Wimbo wa Injili | Kazi ya Mungu Inaendelea Kuboreshwa

16/03/2020

Kazi ya Mungu inaendelea kuwa bora;

ingawa kusudi linabaki bila kubadilika,

mbinu ya kazi Yake inabadilika daima,

na hivyo pia wale wanaomfuata.

Kadiri ambavyo Mungu anafanya kazi zaidi,

ndivyo anavyozidi mwanadamu kumjua, kikamilifu,

ndivyo tabia ya mwanadamu inavyozidi kubadilika

pamoja na kazi Yake ifaavyo.

Kazi ya Mungu inaendelea kuboreshwa;

Kazi Yake kamwe sio nzee na ni mpya daima.

Yeye kamwe harudii kazi ya zamani,

kazi ambayo haijafanywa awali tu ndiyo Atakayoifanya.

Mungu hadumishi kazi ile ile;

inabadilika kila mara na ni mpya daima.

Ni sawa na Mungu kunena maneno mapya

na kufanya kazi mpya kila siku kwako.

Hii ni kazi ambayo Mungu anafanya;

umuhimu upo katika "ajabu," na "mpya."

"Mungu habadiliki na Yeye atakuwa Mungu daima."

Huu ni msemo ambao hakika ni ukweli.

Kazi ya Mungu inaendelea kuboreshwa;

Kazi Yake kamwe sio nzee na ni mpya daima.

Yeye kamwe harudii kazi ya zamani,

kazi ambayo haijafanywa awali tu ndiyo Atakayoifanya.

Lakini kwa kuwa kazi ya Mungu hubadilika kila mara,

kwa wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu,

na wanadamu wapumbavu wasiojua ukweli,

Wao huishia kuwa wapinzani wa Mungu.

Kiini cha Mungu hakitabadilika kamwe;

Mungu ni Mungu kila mara na kamwe sio Shetani.

Lakini hii haimaanishi kuwa kazi Yake haibadiliki,

na ipo daima kama kiini Chake.

Unasema kuwa Mungu habadiliki kamwe,

lakini utaeleza vipi "sio nzee kamwe, mpya daima"?

Kazi ya Mungu inakua na kubadilika,

Anaonyesha mapenzi Yake

na kufanya yajulikane kwa mwanadamu pia.

Kazi ya Mungu inaendelea kuboreshwa;

Kazi Yake kamwe sio nzee na ni mpya daima.

Yeye kamwe harudii kazi ya zamani,

kazi ambayo haijafanywa awali tu ndiyo Atakayoifanya.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp