Wimbo wa Kusifu | Chaguo Lisilo na Majuto (Music Video)

06/05/2020

Wakati ambapo kukamatwa na kuteswa kwa Wakristo na Shetani kunazidi kuwa katili,

jiji linapojawa na tisho la giza, na ninatorokea popote niwezapo,

uhuru unapofungwa katika gereza ya majonzi,

wakati ambapo mwenzi wangu wa pekee ni usiku mrefu wa maumivu,

sitatikisika katika imani yangu katika Mungu,

sitamsaliti Bwana wangu kamwe, Mungu wangu.

Mwenye uweza Mungu wa kweli, moyo wangu ni Wako.

Kufungwa gerezani kunaweza tu kuudhibiti mwili wangu.

Hakuwezi kuzuia nyayo zangu kukufuata.

Hakuwezi kuzuia nyayo zangu kukufuata.

Barabara ya uchungu na yenye mabonde,

nikiongozwa na maneno Yako, siogopi;

nikiandamwa na upendo Wako, moyo wangu unaridhika;

nikiandamwa na upendo Wako, moyo wangu unaridhika.

Mateso ya kuharibu ya pepo wa kishetani yanapozidi kuwa makali sana,

uchungu wa kuunguza unaponipata tena na tena,

wakati uchungu wa mwili wangu uko karibu kufikia kilele chake,

wakati wa mwisho, wakati ambapo maisha yangu yanakaribia kuchukuliwa,

sitajisalimisha kwa joka kubwa jekundu kamwe,

sitakuwa Yuda kamwe, alama ya aibu kwa Mungu.

Mwenye uweza Mungu wa kweli, nitakuwa mwaminifu Kwako hata kufa.

Shetani anaweza tu kunitesa na kuumiza mwili wangu.

lakini hawezi kugusa imani na upendo wangu Kwako,

lakini hawezi kugusa imani na upendo wangu Kwako.

Uzima na kifo vitakuwa chini ya utawala Wako milele.

Nitaacha kila kitu ili kukushuhudia Wewe.

Nikikushuhudia na nimwaibishe Shetani, nitakufa bila malalamiko.

Nikikushuhudia na nimwaibishe Shetani, nitakufa bila malalamiko.

Ni heshima kuu kumfuata Kristo na kufuatilia kumpenda Mungu maishani!

Kwa moyo na roho, ninapaswa kumlipa Mungu;

niko tayari kuachana na yote ili kushuhudia kumhusu Mungu.

Almradi ninaishi, kumpa Mungu maisha yangu yote

ni chaguo ambalo sitajutia kamwe,

ni chaguo ambalo sitajutia kamwe,

ni chaguo ambalo sitajutia kamwe.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp