Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea | Dondoo 482

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea | Dondoo 482

151 |15/09/2020

Kutoka kwa tofauti katika kiini cha Paulo na kiini cha Petro unapaswa kufahamu kuwa wale wote ambao hawafuati uzima wanafanya kazi ya bure! Unamwamini Mungu na unafuata Mungu, na kwa hivyo moyoni mwako ni lazima umpende Mungu. Ni lazima uache tabia yako potovu, lazima utafute kutimiza mapenzi ya Mungu, na ni lazima utekeleze wajibu wako kama kiumbe wa Mungu. Kwa kuwa unamwamini na kumfuata Mungu, unapaswa kutoa kila kitu kwake, na hupaswi kufanya uamuzi au madai ya kibinafsi, na unapaswa kutimiza ukamilishaji wa mapenzi ya Mungu. Kwa kuwa uliumbwa, unapaswa kumtii Bwana aliyekuumba, kwa kuwa wewe huna mamlaka kiasili juu yako mwenyewe, na huna uwezo wa kudhibiti hatima yako. Kwa kuwa wewe ni mtu ambaye anamwamini Mungu, inapaswa utafute utakatifu na mabadiliko. Kwa kuwa wewe ni kiumbe wa Mungu, unapaswa kushika wajibu wako, na kuhifadhi nafasi yako, na ni lazima usivuke mpaka wa wajibu wako. Hii si kwa ajili ya kukuzuia, ama kukukandamiza kupitia mafundisho, bali ndiyo njia ambayo utaweza kutekelezea wajibu wako, na inaweza kufikiwa—na inapaswa kufikiwa—na wote wanaotenda haki. Ukilinganisha kiini cha Petro na kiini cha Paulo, basi utajua jinsi unapaswa kutafuta. Kati ya njia ambazo Petro na Paulo walitembea, njia moja ni ya kufanywa mkamilifu, na nyingine ni njia ya kutolewa katika mashindano; Petro na Paulo wanawakilisha njia mbili tofauti. Ingawa kila moja wao alipokea kazi ya Roho Mtakatifu, na kila mmoja alipata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, na kila mmoja alikubali kile alichokuwa ameaminiwa na Bwana Yesu, tunda lililozaliwa katika kila mmoja wao halikuwa sawa. Mmoja kwa kweli alizaa tunda, na mwingine hukuzaa tunda. Kutokana na kiini cha kila mmoja wao, kazi waliyofanya, hiyo walioonyesha kwa upande wa nje, na hatima yao ya mwisho, unapaswa kuelewa ni njia gani unayopaswa kuchukua, njia ambayo unapaswa kuchagua kuitembea. Walitembelea njia mbili ambazo dhahiri ni tofauti. Paulo na Petro, walikuwa mifano ya kila njia, na kwa hivyo tangu mwanzo walionekana kuwakilisha njia hizi mbili. Je, ni mawazo gani muhimu katika uzoefu wa Paulo, na ni kwa nini yeye hakufaulu? Je, ni pointi gani muhimu katika matukio ya Petro, na ni jinsi gani yeye alishuhudia kufanywa mkalifu? Ukilinganisha kile ambacho kila alijali kuhusu, basi utajua aina hasa ya mtu ambaye Mungu anamtaka, mapenzi ya Mungu ni gani, na tabia ya Mungu, ni mtu wa aina gani ambaye hatimaye atafanywa mkamilifu, na pia aina gani ya mtu hawezi kufanywa mkamilifu, nini tabia ya wale ambao watafanywa wakamilifu, na nini tabia ya wale ambao hawatafanywa wakamilifu—masuala haya ya kiini yanaweza kuonekana katika uzoefu wa Petro na Paulo. Mungu aliumba kila kitu, na hivyo yeye hufanya viumbe wote kuwa chini ya utawala wake, na kujiwasilisha kwenye utawala wake; Yeye ataamuru kila kitu, ili kila kitu kiwe mikononi mwake. Vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, pamoja na wanyama, mimea, mwanadamu, milima na mito, na maziwa—vyote ni lazima vije chini ya utawala Wake. Vitu vyote mbinguni na ardhini lazima zije chini ya utawala Wake. Haviwezi kuwa na hiari yoyote na vyote ni lazima vitii mipango Yake. Hii iliagizwa na Mungu, na ni mamlaka ya Mungu. Mungu huamuru kila kitu, na huagiza na kuainisha kila kitu, ambapo kila kimoja huainishwa kulingana na aina, na kutengewa nafasi zao zenyewe, kulingana na mapenzi ya Mungu. Bila kujali kitu ni kikubwa namna gani, hakuna kitu kinachoweza kumpita Mungu, na vitu vyote ambavyo vinamtumikia mwanadamu aliyeumbwa na Mungu, na hakuna kitu kinachothubutu kumuasi Mungu ama kumdai Mungu. Na kwa hivyo mwanadamu, kama kiumbe wa Mungu, ni lazima atekeleze wajibu wa mwanadamu. Bila kujali iwapo yeye ni bwana au mtawala wa vitu vyote, bila kujali jinsi hadhi ya mwanadamu ni kuu miongoni mwa vitu vyote, bado yeye ni binadamu mdogo anayetawaliwa na Mungu, na si zaidi ya binadamu asiye na umuhimu, kiumbe wa Mungu, na kamwe hatawahi kuwa juu ya Mungu. Kama kiumbe wa Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kumpenda Mungu bila kufanya chaguo lingine kwa kuwa Mungu anastahiki upendo wa mwanadamu. Wale ambao wanatafuta kumpenda Mungu hawapaswi kutafuta faida zozote za kibinafsi au lile ambalo wanatamani binafsi; hii ndiyo njia sahihi kabisa ya ufuatiliaji. Kama kile ambacho unatafuta ni ukweli, kile ambacho unatenda ni ukweli, na kile ambacho unafikia ni badiliko katika tabia yako, basi njia unayopitia ni sahihi. Iwapo utafutacho ni baraka za mwili, na kile unachoweka katika vitendo ni ukweli wa dhana zako mwenyewe, na iwapo hakuna mabadiliko katika tabia yako, na wewe si mtiifu kabisa kwa Mungu katika mwili, na bado unaishi kwenye mashaka, basi unachotafuta bila shaka kitakupeleka kuzimu, kwa kuwa njia ambayo unatembea ni njia ya kushindwa. Iwapo utafanywa mkamilifu ama utatolewa katika mashindano inategemea na harakati yako mwenyewe, ambayo pia ni kusema kuwa mafanikio au kushindwa kunategemea njia ambayo mwanadamu anapitia.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

What a Believer in God Should Pursue

I

Because you are a person that believes in God, you should seek holiness and you should seek change. Look to Peter and Paul. You need to look close to understand it all that all those who do not learn to pursue life, their labor is in vain, their labor is futile. If you believe in God and follow Him, then you must, in your heart, indeed love Him, cast aside your disposition that’s corrupt, and do the duty of God’s creation, with all your heart. Because you are a person that believes in God, you should seek holiness and you should seek change.

II

Since you believe in God and follow Him, you should give your everything to Him. You shouldn’t choose on your own or make demands, but rather work to satisfy all God commands. You should obey who created you, for you have no dominion over you, and that is true that you have no ability to govern and control your own destiny. Because you are a person that believes in God, you should seek holiness and you should seek change. Because you are a person that believes in God, you should seek holiness and you should seek change.

from Follow the Lamb and Sing New Songs

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi