Wimbo wa Kusifu | Upendo wa Mungu Unauzingira Moyo Wangu

12/09/2018

Jua la haki linainuka Mashariki.

Ee Mungu! Utukufu Wako unajaza mbingu na dunia.

Mpendwa wangu, upendo Wako unauzunguka moyo wangu.

Wale wanaotafuta ukweli—wanampenda Mungu, kila mmoja.

Asubuhi na mapema, ingawa naamka peke yangu,

furaha iko moyoni mwangu ninavyoyatafakari maneno ya Mungu.

Maneno Yake ya upole, kama yale ya mama mwenye upendo; Maneno Yake ya hukumu, makali kama kukaripia kwa baba.

Hakuna kingine duniani ninachopenda, kwa moyo wangu wote ninampenda Mwenyezi Mungu pekee.

Aa, we, aa we,

aa we, aa we.

Hakuna kingine duniani ninachopenda, kwa moyo wangu wote ninampenda Mwenyezi Mungu pekee.

Mapenzi ya Mungu yamefichuliwa—kuwakamilisha wale wanaompenda kweli.

Msio na hatia, mnaobubujikwa na uzima, toneni sifa zenu Kwake.

Dansi ya furaha ni nzuri, rukeni na kucheza karibu na kiti cha enzi.

Kutoka katika pembe nne za dunia, tunakuja, tukiitwa na sauti ya Mungu.

Maneno Yake ya uzima tulipewa sisi, tunatakaswa na hukumu Yake.

Upendo unakuwa wa nguvu zaidi kwa kusafishwa. Ni utamu kufurahia upendo wa Mungu.

Mwenyezi Mungu ni mzuri sana, ninampenda Yeye tu.

Aa, we, aa we,

aa we, aa we.

Mwenyezi Mungu ni mzuri sana, ninampenda Yeye tu.

Aa, we, aa.

Eeh, eeh.

kutoka kwa Mfuate Mwanakondoo na Imba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp