Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Tabia ya Mungu na Kile Anacho na Alicho | Dondoo 233

03/09/2020

Nimeanza kuchukua hatua kuadhibu wale ambao hufanya uovu, wale ambao hushika madaraka, na wale ambao hutesa wana wa Mungu. Kuanzia sasa kuendelea, mkono wa amri Zangu za utawala utakuwa daima juu ya wale wanaonipinga mioyoni mwao. Fahamu hili! Huu ndio mwanzo wa hukumu Yangu, na hakuna huruma itakayoonyeshwa kwa yeyote wala hakuna atakayesamehewa, kwani Mimi ni Mungu asiyependelea ambaye hutenda haki, na ingekuwa vyema kwenu nyote kutambua hili.

Si kwamba Nataka kuadhibu wale ambao hufanya uovu, badala yake ni adhabu inayoletwa kwao na uovu wao wenyewe. Mimi siwi na haraka ya kumwadhibu yeyote, wala Simtendei yeyote bila haki—Natenda haki kwa wote. Kwa hakika Napenda wana Wangu na hakika Nachukia wale waovu wasionitii; hii ndiyo kanuni ya matendo Yangu. Kila mmoja wenu anapaswa kuwa na umaizi wa amri Zangu za utawala. Iwapo sivyo, hamtakuwa na hofu hata kidogo na mtakuwa wazembe mbele Yangu, na hamtajua kile Ninachotaka kutimilisha, kile Ninachotaka kufanya kuwa kamili, kile Ninachotaka kupata ama ufalme Wangu unahitaji mtu wa aina gani.

Amri Zangu za utawala ni:

1. Haijalishi wewe ni nani, ukinipinga Mimi katika moyo wako, utahukumiwa.

2. Kwa wale ambao Nimechagua, watafundishwa nidhamu mara moja kwa sababu ya wazo lolote lisilo sahihi.

3. Nitawaweka wale wasioniamini kwa upande mmoja. Nitawaruhusu wazungumze na kutenda kwa uzembe hadi mwisho kabisa ambapo Nitawaadhibu kabisa na kupambana nao.

4. Kwa wale ambao wananiamini, Nitawatunza na kuwalinda nyakati zote. Nyakati zote Nitawapa uzima kwa kutumia njia ya wokovu. Watu hawa watakuwa na upendo Wangu na hakika hawataanguka ama kupoteza njia yao. Udhaifu wowote ambao wako nao utakuwa wa muda, na kwa hakika Sitaukumbuka.

5. Kwa wale ambao wanaonekana kuamini lakini ambao kwa kweli hawaamini—kumaanisha wale ambao wanaamini kuna Mungu lakini hawamtafuti Kristo, lakini ambao pia hawapingi—watu wa aina hizi ni wa kusikitisha zaidi, na kupitia vitendo Vyangu Nitawafanya waone kwa dhahiri. Kupitia matendo Yangu, Nitawaokoa watu wa aina hizi na kuwarudisha.

6. Wazaliwa wa kwanza ambao walikuwa wa kwanza kukubali jina Langu watabarikiwa! Hakika Nitawapa baraka bora zaidi na mtakuwa na furaha hadi kuridhika kwa mioyo yenu; hakuna atakayethubutu kuizuia. Kila kitu kimetayarishwa kabisa kwa ajili yenu, kwani hii ni amri Yangu ya utawala.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 56

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp