Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 443

02/11/2020

Je, mnajua ni nini mnachopaswa kujiandaa nacho? Jambo moja ni maono juu ya kazi, na jambo jingine ni matendo yako. Lazima ufahamu mambo yote mawili. Kama huna maono katika jitihada zako za kufanya maendeleo katika maisha, basi huna msingi. Kama una njia za matendo tu na huna maono hata kidogo, na huna ufahamu wowote wa kazi ya mpango mzima wa usimamizi, basi wewe ni bure. Lazima uelewe ukweli wa kipengele cha njozi, na kwa ukweli kuhusu matendo, unahitaji kupata njia mwafaka za kutenda mara unapozielewa; unahitaji kutenda kulingana na maneno, na uingie kulingana na hali zako. Maono ndiyo msingi, na usipozingatia hili, hutaweza kufuata hadi mwisho. Unapopitia njia hii, ama utapotea au kuanguka chini na kushindwa. Hakutakuwa na njia ya kufanikiwa! Watu ambao hawana maono makubwa kama msingi wao wanaweza tu kushindwa na si kufanikiwa. Huwezi kusimama imara! Je, unajua kuamini katika Mungu ni nini? Je, unajua kumfuata Mungu ni nini? Bila maono, ni njia gani ungeitembea? Katika kazi ya leo, kama huna maono hutaweza kufanywa mkamilifu kamwe. Unaamini katika nani? Kwa nini unamwamini Yeye? Mbona unamfuata Yeye? Je, unaamini kama aina ya mchezo? Je, unashughulikia maisha yako kama aina ya mtu anayechezewa? Mungu wa leo ndiye maono makubwa zaidi. Je, ni kiasi gani Chake unachokijua? Je, ni kiasi gani Chake ambacho umekiona? Je, baada ya kumwona Mungu wa leo, msingi wa imani yako katika Mungu u salama? Je, unafikiri kwamba mradi unafuata katika njia hii iliyovurugika, utapata wokovu? Unafikiri unaweza kuvua samaki katika maji yenye tope? Je, ni rahisi hivyo? Je, ni maoni mangapi yako kuhusu kile ambacho Mungu wa leo anasema umeweka chini? Je, una maono ya Mungu wa leo? Ufahamu wako wa Mungu wa leo umesimamia wapi? Daima wewe huamini kuwa unaweza kumpata Yeye kwa kumfuata tu, kwamba kwa kumuona Yeye, na kwamba hakuna yeyote anayeweza kukukwepa. Usifikiri kwamba kumfuata Mungu ni rahisi sana. Cha muhimu ni kwamba ni lazima umjue Yeye, lazima uijue kazi Yake, na lazima uwe na nia ya kuvumilia shida kwa ajili Yake, uwe na nia ya kutoa maisha yako kwa ajili Yake, na uwe na nia ya kukamilishwa na Yeye. Haya ndiyo maono ambayo unapaswa kuwa nayo. Haitafaidi kama wewe daima unafikiria kufurahia neema. Usifikiri kwamba Mungu yupo tu kwa ajili ya starehe za watu, na kukirimu neema kwa watu. Wewe ulifikiri vibaya! Kama mtu hawezi kuhatarisha maisha yake ili kufuata, ama mtu hawezi kuacha kila mali ya dunia ili kufuata, basi kwa uhalisi hataweza kufuata hadi mwisho. Lazima uwe na maono kama msingi wako. Kama siku ya kupatwa kwako na maafa itakapokuja, unapaswa kufanya nini? Bado ungeweza kufuata? Usiseme kwa wepesi kama utaweza kufuata hadi mwisho. Ni bora kwanza ufungue macho yako wazi kabisa ili uone wakati wa sasa ni upi. Ingawa sasa mnaweza kuwa kama nguzo za hekalu, wakati utakuja ambapo nguzo hizi zote zitatafunwa na funza, na kusababisha hekalu kuanguka, kwa sababu kwa sasa kuna maono mengi sana ambayo mmekosa. Mnachozingatia tu ni dunia zenu wenyewe ndogo, na hamjui njia iliyo ya kutegemewa kabisa, njia iliyo mwafaka zaidi ya kutafuta ni ipi. Hamtilii maanani maono ya kazi ya leo, na hamyashikilii mambo haya mioyoni mwenu. Je, mmefikiria kwamba siku moja Mungu atawaweka katika mahali pasipojulikana? Je, mnaweza kuwazia siku ambayo huenda Nikawapokonya kila kitu, ni kipi kingewakumba? Nguvu yenu siku hiyo ingekuwa vile ilivyo sasa? Je, imani yenu ingejitokeza tena? Katika kumfuata Mungu, lazima myajue maono haya makubwa ambayo ni “Mungu.” Hili ndilo suala muhimu zaidi. Pia, msidhani kwamba katika kuachana na watu wa kidunia ili kuwa watakatifu kwamba nyinyi ni familia ya Mungu. Leo ni Mungu Mwenyewe ambaye anafanya kazi miongoni mwa uumbaji. Ni Mungu aliyekuja miongoni mwa watu kufanya kazi Yake mwenyewe, si kutekeleza kampeni. Miongoni mwenu, hakuna hata wachache ambao wanaweza kujua kwamba kazi ya leo ni kazi ya Mungu aliye mbinguni ambaye amekuwa mwili. Siyo juu ya nyinyi kufanywa watu waliojipambanua wenye vipaji. Badala yake, ni kuwasaidia kujua umuhimu wa maisha ya binadamu, kujua hatima ya binadamu, na kuwasaidia kumjua Mungu na uzima Wake. Unapaswa kujua kwamba wewe ni uumbaji mikononi mwa Muumba. Unachopaswa kufahamu, unachopaswa kufanya, na unavyopaswa kumfuata Mungu—je, huu si ni ukweli unaopaswa kuuelewa? Je, haya si ni maono ambayo unapaswa kuyaona?

Wakati ambapo mtu ana maono ana msingi. Unapotenda kwa msingi wa kanuni hii, itakuwa rahisi zaidi kuingia ndani. Kwa njia hii hutakuwa na wasiwasi punde unapopata msingi wa kuingia ndani, na itakuwa rahisi sana kwako kuingia ndani. Kipengele hiki cha kuyaelewa maono, cha kuielewa kazi ya Mungu ni muhimu. Lazima muwe mmejiandaa na kipengele hiki. Kama hujajiandaa na kipengele hiki cha ukweli, na wewe huongea tu juu ya njia za matendo, hii ni kasoro kubwa. Nimegundua kwamba wengi wenu hamsisitizi kipengele hiki, na wakati unaposikiliza kipengele hiki cha ukweli ni kama tu kusikiliza maneno ya mafundisho. Siku moja huenda ukapoteza. Kuna baadhi ya maneno sasa ambayo huyafahamu na huyakubali; kwa hiyo unapaswa kutafuta kwa uvumilivu, na siku itakuja utakapoelewa. Jiandae kidogo kidogo. Hata kama unaelewa mafundisho machache tu ya kiroho, ni bora kuliko kutoyazingatia. Ni bora kuliko kutoelewa mafundisho yoyote kamwe. Haya yote ni ya kusaidia kwa kuingia kwako, na yataondoa mashaka hayo yako. Ni bora kuliko kujazwa kwako na dhana. Ni bora zaidi kuwa na maono haya kama msingi. Bila kuwa na wasiwasi kamwe, inawezekana kuingia ndani kwa mikogo na majivuno. Kwa nini kujisumbua daima ukifuata kwa kukanganyikiwa kwa njia ya shaka? Je, hiyo si ni kama kuziba masikio yako wakati unaiba kengele? Ni jambo zuri kama nini kuingia katika ufalme kwa mikogo na majivuno! Kwa nini ujawe wasiwasi? Je, si huku hasa kungekuwa ni kupitia mateso? Unapokuwa na ufahamu wa kazi ya Yehova, wa kazi ya Yesu, na wa hatua hii ya kazi, basi utakuwa na msingi. Sasa unaweza kufikiri kwamba ni rahisi sana. Baadhi ya watu husema, “Wakati unapofika na Roho Mtakatifu anaanza kazi hii kubwa, nitaweza kuzungumza kuhusu mambo haya yote. Ukweli kwamba kwa kweli sielewi sasa ni kwa sababu Roho Mtakatifu hajanipatia nuru sana.” Si rahisi sana; sio kwamba huko tayari kuikubali ukweli sasa, na kisha wakati utakapowadia utaitumia kwa ustadi. Si lazima iwe hivyo! Unaamini kuwa sasa umejiandaa vizuri sana, na kwamba haingekuwa shida kuwajibu wale watu wa kidini na wanadhaharia wakuu zaidi, na hata kuwakanusha. Je, ungeweza kweli kufanya hivyo? Je, ni ufahamu upi unaoweza kuuzungumzia na huo uzoefu wako duni tu? Kuwa umejiandaa na ukweli, kupigana vita ya ukweli, na kutoa ushuhuda kwa jina la Mungu si kile unachofikiri ndicho—kwamba mradi Mungu yuko kazini yote yatakamilishwa. Wakati huo labda utatatizwa na swali fulani, na utafadhaishwa. Cha muhimu ni kama uko dhahiri kuhusu hatua hii ya kazi au la, na ni kiasi gani unaielewa. Ikiwa huwezi kuyashinda majeshi ya adui, na wala kuyashinda majeshi ya kidini, basi si wewe ungekuwa bure? Kama umepata uzoefu wa kazi ya leo, ukaiona kwa macho yako mwenyewe na kuisikia kwa masikio yako mwenyewe, lakini mwishowe unashindwa kushuhudia, bado unathubutu kuendelea kuishi? Ungeweza kukabiliana na nani? Usifikiri kwa kawaida sana sasa. Kazi baadaye haitakuwa rahisi kama unavyofikiri itakuwa. Kupigana vita vya ukweli si rahisi au kawaida sana. Sasa unahitaji kujiandaa. Usipokuwa umejiandaa kwa ukweli sasa, wakati utakapowadia na Roho Mtakatifu hafanyi kazi kwa njia ya mwujiza, basi utakuwa umechanganyikiwa.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp