Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 440

12/12/2020

Kwa hivyo mnapopitia shida au kikwazo kidogo, ni yenye manufaa kwenu; kama lingekuwa jambo rahisi kwenu basi mngeangamia, na kisha mngelindwaje? Leo, ni kwa sababu mnaadibiwa, kuhukumiwa, na kulaaniwa ndiyo mnapewa ulinzi. Ni kwa sababu mmeteseka sana ndiyo mnalindwa. Kama sivyo, mngekuwa tayari mmepotoka. Huku si kufanya mambo yawe magumu kwenu kwa makusudi—asili ya mwanadamu ni ngumu kubadili, na lazima iwe hivyo ili tabia zao zibadilishwe. Leo, hamna hata dhamiri au akili ambazo Paulo alikuwa nazo, wala hamwezi hata kujitambua kama yeye. Lazima mushurutishwe kila wakati, na kila wakati lazima muadibiwe na kuhukumiwa ili roho zenu zichangamshwe. Kuadibu na hukumu ndivyo bora kabisa kwa maisha yenu. Na inapolazimu, lazima pia ukweli unaowafikia uadibiwe; ni hapo tu ndipo mtakapotii kikamilifu. Asili zenu ni kana kwamba bila kuadibu na kulaani, hamngetaka kuinamisha vichwa vyenu, hamngetaka kutii. Bila ukweli ulio mbele yenu, hakungekuwa na matokeo. Ninyi ni duni sana na msio na thamani katika tabia! Bila kuadibu na hukumu, itakuwa vigumu kwenu kushindwa, na itakuwa vigumu kwa udhalimu na kutotii kwenu kushindwa. Asili yenu ya zamani imekita mizizi sana. Kama mngewekwa juu ya kiti cha enzi, hamngefahamu urefu wa mbingu na kina cha dunia, sembuse kujua mnakoelekea. Hamjui hata mlikotoka, hivyo mngewezaje kumjua Bwana wa uumbaji? Bila kuadibiwa na kulaaniwa kwa wakati unaofaa leo, siku yenu ya mwisho ingekuwa imeshawadia kitambo. Hiyo ni kando na majaaliwa yenu—je, hayo hayatakuwa katika hatari ya karibu zaidi? Bila kuadibu na hukumu hii ya wakati unaofaa, ni nani anayejua jinsi ambavyo mngekuwa wenye kiburi, au jinsi ambavyo mngekuwa wapotovu. Kuadibu huku na hukumu hii vimewafikisha leo, na vimehifadhi kuwepo kwenu. Kama bado “mngeelimishwa” kwa kutumia njia zile zile kama za “baba” yenu, ni nani ajuaye mngeingia katika ulimwengu upi! Hamna uwezo wa kujidhibiti na kutafakari kujihusu wenyewe hata kidogo. Kwa watu kama ninyi, mkifuata na kutii tu bila kusababisha ukatizaji au usumbufu wowote, malengo Yangu yatatimia. Je, hamfai kufanya vema zaidi katika kukubali kuadibu na hukumu ya leo? Je, mna chaguo gani jingine?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (6)

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp