Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 346

26/08/2020

Ikiwa kazi nyingi, na maneno mengi, hayajakuwa na mabadiliko kwako, basi wakati utakapofika wa kueneza kazi ya Mungu hutaweza kufanya kazi yako, na utaaibika na kufedheheshwa. Wakati huo utajisikia kuwa una deni kubwa kwa Mungu, kwamba maarifa yako juu ya Mungu ni juujuu. Usipofuata maarifa ya Mungu leo, Akiwa bado Anafanya kazi, basi baadaye itakuwa umechelewa. Mwishowe hutakuwa na maarifa yoyote ya kuongelea—utawachwa tupu, bila chochote. Ni nini, basi, utakachotumia kupeana uwajibikaji wako kwa Mungu? Je, una uchungu kuangalia Mungu? Unafaa kujitahidi katika shughuli yako sasa, ili mwishowe uweze, kama, Petro, kujua jinsi adabu na hukumu ya Mungu ina manufaa kwa binadamu, na bila adabu na hukumu Yake mwanadamu hawezi kuokolewa, na atazidi kuzama kwenye ardhi chafu, ndani zaidi kwenye tope. Wanadamu wamepotoshwa na Shetani, wamefitini wenyewe kwa wenyewe, wamekuliana njama wenyewe kwa wenyewe, wamepoteza heshima yao kwa Mungu, na uasi wao ni mkubwa sana, dhana zao ni nyingi, na wote ni wa Shetani. Bila adabu na hukumu ya Mungu, tabia potovu ya mwanadamu haiwezi kutakaswa na hangeweza kuokolewa. Kinachoelezwa na Mungu anayefanya kazi katika mwili hasa ndicho kile kinachoelezwa na Roho, na kazi afanyayo inafanyika kulingana na ile ifanywayo na Roho. Leo, kama huna maarifa yoyote juu ya hii kazi, basi wewe ni mpumbavu sana, na umepoteza mengi! Kama hujapata wokovu wa Mungu, basi imani yako ni ya kidini, na wewe ni Mkristo wa dini. Kwa sababu umeshikilia mafundisho yaliyokufa, umepoteza kazi mpya ya Roho Mtakatifu; wengine, wanaofuata upendo wa Mungu, wanaweza kupata ukweli na uhai, ambapo imani yako haiwezi kupata idhini ya Mungu. Badala yake, umekuwa mtenda maovu, mtu afanyaye vitendo vyenye kuharibu na vya chuki, umekuwa kilele cha utani wa Shetani, na mfungwa wa Shetani. Mungu si wa kuaminiwa na mwanadamu, lakini wa kupendwa na yeye, na kufuatwa na kuabudiwa na yeye. Usipomfuata leo, basi siku itakuja ambapo utasema, “Kama ningalimfuata Mungu, na kumkidhi vizuri. Kama ningalibadilisha tabia ya maisha yangu. Najuta kutojiwasilisha kwa Mungu kwa wakati ufaao, na kutotafuta maarifa ya neno la Mungu. Mungu alisema mengi wakati ule; nilikosa vipi kufuata? Nilikuwa mjinga!” Utajichukia mpaka kiwango fulani. Leo, huamini maneno ninayosema, na huyatilii maanani; wakati utakapofika kwa hii kazi kuenezwa, na unaona ukamilifu wake, utajuta, na wakati huo utakuwa bubu. Kuna baraka, ilhali hujui kuzifurahia, na kuna ukweli, ilhali hujui kuufuata. Je, hujiletei dharau? Leo ingawa hatua inayofuata kwa kazi ya Mungu haijaanza, hakuna kitu cha kipekee juu ya mahitaji yanayohitajika kwako na unachoulizwa kuishi kwa kudhihirisha. Kuna kazi nyingi, na ukweli mwingi; Je, hazina maana kujulikana na wewe? Je, adabu na hukumu ya Mungu haitoshi kuamsha roho yako? Je, adabu na hukumu ya Mungu haitoshi kukufanya ujichukie? Umetosheka kuishi katika ushawishi wa Shetani, kwa amani na furaha, na raha kidogo ya kimwili? Je, wewe si mtu wa chini zaidi kati ya watu wote? Hakuna aliye mpumbavu kuliko wale ambao wameona wokovu lakini hawaufuati ili kuupata: Ni watu ambao wanalafua mwili na kufurahia Shetani. Unatumai kwamba imani yako kwa Mungu haitakuwa na changamoto ama dhiki, ama mateso yoyote. Unafuata vile vitu ambavyo havina maana, na huambatanishi faida yoyote kwa maisha, badala yake kuweka mawazo ya fujo kabla ya ukweli. Huna maana! Unaishi kama nguruwe—kuna tofauti gani kati yako, nguruwe na mbwa? Je, hao wasiofuata ukweli na badala yake wanafuata mapenzi ya kimwili, si wote ni wanyama? Hao waliokufa na bila roho si wafu wanaotembea? Maneno mangapi yamenenwa kati yenu? Je, kazi kidogo imefanywa kati yenu? Ni kiasi gani nimetoa kati yenu? Na mbona hujapata chochote? Una nini cha kulalamikia? Je, si ni kweli kuwa hujapata chochote kwa sababu unapenda mwili sana? Na ni kwa sababu mawazo yako ni ya fujo sana? Je, si kwa sababu wewe ni mpumbavu sana? Kama huna uwezo wa kupata baraka hizi, unaweza kumlaumu Mungu kwa kutokukuokoa? Unachofuata ni cha kukuwezesha kupata amani baada ya kumwamini Mungu—watoto wako wawe huru kutokana na magonjwa, ili mme wako apate kazi nzuri, ili mwana wako apate mke mwema, binti wako apate mme anayeheshimika, ili ndume na farasi wako walime shamba vizuri, kwa mwaka wa hali ya anga nzuri kwa mimea yako. Hili ndilo unalolitafuta. Harakati yako ni kuishi kwa starehe, ili ajali isipate familia yako, ili upepo ukupite, ili uso wako usiguswe na changarawe, ili mazao ya familia yako yasipate mafuriko, ili usiguswe na majanga yoyote, kuishi katika mikono ya Mungu, kuishi kwenye kiota chenye joto. Mwoga kama wewe, anafuata mwili kila wakati—je, una moyo, una roho? Si wewe ni mnyama? Nakupa njia ya ukweli bila kukuuliza chochote, ilhali hauifuati. Je, wewe ni wale wamwaminio Mungu? Nahifadhi uhai wa ukweli wa binadamu juu yako, ila hauufuati. Je, una tofauti kati ya nguruwe na mbwa? Nguruwe hawafuati maisha ya binadamu, hawafuati kutakaswa, na hawaelewi maana ya maisha. Kila siku wanapokula na kushiba, wanalala. Nimekupa njia ya ukweli, ila hujaipata: Wewe u mkono mtupu. Je, unakubali kuendelea na maisha haya, maisha ya nguruwe? Umuhimu wa watu hao kuwa hai ni nini? Maisha yako ni ya kudharauliwa na kutoheshimika, unaishi huku ukiwa na uchafu na uzinzi, na hufuati lengo lolote; je, si maisha yako ni ya kutoheshimika kwa yote? Je, una ujasiri wa kumtazamia Mungu? Ukiendelea kuwa na uzoefu wa haya, je, si utakosa kupata chochote? Umepewa njia ya ukweli, lakini kama utaipata ama hapana inategemea na kutafuta kwako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp