyo, asili ya mwanadamu hutoka kwenye nafsi, si kutoka kwa mwili. Nafsi ya kila mtu tu ndiyo inayojua jinsi alivyopitia majaribu, mateso na upotovu wa Shetani. Mwili wa mwanadamu hauyajui mambo haya. Kwa hiyo, bila kujua, wanadamu huwa waovu zaidi, wachafu zaidi, na wabaya zaidi, wakati umbali kati ya mwanadamu na Mimi unazidi kuwa mkubwa, na maisha yanakuwa yenye giza zaidi kwa wanadamu. Shetani huzishika nafsi za wanadamu kwa nguvu, kwa hiyo, bila shaka, mwili wa mwanadamu pia umemilikiwa na Shetani. Mwili kama huo na wanadamu kama hao wangewezaje kutompinga Mungu? Wangewezaje kulingana naye kiasili? Sababu iliyofanya Nimtupe Shetani chini angani ni kwa sababu alinisaliti. Je, basi wanadamu wanawezaje kutohusishwa? Hii ndiyo sababu usaliti ni asili ya kibinadamu. Ninaamini kwamba mara mnapoielewa fikira hii, pia mnapaswa kukiamini kiini cha Kristo. Mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu ni mwili wa Mungu mwenyewe. Roho wa Mungu ni mwenye mamlaka; Yeye ni mwenye uweza, mtakatifu, na mwenye haki. Vivyo hivyo, mwili Wake pia ni wenye mamlaka, wenye uweza, mtakatifu, na wenye haki. Mwili kama huo unaweza kufanya tu kile ambacho ni cha haki na chenye faida kwa wanadamu, kile ambacho ni kitakatifu, kitukufu na chenye nguvu; Yeye hawezi kutenda jambo lolote ambalo linakiuka ukweli, ambalo linakiuka maadili na haki, sembuse kufanya jambo lolote linaloweza kumsaliti Roho wa Mungu. Roho wa Mungu ni mtakatifu, na kwa hiyo mwili Wake hauwezi kupotoshwa na Shetani; mwili Wake ni wenye kiini tofauti na mwili wa mwanadamu. Kwa maana ni mwanadamu na si Mungu, ambaye anapotoshwa na Shetani; Shetani hawezi kamwe kuupotosha mwili wa Mungu. Kwa hiyo, licha ya ukweli kwamba mwanadamu na Kristo wanaishi katika sehemu sawa, ni mwanadamu tu ndiye anayemilikiwa, anayetumiwa, na anayenaswa na Shetani. Kinyume na hilo, Kristo hapenyeki kabisa na upotovu wa Shetani, kwa sababu Shetani hatawahi kuweza kupanda hadi mahali pa juu zaidi, na hatawahi kuweza kumkaribia Mungu. Leo, nyote mnapaswa kuelewa kuwa ni wanadamu tu, jinsi walivyopotoshwa na Shetani, ndio hunisaliti. Usaliti hautawahi kuwa suala linalomhusisha Kristo hata kidogo.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp