Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 305

10/08/2020

Kila mara mnataka kumwona Kristo, lakini Nawasihi msijipandishe hadhi hivyo; kila mtu anaweza kumwona Kristo, lakini Nasema hakuna ambaye ni wa kufaa kumwona Kristo. Kwa sababu asili ya binadamu imejazwa na uovu, kiburi, na uasi, wakati unapomwona Kristo, asili yako itakuharibu na itakuhukumu hadi kufa. Ushirika wako na ndugu (au dada) huenda usionyeshe mengi kukuhusu wewe, lakini si rahisi hivyo unaposhiriki na Kristo. Wakati wowote, fikira zako zinaweza kukita mizizi, kiburi chako kianze kuchipuka, na uasi wako kuzaa mitini. Unawezaje kufaa kushiriki na Kristo na ubinadamu kama huo? Je, kweli unaweza kumchukua Yeye kama Mungu kila wakati wa kila siku? Je, kweli utakuwa na hali halisi ya utiifu kwa Mungu? Mnamuabudu Mungu mkubwa ndani ya mioyo yenu kama Yehova wakati mnamchukua Kristo anayeonekana kama mwanadamu. Hisia zenu ni duni mno na ubinadamu wenu ni wa hali ya chini! Hamwezi kumfikiria Kristo kama Mungu milele; ni mara chache tu, mnapotaka, ndio mnamshika na kumwabudu kama Mungu. Hii ndiyo sababu Ninasema nyinyi si waumini wa Mungu, lakini kikundi cha washirika ambao wanapigana dhidi ya Kristo. Hata watu ambao huonyesha wema kwa wengine hulipwa, lakini Kristo, ambaye amefanya kazi ya namna hiyo kati yenu, hajapokea upendo wa Mungu au fidia na utii wake. Je, hili si ni jambo la kusikitisha mno?

Inaweza kuwa kwamba katika miaka yako yote ya imani katika Mungu, kamwe hujamlaani mtu yeyote wala kufanya tendo mbaya, lakini katika ushirika wako na Kristo, huwezi kusema ukweli, kutenda kwa uaminifu, au kutii neno la Kristo; basi, Ninasema kwamba wewe ni mtu mbaya na mwovu zaidi katika dunia. Unaweza kuwa mkunjufu na mwaminifu mno kwa jamaa zako, marafiki, mke (au mume), wanao na mabinti, na wazazi, na kamwe huwatumii wengine vibaya, lakini kama huwezi kulingana na kupatana na Kristo, basi hata ukitumia vitu vyako vyote kuwasaidia majirani zako au kulinda vizuri baba yako, mama, na wanakaya, Ningesema kwamba wewe bado ni mwovu, na zaidi ya hayo aliyejaa hila za ujanja. Usifikiri, kwamba wewe unalingana na Kristo kwa sababu tu unapatana na wengine au unafanya baadhi ya matendo mema. Je, unafikiri kwamba nia yako ya huruma inaweza kupata baraka kutoka Mbinguni kwa udanganyifu? Je, unafikiri kwamba matendo machache mema yanaweza kubadilishwa na utii wako? Hakuna hata mmoja wenu anaweza kukubali kushughulikiwa na kupogolewa, na wote wanaona vigumu kukubali ubinadamu wa kawaida wa Kristo, hata hivyo siku zote mnatangaza utiifu wenu kwa Mungu. Imani kama yenu italeta adhabu ya kufaa. Wacheni kujihusisha katika ndoto za ajabu na kutaka kumwona Kristo, kwa maana nyinyi ni wadogo sana katika kimo, kiasi kwamba nyinyi hata hamstahili kumwona. Wakati umeuwacha kabisa uasi wako na unaweza kupatana na Kristo, wakati huo Mungu Atakuonekania kwa kawaida. Iwapo utaenda kumwona Mungu kabla ya kupogolewa au kupitia hukumu, basi bila shaka utakuwa mpinzani wa Mungu na utakuwa katika njia ya kuangamizwa. Asili ya mwanadamu kwa kawaida ina uhasama kwa Mungu, kwa kuwa watu wote wamepotoshwa kabisa na shetani. Hakuna kizuri kinachoweza kupatikana kwa mtu kujaribu kushirikiana na Mungu kutokana na upotovu wake. Vitendo na maneno yake kwa hakika vitafichua upotovu wake kila wakati; na katika kushirikiana na Mungu, uasi wake utafichuka katika vipengele vyote. Binadamu, kwa kutojua anakuja anampinga Kristo, kumdanganya Kristo, na kumtelekeza Kristo; hili litakapofanyika, mwanadamu atakuwa katika hali ya hatari zaidi na, hili likiendelea, atapata adhabu.

Baadhi ya watu wanaweza kuamini kwamba, kama kushirikiana na Mungu ni hatari sana, basi huenda likawa jambo la busara zaidi kukaa mbali na Mungu. Ni nini watu kama hawa wanaweza kupokea? Je, wanaweza kuwa waaminifu kwa Mungu? Hakika, kushirikiana na Mungu ni kugumu sana, lakini hiyo hasa ni kwa sababu mwanadamu amepotoka na si kwa sababu Mungu hawezi kushiriki naye. Ingekuwa bora kwenu kuweka juhudi zaidi kwa ukweli wa kuzijua nafsi zenu. Mbona hamjapata fadhili kwa Mungu? Kwa nini tabia zenu ni chukizo sana Kwake? Kwa nini maneno yenu yanachochea chuki Yake? Punde ambapo mmeonyesha uaminifu kidogo, nyinyi mnajisifu wenyewe, na mnadai malipo kwa ajili ya mchango mdogo; nyinyi huwadharau wengine wakati nyinyi mnaonyesha utiifu kidogo, na kumdharau Mungu baada ya kufanya kazi ndogo. Mnataka utajiri, zawadi na pongezi kwa ajili ya kumpokea Mungu. Nyoyo zenu huumwa wakati mnatoa sarafu moja au mbili; wakati mnatoa kumi, mnataka kubarikiwa na kutendewa kwa heshima. Ubinadamu kama wenu kweli ni wa kukera kuzungumziwa au kusikizwa. Kuna chochote kinachostahili sifa katika maneno na matendo yenu? Wale ambao wanatekeleza wajibu wao na wale wasiofanya; wale ambao huongoza na wale ambao hufuata; wale wanaompokea Mungu na wale wasiompokea; wale wanaotoa na wale wasiotoa; wale wanaohubiri na wale ambao hupokea neno, na kadhalika; watu wote kama hawa hujisifu wenyewe. Je, hamuoni hili likiwa la kuchekesha? Mkijua vyema kwamba mnamwamini Mungu, hata hivyo ninyi hamwezi kulingana na Mungu. Mkijua vyema kutostahili kwenu, mnaendelea bado kujigamba. Je, hamhisi kuwa hisia yenu imepunguka kiasi kwamba hamwezi tena kujizuia? Na hisia kama hii, mnastahili vipi kushirikiana na Mungu? Je, kufikia hapa nyinyi hamjionei hofu? Tabia yenu tayari imepunguka kiasi kwamba hamwezi kulingana na Mungu. Hali ikiwa hivi, je, imani yenu si ya kuchekesha? Imani yenu si ya kipuuzi? Ni jinsi gani utashughulikia maisha yako ya baadaye? Ni jinsi gani utachagua njia ya kutembelea?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp