Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 330

28/09/2020

Unapoitembea njia ya leo, ufuatiliaji unaofaa zaidi ni wa aina gani? Katika ufuatiliaji wako, unapaswa kujiona kama mtu wa aina gani? Unafaa kujua jinsi unavyopaswa kukabili yote yanayokukumba leo, yawe majaribu ama taabu, ama kuadibu na laana isiyo ya huruma. Unapaswa kuyazingatia kwa uangalifu katika hali zote. Mbona Nasema hili? Nasema hili kwa sababu yanayokukumba leo hata hivyo ni majaribu mafupi yanayotokea tena na tena; huenda huyaoni kuwa yanayosumbua sana kiakili, na hivyo unayaacha mambo yaende mrama, na huyachukulii kuwa rasilmali ya thamani katika ufuatiliaji wa maendeleo. Wewe ni asiyejali kweli! Ni dhahiri kwamba unaifikiria rasilmali hii ya thamani kuwa jambo la muda mfupi; huyathamini haya mapigo makali yanayokuja mara kwa mara—mapigo ambayo ni ya muda mfupi na yanayoonekana kuwa dhaifu kwako—ila unayatazama kwa utulivu, usiyafikirie kwa dhati na kuyachukulia tu kama mapigo ya mara moja. Wewe ni mfidhuli sana! Kwa mashambulio haya makali, mashambulio yaliyo kama dhoruba na yanayokuja mara kwa mara unaonyesha tu uchangamfu; wakati mwingine hata unatabasamu bila hisia, ukifichua jinsi usivyojali—kwani hujawahi kujiwazia mbona unashinda ukipitia “misiba” kama hii. Je, Namtendea mwanadamu bila haki kwa kiasi kikubwa? Je, Natafuta makosa kwako? Ingawa shida zako za akili huenda zisiwe nzito jinsi Nilivyoeleza, kupitia utulivu wako wa nje, tangu zamani umebuni taswira nzuri sana ya dunia yako ya ndani. Hakuna haja ya Mimi kukuambia kwamba jambo la pekee lililofichika katika vina vya moyo wako ni matusi yasiyo adilifu na huzuni inayoonekana kwa shida. Kwa sababu unahisi kwamba si haki hata kidogo kupitia majaribu kama haya, unatoa matusi; majaribu hayo hukufanya uhisi ukiwa wa dunia, na kwa sababu ya hili, unajawa na ghamu. Badala ya kutazama nidhamu na mapigo haya yanayorudiwa kama ulinzi bora kabisa, unayaona kuwa uchokozi wa Mbinguni usio na sababu, ama vinginevyo kama adhabu inayokufaa. Wewe ni mpumbavu sana! Unazifungia nyakati nzuri gizani bila huruma; mara kwa mara unaona nidhamu na mapigo mazuri kuwa mashambulio kutoka kwa adui zako. Huwezi kubadilika kulingana na mazingira yako sembuse kutaka kufanya hivyo kwani huna hiari ya kupata chochote kutoka kwa kuadibu huku kunakorudiwa na unakoona kuwa katili. Hutafuti wala kuchunguza, unakubali tu yale yatakayokujia na kukubali pahali ulipo. Yanayoonekana kwako kuwa marudio makali hayajaubadili moyo wako wala hayajatwaa udhibiti wa moyo wako; badala yake, yanakuchoma moyoni. Unaona “kuadibu huku katili” kuwa adui wako katika maisha haya tu na hujapata chochote. Wewe unajidai sana! Ni mara chache ambapo unaamini kwamba unapitia majaribu kama haya kwa sababu wewe ni duni sana; badala yake, unajiona aliye na bahati mbaya sana, na kusema kwamba Mimi daima hutafuta makosa kwako. Kufikia leo, kwa kweli una kiasi kipi cha maarifa ya kile Ninachosema na kufanya? Usifikiri kwamba una kipaji cha asili, uliye chini kidogo ya mbingu lakini juu sana ya dunia. Wewe si mwerevu zaidi kuliko mtu mwingine yeyote—na hata inaweza kusemwa kwamba wewe ni mpumbavu zaidi kuliko watu wowote duniani walio na mantiki, kwani unajiona sana kuwa bora, na hujawahi kujiona kuwa mtu wa chini; inaonekana kwamba unayachunguza matendo Yangu kwa utondoti kabisa. Kwa kweli, wewe ni mtu ambaye kimsingi hana mantiki, kwa kuwa hufahamu kabisa Nitakachofanya sembuse kutambua Ninachofanya sasa. Kwa hivyo Nasema kwamba wewe hata hulingani na mkulima mzee anayefanya kazi kwa bidii shambani, mkulima ambaye hafahamu maisha ya binadamu hata kidogo na bado anategemeabaraka za Mbinguni wakati anapolima shamba. Huyafikirii maisha yako hata kidogo, hujui chochote chenye sifa sembuse kujijua. Wewe “una hadhi ya juu” sana!

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp