Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kupata Mwili | Dondoo 118

01/09/2020

Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii kabisa kwamba mwili wa mwanadamu umeharibiwa ndio maana Mungu akamfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mhusika wa uharibifu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu. Mwanadamu ni kiumbe anayekufa, ni wa mwili na damu, na Mungu ndiye tu Anayeweza kumwokoa mwanadamu. Kwa namna hii, Mungu ni lazima Awe mwili ambao una tabia zinazofanana na mwanadamu ili Aweze kufanya kazi Yake, ili kwamba kazi Yake iweze kupata matokeo mazuri zaidi. Mungu lazima Awe mwili ili Aweze kufanya kazi Yake kwa ufanisi kwa sababu mwanadamu ni wa mwili, na hana uwezo wa kushinda dhambi au kujivua mwili. Ingawa dutu na utambulisho wa Mungu unatofautiana kwa kiasi kikubwa na dutu na utambulisho wa mwanadamu, bado kuonekana Kwake kunafanana na kuonekana kwa mwanadamu, ana umbo la mwanadamu wa kawaida, na anaishi maisha ya mwanadamu wa kawaida, na wale wanaomwona hawawezi kuona tofauti na mtu wa kawaida. Kuonekana huku kwa kawaida na ubinadamu wa kawaida vinatosha kwake kwa ajili ya kufanya kazi yake ya kiungu katika ubinadamu wa kawaida. Mwili wake unamruhusu kufanya kazi Yake katika ubinadamu wa kawaida, na inamsaidia kufanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu, na ubinadamu Wake wa kawaida, aidha, humsaidia kufanya kazi ya wokovu miongoni mwa wanadamu. Ingawa ubinadamu Wake wa kawaida umeleta msukosuko miongoni mwa mwanadamu, msukosuko huo haujaathiri matokeo ya kawaida ya kazi Yake. Kwa ufupi kazi ya ubinadamu Wake wa kawaida ni ya manufaa makubwa kwa mwanadamu. Ingawa watu wengi hawakubali ubinadamu Wake wa kawaida, kazi Yake bado inaweza kuwa ya ufanisi, na matokeo haya yanapatikana kutokana na ubinadamu wake wa kawaida. Kuhusu hili hakuna shaka. Kutokana na kazi Yake ya mwili, mwanadamu anapata vitu mara kumi au dazeni kadha zaidi kuliko mitazamo iliyopo miongoni mwa mwanadamu kuhusu ubinadamu Wake wa kawaida, na mitazamo hiyo hatimaye itamezwa na kazi yake. Na matokeo ambayo kazi Yake imefanikiwa, ambayo ni kusema, maarifa ambayo mwanadamu anayo juu Yake, yanazidi kwa mbali sana mitazamo ya mwanadamu kuhusu Yeye. Hakuna namna ya kufikiri au kupima kazi Anayofanya katika mwili, maana mwili wake si kama wa mwanadamu; ingawa mwonekano wa nje unafanana; dutu yao si sawa. Mwili wake unatoa mitazamo mingi kuhusu Mungu miongoni mwa mwanadamu, bado mwili wake unaweza pia kumruhusu mwanadamu kuwa na maarifa mengi, na anaweza hata kumshinda mwanadamu yeyote mwenye ganda la nje kama lake. Maana Yeye si mwanadamu wa kawaida tu, bali ni Mungu mwenye umbo la nje kama la mwanadamu, na hakuna anayeweza kumwelewa au kumfahamu kikamilifu. Mungu asiyeonekana na kushikika anapendwa na kukaribishwa na wote. Ikiwa Mungu ni Roho tu ambayo haionekani kwa mwanadamu, ni rahisi sana kwa mwanadamu kumwamini Mungu. Mwanadamu anaweza kuzipa uhuru fikra zake mwenyewe, anaweza kuchagua taswira yoyote anayotaka kama taswira ya Mungu ili kujifurahisha mwenyewe na kujifanya mwenyewe awe na furaha. Kwa njia hii, mwanadamu anaweza kufanya chochote kile kinachomfurahisha Mungu wake, na kile ambacho Mungu huyu yuko tayari kukifanya bila wasiwasi. Aidha, mwanadamu huyu anaamini kwamba hakuna ambaye ni mwaminifu zaidi anayejitolea kwa Mungu kuliko yeye, na kwamba wengine wote ni mbwa wa Mataifa, na wasiokuwa watiifu kwa Mungu. Tunaweza kusema kwamba hiki ndicho kinachotafutwa na wale ambao imani yao kwa Mungu ni ya kidhahania na ambayo imejikita katika mafundisho; wanavyovitafuta vinafanana, tofauti ikiwa ndogo tu. Ni kwamba taswira za Mungu katika fikra zao ni tofauti, lakini dutu yao kimsingi inafanana.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp