Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 478

18/09/2020

Petro alifanywa mkamilifu kwa kupitia ushughulishaji na usafishaji. Alisema, “Mimi ni lazima nikidhi mapenzi ya Mungu wakati wote. Kwa yote nifanyayo mimi natafuta tu kukidhi mapenzi ya Mungu, na kama mimi ninaadibiwa, au kuhukumiwa, bado nina furaha kufanya hivyo.” Petro alimpa Mungu kila kitu chake, na kazi yake, maneno, na maisha yote yalikuwa yote kwa ajili ya kumpenda Mungu. Alikuwa mtu ambaye alitafuta utakatifu, na alipopitia zaidi, ndivyo upendo wake wa Mungu ndani ya moyo wake ulikuwa mkubwa zaidi. Paulo, wakati huo huo, alifanya tu kazi ya nje, na ingawa alitia bidii katika kazi yake, juhudi zake zilikuwa kwa ajili ya kufanya kazi yake vizuri na hivyo kupata tuzo. Angalijua kuwa hatapokea tuzo, yeye angalikata tamaa katika kazi yake. Kitu ambacho Petro alijali mno ni upendo wa kweli moyoni mwake, na ule ambao ulikuwa wa vitendo na ungeweza kutimizika. Yeye hakujali kuhusu iwapo angepokea tuzo, lakini kuhusu iwapo tabia yake ingebadilishwa. Paulo alijali kuhusu kufanya kazi kwa bidii hata zaidi, yeye alijali kuhusu kazi ya nje na kujitolea, na mafundisho ambayo hayashuhudiwi na watu wa kawaida. Yeye hakujali chochote kuhusu mabadiliko ndani yake na upendo wa kweli wa Mungu. Uzoefu wa Petro ulikuwa kwa ajili ya kupata upendo wa kweli na maarifa ya kweli. Uzoefu wake ulikuwa ili kupata uhusiano wa karibu na Mungu, na kwa kuishi kwa kudhihirisha kwa vitendo. Kazi ya Paulo ilikuwa ni kwa sababu ya ile aliyoaminiwa na Yesu, na ili apate vitu ambavyo alitamani, lakini haya hayakuwa na uhusiano na elimu yake mwenyewe na ya Mungu. Kazi yake ilikuwa tu kwa ajili ya kuepuka kuadibu na hukumu. Kitu ambacho Petro alitafuta kilikuwa ni upendo safi, na Paulo alitafuta taji ya hali ya kuwa mwenye haki. Petro alishuhudia miaka mingi ya kazi ya Roho Mtakatifu, na alikuwa na elimu ya vitendo kuhusu Kristo, na vile vile elimu ya kina kujihusu yeye mwenyewe. Na hivyo, upendo wake wa Mungu ulikuwa safi. Miaka mingi ya usafishaji Ilikuwa Imeinua elimu yake kuhusu Yesu na maisha, na upendo wake ulikuwa upendo usio na masharti, ulikuwa upendo wa hiari, na hakuagiza chochote akitarajia malipo, na wala hakutumainia kuwa na faida yeyote. Paulo alifanya kazi kwa miaka mingi, ilhali hakumiliki elimu kubwa ya Yesu, na elimu yake ya kibinafsi ilikuwa ndogo mno. Yeye kwa kifupi hakuwa na upendo kwa Kristo, na kazi yake na mwendo ambao alikimbia ilikuwa ili apate heshima na taji la mwisho. Kitu ambacho alitafuta kilikuwa taji zuri kabisa, wala si upendo safi. Yeye hakutafuta kikamilifu, lakini alifanya hivyo kwa kutoonyesha hisia; hakuwa anatekeleza majukumu yake, lakini alilazimika katika harakati yake baada ya kukamatwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa hivyo, harakati yake haithibitishi kuwa yeye alikuwa kiumbe wa Mungu kilichokuwa na sifa zinazostahili; ilikuwa ni Petro ambaye alikuwa kiumbe wa Mungu aliyekuwa na sifa zilizostahili na ambaye alitekeleza wajibu wake. Mwanadamu anafikiri kuwa wale wote wanaotoa mchango kwa Mungu wanapaswa kupokea tuzo, na kwamba mchango unavyokuwa mkubwa zaidi, ndivyo mwanadamu anavyosadiki zaidi kuwa atapokea fadhila za Mungu. Kiini cha mtazamo wa mwanadamu ni wa shughuli, na hatafuti kikamilifu kutekeleza wajibu wake kama kiumbe wa Mungu. Kwa Mungu, watu wanavyozidi kutafuta upendo wa Mungu wa kweli na utii mkamilifu kwa Mungu, ambayo pia ina maana kutafuta kutekeleza wajibu wao kama viumbe wa Mungu, ndivyo zaidi wanaweza kupata kibali cha Mungu. Mtazamo wa Mungu ni kudai kwamba mwanadamu arejeshe hadhi na wajibu wake wa awali. Mwanadamu ni kiumbe wa Mungu, na kwa hivyo mwanadamu hapaswi kuvuka mpaka mwenyewe kwa kutoa madai yoyote kwa Mungu, na anapaswa asifanye lolote zaidi ya kutekeleza wajibu wake kama kiumbe wa Mungu. Hatima ya Paulo na hatima ya Petro ilipimwa kulingana na iwapo wangeweza kutekeleza wajibu wao kama viumbe wa Mungu, na wala si kulingana na ukubwa wa michango yao; hatima zao ziliamuliwa kulingana na kile ambacho walitafuta tangu mwanzo, wala si kulingana na kiasi cha kazi waliyofanya, au makadirio ya watu wengine kuwahusu. Kwa hivyo, kutafuta kutekeleza kikamilifu wajibu wa mtu kama kiumbe wa Mungu ndiyo njia ya mafanikio; kutafuta njia ya upendo wa kweli wa Mungu ndiyo njia sahihi kabisa; kutafuta mabadiliko katika tabia ya zamani ya mtu, na upendo safi wa Mungu, ndiyo njia ya mafanikio. Njia kama hii ya mafanikio ndiyo njia ya kurejeshwa kwa wajibu wa awali na vile vile pia kuonekana kwanza kwa kiumbe wa Mungu. Hiyo ndiyo njia ya kurejeshwa, na pia ni lengo la kazi yote ya Mungu kuanzia mwanzo hadi mwisho. Kama harakati ya mwanadamu inatiwa doa na madai badhirifu ya kibinafsi na tamaa isiyo ya akili, basi athari ambayo inatimizwa haitakuwa mabadiliko katika tabia ya mwanadamu. Hii ni kinyume na kazi ya kurejeshwa. Bila shaka siyo kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu, na hivyo inathibitisha kuwa harakati ya aina hii haikubaliki na Mungu. Harakati ambayo haijakubalika na Mungu ina umuhimu gani?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp